Friday, March 22, 2013

WAZIRI SITTA ACHONGEWA KWA LOWASSA

                                                                                      Edward Lowassa 
KWA UFUPI
Historia ya kisiasa baina ya vio ngozi hao inakifanya kikao cha leo kuwa mvuto wa aina yake kwani kitendo cha wabunge kuichongea Wizara ya Sitta kwa Kamati ya Lowassa kitatoa mwanya wa mpambano kati ya wanasiasa hao wawili.
Wakati hayo yanatokea, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Edward Lowassa itakutana na Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Samuel Sitta kujadili mambo mbalimbali yakiwamo sera ya Tanzania katika jumuiya hiyo.
Lowassa, alijiuzulu Uwaziri Mkuu 2008 wakati Sitta akiwa Spika na inasadikiwa kwamba tukio hilo lilijenga ufa kati ya wanasiasa hao wawili, ambao tayari wanatajwa katika kinyang’anyiro cha Urais 2015.
Historia ya kisiasa baina ya vio ngozi hao inakifanya kikao cha leo kuwa mvuto wa aina yake kwani kitendo cha wabunge kuichongea Wizara ya Sitta kwa Kamati ya Lowassa kitatoa mwanya wa mpambano kati ya wanasiasa hao wawili.
Wakizungumza mbele ya kamati hiyo, wabunge wa EAC walisema wizara hiyo haijawapa mwongozo wa kutetea maslahi ya Tanzania ndani ya jumuiya, jambo ambalo linawafanya washindwe kuchangia hoja zenye uzito.
“Tunatengwa na wizara, jambo ambalo linatufanya tutoe hoja tunazozijua wenyewe, kutokana na hali hiyo wanapaswa kubadilika,”alisema Shyrose Bhanji.
Aliongeza kuwa kila wanapojaribu kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wamekuwa waki pigwa kalenda, jambo ambalo linawafanya kupata taarifa nyingine kupitia vyombo vya habari.
“Tulitarajia tungeelezwa msimamo wa nchi, lakini mpaka sasa hatujaelezwa chochote na kwamba kila mmoja anachangia kutokana na upeo wake,” aliongeza. Mbunge mwingine, Abdallah Mwinyi alisema mpaka sasa Tanzania haina sera ya mtangamano ambao utawaweka pamoja wabunge hao katika kujadili mambo ya jumuiya.
“Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zina sera ya mtangamano ambazo zinawaweka pamoja wabunge kujadili mambo mbalimbali yanayohusu maslahi ya nchi zao, lakini sisi hatuna, wakati Rwanda imejiunga juzi tu tayari wameandaa sera inayowapa mwongozo wabunge wao,” alisema Mwinyi.
Sitta akana
Alipoulizwa juu ya malalamiko, Sitta, ambaye jana jioni alikuwa anahudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, alijibu kwa ujumbe mfupi wa maandishi;”Si kweli...niko kwenye kikao nitakupigia baadaye.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Stargomena Tax amewashangaa wabunge hao kwa kulalamika kukosa ushirikiano na kwamba madai hayo si ya kweli.
“Hivi wabunge hawa wanataka tuwape ushirikiano wa aina gani? Mbona tumekuwa tukikutana nao mara kwa mara na kuwapa misimamo ya nchi?
“Tulishakaa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na tuliwapa hadidu za rejea ili wawape wabunge wa Afrika Mashariki,” alieleza Dk Tax.
Dk Tax pia alisema wamechapisha kijitabu cha kuwapa mwongoza wa maeneo ya kuzingatia wakati wanapokwenda kwenye vikao vya Bunge la Afrika Mashariki.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...