Friday, December 26, 2014

MAASKOFU WATAKA JK AENDELEZE FAGIO LAKE

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Michael Hafidh (kulia) akifurahi jambo na Fred Msongole aliyebeba mtoto wake, Jonathan Msongole (miezi 8) baada ya kukamilisha ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana. (Picha na Fadhili Akida).
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Michael Hafidh (kulia) akifurahia jambo na Fred Msongole.

MAASKOFU wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo nchini, wamepongeza uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwajibisha watendaji wake, huku wakimtaka asiishie kuchukua hatua kwa waliotajwa kuhusika na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow pekee, bali pia wazembe na wote wanaokutwa na tuhuma mbalimbali katika utawala wake.
Aidha, wamesisitiza kamwe asicheke nao, kwani kitendo cha kuwavumilia kinaweza kugeuka shubiri katika utawala wake kwa kuwa watamharibia kazi. Walisema hayo kwa nyakati tofauti katika salamu zao za maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi, jana.
Weka pembeni Akiongoza mahubiri katika Ibada Kuu ya Krismasi katika Kanisa la Champlesy la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Askofu Michael Hafidh wa Zanzibar, alishauri Rais Kikwete aendeleze utaratibu wa kuwawajibisha viongozi wazembe na wasio waadilifu katika kazi zao.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MABASI 21 YAADHIBIWA KWA NAULI JUU KRISMASI

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamedi Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi Dar es Salaam juzi kuhusu kupanda kwa nauli ya mabasi yaendayo mikoani, daladala zinazoishia Mnazi Mmoja, ajali za barabarani na mambo mbalimbali yanayohusu usalama wa abiria. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) Kanda ya Mashariki, Thomas Haule na Mwenyekiti CHAKUA,Hassan Mchanjama. (Picha na Yusuf Badi).
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamedi Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
 
JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), limewaadhibu wamiliki wa magari zaidi ya 21.
Mawakala wao wa kukata tiketi, wamesombwa na kuburuzwa mahakamani, ambao baada ya kesi zao kusogeswa mbele, sasa wanasota mahabusu, watakakokuwa hadi baada ya shamrashamra za kuukaribisha Mwaka mpya 2015.
Wakati mabasi mengi yakinaswa Morogoro, mawakala wa tiketi ambao pia ni maarufu kama wapigadebe, wamekamatwa katika kikuo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo, Dar es Salaam.
Hayo yamethibitishwa na Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoawa Morogoro, Allen Mwanri aliyesema mabasi zaidi ya 21 yalikamatwa kwa makosa ya mbalimbali, likiwemo kubwa la kuzidisha nauli na kutoza nauli kubwa.
Hata hivyo, alisema kila mmiliki wa basi lililokamatwa kwa kuzidisha nauli na nauli kubwa, alitozwa adhabu ya kiasi cha Sh 250,000. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MALASUSA: UFISADI NI ZAO LA KUTOKUWA NA HOFU YA MUNGU




Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa akihubiri katika ibada ya Krisimasi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam 
 

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa amesema watanzania wengi hivi sasa wamekosa kitu muhimu na cha thamani katika maisha yao, ambacho ni kutokuwa na hofu ya Mungu.

Amesema kufuatia hali hiyo Tanzania imejikuta ikiingia kwenye vitendo vya rushwa na ufisadi, huku viongozi waliopewa dhamana na wananchi wakiweka mbele maslahi yao binafsi badala ya Taifa.

Askofu Malasusa ameyasema haya leo katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu na akihubiri katika ibada ya Krisimasi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 26, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


DSC07606
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

KIJANA AKAMATWA KWA KUMTUKANA RAIS

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki 
 
Polisi nchini Uturuki wamemkamata mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka kumi na sita kwa tuhuma za kumtukana Rais Recep Tayyip Erdogan.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, kijana huyo alipelekwa mahabusu baada ya kumtuhumu Bwana Erdogan na chama chake tawala cha AK kwa vitendo vya rushwa wakati wa mkutano wa hadhara katikati ya mji wa Anatolia.
Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu ametetea kukamatwa kwa mwanafunzi huyo akisema ofisi ya rais lazima iheshimiwe.
Kumtukana mkuu wa nchi ni makosa kwa mujibu wa sheria za Uturuki na mwanafunzi huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka minne jela endapo atapatikana na kosa. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

INDONESIA WAKUMBUKA TSUNAMI

Wanawake eneo la Aceh wakifanya sala ya kukumbuka maafa makubwa yaliyosababishwa na tsunami miaka kumi iliyopita nchini Indonesia 
 
Wananchi wa Indonesia wameanza kuadhimisha mwaka wa kumi tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha mawimbi makubwa katika bahari ya Hindi, tsunami na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watu laki mbili na elfu ishirini katika eneo kubwa.
Umati wa watu umekusanyika karibu na jengo la makumbusho la tsunami katika eneo la Banda Aceh katika kisiwa cha Sumatra.
Mji huo ulisambaratishwa kabisa na tetemeko kubwa la ardhi na mawimbi ya tsunami. Makamu wa Rais wa Indonesia(Jusuf Kalla) anaongoza maadhimisho hayo na atawashukuru wafanyakazi wa kujitolea katika eneo hilo na duniani kote kwa kulisaidia eneo la Aceh kurejea katika hali ya kawaida baada ya mkasa huo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

ASKARI WATATU WA AU WAUAWA SOMALIA

Askari wa Somalia wakiangalia mabaki ya magari katika moja ya mashambulio ya kigaidi mjini Mogadishu, Somalia. 
 
Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia limesema askari wake watatu na kandarasi raia wameuawa katika shambulio lililofanyika katika makao yake makuu mjini Mogadishu.
Taarifa ya Umoja wa Afrika imesema wapiganaji wa al-Shabab waliingia katika kambi wakivalia sare kama askari wa jeshi la serikali ya Somalia.
Taarifa hiyo imesema washambuliaji watano waliuawa na wengine kadha kukamatwa. Pamoja na kutoa eneo hilo kuwa makao makuu ya majeshi ya kulinda amani ya AU nchini Somalia, eneo hilo lililoimarishwa pia makao ya balozi za Uingereza na Italia. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

LIGI KUU TANZANIA BARA KUANZA LEO

 Kikosi cha timu ya Azam ya Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania 
  
Ligi kuu ya Tanzania bara, maarufu kama Ligi Kuu ya Vodacom inaanza rasmi mzunguko wa pili leo, Ijumaa baada ya kusitishwa tangu Novemba 7, 2014.
Hadi ligi hiyo ilipositisha mzunguko wa kwanza, tayari timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo zilikuwa zimecheza michezo saba kila moja.

Timu ya Simba ya ligi kuu ya Vodacom
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania, TFF, Simba ambayo ni miongoni mwa timu kongwe za ligi hiyo na ambayo katika mzunguko wa kwanza haikuwa na matokeo mazuri baada ya kwenda sare mara sita na kushinda mchezo mmoja na kujikusanyia pointi tisa ikishika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo, leo inaikaribisha Kagera Sugar inayoshikilia nafasi ya tano katika pambano litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Michezo mingine itafanyika katika viwanja mbalimbali kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wiki hii.

Wachezaji wa timu ya Yanga
Mpaka sasa Mtibwa Sugar ndiyo inayoongoza ligi hiyo ya Vodacom baada ya kujikusanyia pointi 15, ikifuatiwa na Young Africans(Yanga) kwa kuwa na pointi 13 sawa na Azam mabingwa watetezi. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

WENGER AMUWINDA BEKI WA REAL MADRID

Sergio Ramos wa Real Madrid.Kocha wa Arsenal adaiwa kummezea mate 
 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amewasiliana na ajenti wa beki wa Real Madrid Sergio Ramos kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na kilabu hiyo ya uwanja wa Emirates.
Ramos mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na kilabu hiyo ya Los Blancos kwa takriban muongo mmoja baada ya kuwasili kutoka sevilla kwa kitita cha pauni millioni 20 mwaka 2005.
Hatahivyo ripoti za hivi majuzi zimedai kwamba Ramos huenda akaondoka katika kilabu hiyo ya Santiago Bernabeu baada ya mazungumzo ya kandarasi yake mpya kugonga mwamba.
Na kulingana na mwandishi Esteban Manolete wa AS ,mkufunzi huyo wa The Gunners amewasiliana na wawakilishi wa Ramos ili kuona iwapo anaweza kumvuta mchezaji huyo katika eneo la London kazkazini.
''Wenger amewasiliana na Rene Ramos ajenti na ndugu ya Sergio Ramos'',mwandishi huyo alikimbia kipindi cha La Goleada.
Wenger juma hili alikiri kwamba safu ya ulinzi ya Arsenal haina uongozi baada ya kufungwa bao la dakika za mwisho na liverpool na hivyobasi kupata sare ya 2-2. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...