Thursday, July 04, 2013

FBI WAKAGUA OFISI YA KOVA KWA MBWA...!!!

 
 
Ofisa mmoja wa Usalama wa Marekani (FBI), akiwa na mbwa jana aliingia Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kufanya ukaguzi.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya msafara wa magari ya Marekani kupita yakitokea Ikulu kwenda Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kumlaki Rais Barack Obama.

Polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema ofisa huyo aliingia na mbwa hadi maeneo ya mapokezi, lakini muda mfupi walitoka.

“Walikwenda moja kwa moja mapokezi wakafanya ukaguzi, kisha wakatoka nje ya jengo na kama hiyo haitoshi, ofisa huyo akiwa na mbwa alikwenda sehemu ya kuegesha magari yenye kesi na yale ya kawaida na kuanza kufanya ukaguzi, baada ya hapo waliondoka,” alisema polisi huyo na kuongeza:

“Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale, lakini hili la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo Kikuu.”

Hata hivyo, usalama kwenye vituo vingi ikiwamo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusu Nyerere, vilikuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa makachero wa Marekani.
Na Mwananchi.

HATIMAYE SWANSEA CITY YAKAMILISHA USAJILI WA JONJO SHELVEY

Kiungo Mpya wa timu ya Swansea City ya Uingereza Jonjo Shelvey

Hatimaye klabu ya Swansea City imekamilisha zoezi la Kumsajili kiungo wa zamani wa liverpool Jonjo Shelvey kwa dau la Pauni Milioni 5. Jonjo Shelvey amesajiliwa na timu ya swansea akitokea timu ya liverpool.

Kinda huyo mpya wa Swansea Mwenye umri wa Miaka 21 ameweka saini yake na kukubali kufunga ndoa ya miaka minne baada ya kukubali masharti yake binafsi na kufuzu kwa vipimo vya afya na hatimaye atakuwa kwenye dimba la libert kwa miaka minne.

Safari ya Jonjo katika Soka ilianza pale alipokuwa akiichezea timu ya Charlton kabla hajaamia liverpool kwa dau la Pauni Milioni 1.7 mnamo mwaka 2010.

Baada ya kumaliza kutia saini katika mkataba wake wa miaka minne na timu ya Swansea Jonjo Shelvey aliandika katika Ukurasa wake wa twitter kuwa "napenda kuwashukuru kila mmoja na mashabiki wote wa liverpool kwa msaada wake na pia nitawamiss kweli hakika hii ni daraja la kwanza"

"Nitakumbuka sana Jiji pamoja na klabu.Hallaa kwa kila mmoja hapa, Asante sana. Huu ni muda sasa wakuanza ukurasa mpya katika maisha yangu ya Wales. Asante"

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULAI 4, 2013


DSC 0280 ac6c7



DSC 0279 63be0

MGAMBO WAMUUA MKULIMA KWA KUMPIGA FIMBO YA KICHWA MBEYA...!!!

Watu wawili ambao ni askari mgambo, wamekimbilia kusikojulikana bado, wanatafutwa na polisi baada ya kumpiga kwa fimbo kichwani na kumwua mkulima aliyetambulika kwa jina la Gigwa Malegi (55, Msukuma) na mkazi wa kijiji cha Iyonyo.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Barakael Masaki inasema kuwa mauaji hayo yalitokea tarehe Mosi Julai, 2013 majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Totowe wilayani Chunya, Mbeya. 


Taarifa hiyo imewataja watuhumiwa kuwa ni Focus Fabian na Charles (jina la pili halijafahamika bado).

Imeelezwa kuwa chanzo cha kupigwa na kuuawa marehemu kinatokana na kukutwa akilisha mifugo (ng'ombe) kaitka eneo oevu kandoni mwa ziwa Rukwa.

Kamanda Masaki ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake amewasihi watatue matatizo yao kwa mazungumzo na kwa kufuata sheria.

Ametoa wito kwa watuhumiwa kujisalimisha mikononi mwa askari mara moja ama yeyote mwenye taarifa za watuhumiwa, azitoe mara moja katika mamlaka husika ili hatua za kisheria zichukuliwe.

RAIS WA MISRI ATIMULIWA NA JESHI LA NCHI HIYO


jeshi nchini Misri limemuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo Mohamed Morsi na imemteuwa kiongozi wa muda wa nchi baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali.

Akihutubia kwa njia ya televisheni jumatano jioni, mkuu wa jeshi, Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema katiba ya Misri imesitishwa kwa muda na mkuu wa mahakama ya katiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa muda nchini humo. 


Sisi alitangaza kwamba jeshi linaangalia watu wa Misri kufuatana na maandamano makubwa ya upinzani yakidai kuwa Rais Mohamed Morsi ajiuzulu.

Kufuatia hotuba ya kwenye televisheni Bwana Morsi alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter, akiita hatua ya jeshi ni “mapinduzi kamili”. Aliwasihi wa-misri wote kukataa hatua ya jeshi lakini pia aliwataka kuwa na amani.

Kiongozi mpya wa muda nchini Misri, Adli Mansour ana umri wa miaka 68 ni mkuu wa sheria katika mahakama ya juu ya katiba. Ataapishwa alhamisi.

Kama sehemu ya mwongozo mpya unaoungwa mkono na jeshi kwa nchi, sisi aliutaka uchaguzi wa urais na wabunge, jopo kutathmini katiba na kamati ya mashauriano kitaifa. Alisema mwongozo ulikubaliwa na makundi kadhaa ya kisiasa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...