Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na vijana wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu mkazi Tabora mjini.
Mbali
ya Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni Evodius Justinian wa Buboka,
Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel
Kihawa wa Dodoma, leo wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na
kumwagia tindikali Musa Tesha katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa
Igunga uliofanyika mwaka 2011.
Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.
Kesi
hiyo ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi,
ya Tabora Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali
ukiwakilishwa na Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara Baada
ya kusomewa shitaka hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili
Prof Abdalah Safari, ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela
ulitoa hoja kuiomba mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa
sababu, kwanza mashtaka hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.
Sheria
za uendeshaji wa makosa kama hayo hapa nchini zinadai kuwa mashataka
kama hayo yanapofunguliwa ni lazima ridhaa ya Mkurugenzi wa mashtaka
iwepo. Kwa kuwa ridhaa hiyo haikuwepo, mawakili waliiomba mawakili
kuitupilia mbali kesi hiyo.
Sababu
ya pili iliyotolewa na upande wa Utetezi ilikuwa kwamba maelezo ya
kesi kuwa ni ya ugaidi, yalikuwa hayaonyeshi kuwa ni ya kigaidi tofauti
na makosa mengine ya kawaida kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hivyo
waliiomba Mahakama kutupilia mbali shitaka hilo au lifunguliwe kama
kosa la kawaida.
Na
sababu ya tatu ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai,
sheria inaelekeza kuwa mshitakiwa ashitakiwe katika mahakama yenye
mamlaka na hadhi kama ile waliyopelekwa katika maeneo yale
walikokamatwa. Hivyo mawakili waliiomba mahakama itupilie mbali
shitaka, kwani washitakiwa kama walikuwa na hatia walipaswa kushitakiwa
katika maeneo yao walipokamatwa. Baada ya hoja hizo, Mahakama
iliahirisha kesi hiyo na itatajwa tena Julai 8 mwaka huu Tabora Mjini.
Hii
sio mara ya kwanza kwa viongozi au wafuasi wa chadema kufunguliwa kesi
zinazohusiana na ugaidi, tarehe 18 Machi 2013, Mkurugenzi wa Usalama
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare, la
Ludovick Joseph walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya ugaidi.
Kosa
jingine lililowakambili Lwakatare na Ludovick ni kula njama; kosa
ambalo pia linawakabili washtakiwa wote ambalo ni kinyume na kifungu
cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume
na kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka
2002.
Katika
kosa la tatu, washtakiwa wote wawili wanadaiwa kufanya mkutano wa
kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha
Sheria ya Kuzuia ugaidi.
Wakili
wa serikali alidi kuwa washitakiwa wote Desemba 28 Mwaka jana
walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyara
Msaki kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi.
Pamoja
na tuhuma hizo, 8 Mei, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimfutia
mashitaka matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.
Katika
uamuzi huo Jaji Lawrance Kaduri akitoa uamuzi huo alisema ulitokana
kukubaliana na hoja ya mawakili wa Lwakatare; Tundu Lissu, Peter
Kibatara na Mabere Marando na kusema kuwa.
“Baada
ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama inatoa amri ya
kumfutia Lwakatare mashitaka matatu, yaani kosa la pili, tatu na la nne
kwa sababu Jamhuri imeshindwa kuonesha maelezo yanayotesheleza
kumshitaki Lwakatare kwa kesi ya ugaidi.
“Naamuru
jalada la kesi ya msingi lilirudishwe Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya
mshitakiwa kuendelea kushitakiwa kwa kosa moja la kula njama ambalo
linaangukia katika sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002,” alisema
Jaji Kaduri
Imechotwa: Habari Mseto Blog
No comments:
Post a Comment