Sunday, November 10, 2013

TUCTA YATAKA SH. 750, 000 KIMA CHA CHINI

kazi 857ac
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Mkoani Mbeya, limetangaza kiwango kipya cha mishahara inayotakiwa kuwa kima cha chini ni Sh 750,000.
Mwenyekiti wa Tucta mkoani hapa, Alinanuswe Mwakapala alisema kwa maisha ya sasa kima cha chini lazima kiwe Sh750,000 na kwamba, pendekezo hilo la mkoa litawasilishwa kwenye ngazi za juu za Tucta ili kulibariki.
Mwakapala alisema hayo kwenye hafla ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kukabidhiwa jengo la ghorofa tano lililojengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
"Wafanyakazi nchini sasa wamechoshwa na mishahara midogo, hivyo wakati umefika kwa wafanyakazi kutoogopa maandamano na migomo kudai haki," alisema huku akishangiliwa.
Hata hivyo, Rais wa CWT, Gratius Mukoba alisema madai ya wafanyakazi yaliyowasilishwa Serikalini ni kutaka nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100.
Mkoba alisema CWT hivi sasa wanasubiru ndani ya miezi mwili hadi Desemba kupata majibu.
hayatapatikana basi Serikali ijue imejipalia mkaa.
''Hatuwezi kuendelea kuwaona watu wasiofanyakazi wanapata mishahara mikubwa wakati wafanyakazi wanasota. Mwisho wa matatizo hayo ni sasa'' alisema huku akiwataka wafanyakazi hususan walimu kuachana na njama za kutaka kuwatenganisha.
Alisema Serikali inatakiwa kuwalipa walimu Sh49 bilioni wanazodai zikiwamo Sh30 bilioni walizopunjwa katika mishahara na kwamba pia lazima ipunguze kodi kwa wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi.
CHANZO MWANANCHI

NHIF YAWARUKA WANAOTUMIA DAWA ZA KUONGEZA MAUMBILE


article-2265277-17117548000005DC-778 306x423 a9381
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema hautahusika na malipo ya matibabu kwa wanachama wao watakaoathirika na utumiaji wa dawa za kuongeza maumbile.


Akizungumza kwenye kongamano la wadau wa mfuko huo mkoani hapa hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini alisema mfuko hautatoa huduma kwa mwanachama aliyeathirika na dawa za kuongeza maumbile ambazo zimepigwa marufuku na Serikali.
Dk Fikirini alisema mfuko huo unatoa huduma ya matibabu kwa wanachama wake, ila hauhusiki na waathirika wa dawa zilizopigwa marufuku na Serikali ikiwamo za kuongeza maumbile maarufu kama dawa za Kichina.

BUNGE LAITOSA TUME YA WARIOBA

jkbungeni_na_msimamo_13eee_a4a9e.jpg
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013, huku kukiwa na ushindani wa maeneo mawili ambayo baadhi ya wabunge walionyesha hofu.
Muswada huo ulipelekwa bungeni kwa hati ya dharura kutokana na makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo yaliyofanyika Oktoba 15, mwaka huu, baina ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni, baada ya muswada wa awali kususwa na vyama vya upinzani bungeni.
Katika mjadala ulioanza juzi na kuhitimishwa jana, wabunge wengi kutoka pande zote; CCM na upinzani waliyaunga mkono mapendekezo ya Serikali, lakini kulikuwa na hofu kuhusu idadi ya wajumbe watakaoteuliwa na Rais kuingia kwenye Bunge Maalumu na suala la ukomo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Marekebisho hayo yameiweka kando Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo haitakuwapo baada ya kukabidhi rasimu ya pili ya Katiba hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete, Desemba 15, mwaka huu.
Uhai wa tume hiyo ni miongoni mwa mambo yaliyozua ubishi baina ya wabunge wa Kambi ya Upinzani waliokuwa wakitaka iendelee kuwapo na wale wa chama tawala na Serikali, ambao walitaka iondoke kwa maelezo kwamba haitakuwa na kazi baada ya kukabidhi rasimu kwa rais kama inavyoeleza sheria ya kuanzishwa kwake.

MLINZI WA KAGAME AFANYIWA UMAFIA

ALIYEKUWA Mlinzi mkuu (bodyguard) wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Luteni Joel Mutabazi, ametekwa na kikosi cha Jeshi la Uganda na kukabidhiwa kwa Serikali ya Rwanda.

Taarifa za kiintelijensia zinasema kuwa Luteni Mutabazi, alikuwa akiishi nchini Uganda kwa hati maalumu ya ukimbizi ya Umoja wa Mataifa, baada ya kutoroka nchini Rwanda pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo, Faustin Kayumba Nyamwasa.

Luteni Mutabazi alitorokea nchini Uganda Oktoba 2011, baada ya kutoroka jela yenye ulinzi mkali wa kijeshi ya Kami nje kidogo mwa mji wa Kigali akituhumiwa kwa kuhusishwa na kutoroka kwa mkuu huyo wa majeshi na kukimbilia Afrika Kusini. Alikuwa mlinzi mkuu wa Rais Kagame mpaka mwaka 2010, alipotoroka na kukimbilia Uganda.

Mlinzi huyo pia anashutumiwa na Serikali ya Rwanda kwa kutoa siri kwa Kikosi Maalumu cha Umoja wa Mataifa chini ya Majeshi ya Umoja ya Kulinda Amani nchini Kongo, (MONUSCO) na kuwezesha kuchakazwa na kushindwa kwa kikosi cha waasi wa M23.

Kutokana na tukio hilo, hivi sasa Serikali ya Rais Yoweri Museveni, imelazimika kumsimamisha kazi Mkuu wa Intelijensia wa Jeshi la Polisi, Joel Aguma, ambaye alihusika kumteka na kumkabidhi Luteni Mutabazi kwa Serikali ya Rwanda.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 10, 2013

.
.

.
.

TANZANITE YAUA 5-1, KUTUA DAR MCHANA

tanzanite_189c1.jpg
Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada ya leo (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza Msumbiji mabao 5-1.
Mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati mengine yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia Minja.
Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo Jumapili (Novemba 10 mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
Tanzanite inayofundishwa na Rogasian Kaijage itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini. Mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 6 na 8 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22 mwaka huu.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

UTAFITI VYUO VIKUU WAUZWA MITAANI

jengo_9a969.jpg
Wakati Serikali ikiwa katika hatua za utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwenye elimu, imebainika kuwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaohitimu, wanafanya udanganyifu kwenye utafiti kwa kufanyiwa na watu wengine au kununua uliokwisha andikwa.
Kila mwanafunzi anayesomea shahada ya kwanza, uzamili au uzamivu hutakiwa kufanya utafiti ikiwa ni sehemu ya vigezo vya kukamilisha masomo yake.
Hata hivyo, Mwananchi imebaini kuwapo kwa wanafunzi wengi wanaotumia mbinu mbalimbali za kuandika utafiti huo bila kwenda maeneo husika.
Uchunguzi wetu uliofanyika kwa muda mrefu kwenye vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa baadhi ya wanafunzi huchukua tafiti za zamani na kuzinakili upya, huku wengine wakichukua kutoka kwenye mitandao na kuzifanyia marekebisho kidogo ili zifanane na eneo analotaka kufanyia utafiti huo.
Mtafiti Mwandamizi ESRF
Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk Donatila Kaino anasema ni asilimia 20 tu ya wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu nchini, ndiyo wanaoweza kuandika utafiti kwa ufasaha.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...