Friday, January 03, 2014

"SARAFU YA TSH. 50,000 HAITATUMIKA KATIKA MANUNUZI" PROF. NDULU

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.


Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

WACHINA WENGINE WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO 81 BANDARINI DAR ES SALAAM

 
TAARIFA KWA UMMA

Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na vyombo vingine vya Dola, tarehe 2 Januari 2014 majira ya saa tatu asubuhi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, imekamata meno 81 ya tembo yenye uzito wa kilo 303 sawa na tembo 41. Aidha, magamba 120 ya kakakuona na mazao ya bahari nayo yamekamtwa. 

Hii ni baada ya Askari wa Bandari kutilia shaka mizigo iliyokuwa kwenye gari ikiingizwa bandarini. Meno ya tembo yaliyokamatwa bado ni mapya ikiwa na maana tembo hao wameuawa katika kipindi kizichozidi mwezi mmoja uliopita.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

DK.SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Hassan Khatib, (kulia) alipotembelea banda la Ofisi ya faragha Ikulu, wakati wa Maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, yaliyofanyika jana viwanja vya Beit el Ras, katika shamra shamra za sherehe za Mapinduzi
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

WARIOBA: SERIKALI TATU SI MZIGO

MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, ametetea muundo wa serikali tatu kuwa hauna gharama, tofauti na inavyotafsiriwa na wengi. Mbali na kutetea gharama za uendeshaji wa serikali tatu, Jaji Warioba pia amewashukia wanaodhani mapendekezo ya muundo wa serikali tatu ni yake binafsi, kutokana na msimamo wa siku nyingi wa kiongozi huyo.
 
 Akizungumza na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Jaji Warioba alisema muundo wa serikali tatu umepunguza gharama za uendeshaji. Kwa mujibu wa Jaji Warioba, chini ya muundo huo hata Bunge linatarajiwa kuwa na wabunge 75 tu, hatua ambayo itapunguza gharama. Mwenyekiti huyo alisema kuwa gharama za uendeshaji wa Serikali ya Muungano zitakuwa katika Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mambo ya Nje huku katika maeneo yaliyobaki gharama zake zitakuwa zimepungua zaidi. 
“Hivi kwa nini hili la muundo wa muungano tunajadili gharama wakati kila mwaka tunapoongeza mikoa, wilaya, tarafa, majimbo na vijiji gharama zinaongezeka wala hakuna anayezungumzia wala kuhoji? Hivyo hivyo kwa kuwa na serikali tatu, hakuna gharama, tena kimsingi tumepunguza gharama za migogoro ya mara kwa mara ya kushughulikia kero za Muungano,” alisema Jaji Warioba.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 03, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS



.
.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...