Thursday, November 14, 2013

MAELEZO MAPYA ALIYOYATOA MOHAMED MORSI JINSI ALIVYOPINDULIWA EGYPT.

Morsi 1 
Rais Mohamed Morsi aliepinduliwa madarakani nchini Misri July 2013 amesema alitekwa nyara na wanajeshi ambao ndio walimtoa kwenye madaraka ambapo kikundi cha wanasheria waliojitolea ambao hawako kwenye upande wa Morsi, wametangaza hii baada ya kukutana na Morsi gerezani.

Rais huyu aliepinduliwa anataka kulishtaki jeshi na anasema hakutakua na utulivu Misri mpaka hawa watu waliompindua watolewe na wale waliohusika na umwagaji damu za Wamisri  watakapowajibishwa.
morsi gerezani

Kwenye barua aliyoandika, anasema alitekwa nyara na hawa wanajeshi siku moja kabla ya kupinduliwa rasmi na baada ya hapo akashikiliwa kwenye kambi ya jeshi kwa miezi minne na baada ya hapo akahamishiwa kwenye gereza ambalo wanafungwa watu mashuhuri November 4 baada ya kesi kusikilizwa kwa mara ya kwanza kuhusu mauaji ya December 2012.
Mmoja wa wanasheria amesema Morsi ana mpango wa kushtaki kisheria kikundi hicho cha wanajeshi kwa msaada wa wanasheria wake hivi karIbuni na mpaka sasa hajaamua ni wanasheria gani watamsimamia kwenye hii kesi ya January 8 2014 ambapo Aljazeera wameripoti kwamba kauli nyingine ya Morsi ni kwamba Mahakama haistahili kusikiliza hii kesi wala haina mamlaka ya kufanya wanachofanya.

Kwa kumalizia, Morsi ambae aligoma kuvaa sare nyeupe wanazovaa wafungwa kwenda Mahakamani huku akipaza sauti kwamba yeye bado ni rais wa Misri na haitambui hiyo Mahakama inayosikiliza kesi yake, amesema mpaka hapo alipo anajisimamia mwenyewe kisheria.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...