Monday, September 23, 2013

HUYU NDIYE MWANAMKE RAIA WA UINGEREZA ANAYETUHUMIWA KUIONGOZA AL-SHABAAB KUUA WATU NAIROBI

Mwanamke raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa* kuongoza kundi la magaidi wa Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya Westgate ya jijini Nairobi nchini Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68 na kujeruhi wengine zaidi ya 175.

Tayari mashirika makubwa ya habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes yameandika habari kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa magaidi hao walioshambulia Westgate.

Nayo akaunti ya Twitter ya American Jihad Watch ‏@watcherone, imepost picha ya gaidi wa kike iliyedai ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na kudai kuwa ‘huenda’ akawa ni The White Widow. “Female jihadi caught on mall camera at Westgate Centre Shopping mall earlier yesterday may be infamous ‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.


Picha ya gaidi akiwa ndani mall hiyo

Kwa mujibu wa baadhi ya watu waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa kizungu.

Kwa mujibu wa CNN, magaidi watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya, Uingereza, Finland na wawili wa Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.

ALIYEMJERUHI AUNT EZEKIEL KWA CHUPA ASOTESHWA KORTINI


Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.

Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya.

Habari za ndani kutoka kortini zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi Fimbo.

Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi.
Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena.

Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar.

P SQUARE WANATISHA AFRIKA

SQUARE1 89dc2
KUNA jambo moja ambalo mashabiki wa timu ya soka ya Arsenal wa Bongo wanajivunia kwa sasa. Unajua hao mashabiki wamefanya nini? Wamegeuza kibwagizo cha wimbo maarufu wa 'Personally' unaotamba kwa sasa wakaupa jina la 'Arsenally'.


Wimbo huo ni wa wakali wa muziki wa Afrika kwa sasa ambao ni Peter na Paul Okoye wa Nigeria. Kimuziki wakali hao wanajulikana kwa jina la P-Square.
Kwa sasa wamevunja rekodi ya kuwa wasanii ambao nyimbo zao hazijawahi kuachwa kupigwa kwenye majumba ya starehe tangu mwaka 2003 mpaka dakika hii unaposoma ukurasa huu.
Mwaka huo ndipo walipozindua albamu yao ya kwanza 'Last Night' ambayo ilitengenezwa na Timbuk Music Label.
Wasikilizaji wazuri wa muziki, watakumbuka kwamba tangu kutolewa kwa ngoma yao ya kwanza, kila mwaka wakali hao wanadondosha nyingine na mpaka sasa hawajawahi kupotea kwenye ramani.
Unaposoma makala haya, wimbo wao bora wa 'Alingo' unatesa na huku 'Personally' ukiendelea kupasua anga vilevile.

"NIKIRUDI TANAZANIA SITAKI MAPOKEZI KWASABABU WATANZANIA NI WANAFIKI"... AGNESS MASOGANGE

  Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.

Lakini hata hivyo kwa mujibu chanzo chetu toka kwa mtu wa karibu na familia yake,  Masogange  amesema  hatohitaji mapokezi yoyote pindi atakapowasili nchini kwa vile hao wanaopanga mapokezi ndio wanafiki wakubwa ambao walikuwa wanashangilia alipokuwa jela.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 23, 2013

DSC 0027 512b4
DSC 0028 c7bcf

MILIO YA RISASI YASIKIKA NDANI YA WESTGATE


kenya 645db
Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini.


Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Inaarifiwa wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.

BARARBARA YA MLIMA KITONGA MKOANI IRINGA KUPANULIWA

Picha-21 d563b
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli (katikati) akipewa maelezo na Meneja wa Tanroads mkoa wa Iringa Eng. Poul Lyakurwa wakati alipokuwa akipita kukagua eneo la Kitonga katika barabara ya TANZAM mkoani Iringa. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) na Eng. Chrispianus Ako kutoka Tanroads Makao Makuu (wa kwanza Kushoto) pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Ujenzi.

Kujifunga kwa barabara katika eneo la Kitonga katika barabara kuu ya TANZAM kumekuwa kukisababisha adha kubwa kwa wasafiri. Eneo hilo liko mkoani Iringa katika barabara kuu inayoanzia jijini Dar es Salaam ikiunganisha na mikoa ya kusini magharibi mwa nchi yetu pamoja na nchi jirani za Zambia, Congo DR na Malawi.
Barabara katika sehemu ya Kitonga inapita katika muinuko mkali ambapo inapotokea ajali au gari kuharibika, huwa ni vigumu kwa magari mengine kupita hadi gari lilizoba njia liondolewe.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alikutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma ambapo pamoja ya mambo mengine yaliyozungumziwa katika kikao hicho, lilijitokeza suala la kujifunga mara kwa mara kwa barabara ya TANZAM katika eneo la Kitonga.

"NITAHUDHURIA MKUTANO WA UN, MAREKANI" BASHIR

bashiri cf7dd
Rais wa Sudan Omar El bashir amethibitisha kwamba atahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New york juma hili, licha ya kusakwa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC.
Bashir anatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Bashir amesema kuwa tayari amekodisha chumba cha kulala katika hoteli moja mjini humo na kwamba hatishiki kukamatwa na Marekani kwa kuwa sio mwanachama wa ICC.
Hata hivyo haijulikani iwapo atapewa viza kwa kuwa imekuwa utamaduni wa taifa hilo ambalo limetoa vibali hivyo kwa viongozi kama Robert Mugabe wa Zimbabwe na Mahmoud Ahmedinejad wa Iran kuhudhuria mkutano huo. Chanzo: bbcswahili

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...