Friday, March 22, 2013

CHINUA ACHEBE AFARIKI DUNIA



Mwanafasihi mahiri duniani pamoja na mwandishi wa Novel wa Naijeria, Profesa Chinua Achebe amefariki usiku wa leo hospitalini huko Boston Massachusetts, USA akiwa na umri wa miaka 82.
Taarifa kutoka kwa moja ya chanzo karibu na familia wa Chinua Achebe huyu amesema kuwa kwa kipindi sasa Chinua Achebe amekuwa akisumbuliwa na maradhi na amekuwa akitibiwa katika hospitali moja ambayo hakuitaja jina huko Boston.

Taarifa rasmi juu ya kifo hiki kutoka katika familia ya mwanazuoni huyu ambaye alikuwa mwalimu wa chuo kikuu huko Marekani ambapo amekuwa akiishi kwa miaka mingi sasa, itatolewa wakati wowote kuanzia sasa.
Kibongo bongo tunamfahamu sana chinua achebe kwa vitabu vyake maarufu ambavyo vimetumika katika kufundishia shule mbalimbali, kama vile Things Fall Apart alichokichapisha mwaka 1958, Kitabu ambacho kimeandikwa kwa lugha tofauti zaidi ya 50 duniani na kuuza nakala zaidi ya milioni 12, na vitabu vyake vingine maarufu ni pamoja na Arrow of God, No Longer at Ease, Anthills of the Savannah pamoja na A man of the People.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...