Friday, December 26, 2014

MAASKOFU WATAKA JK AENDELEZE FAGIO LAKE

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Michael Hafidh (kulia) akifurahi jambo na Fred Msongole aliyebeba mtoto wake, Jonathan Msongole (miezi 8) baada ya kukamilisha ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana. (Picha na Fadhili Akida).
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Michael Hafidh (kulia) akifurahia jambo na Fred Msongole.

MAASKOFU wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo nchini, wamepongeza uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwajibisha watendaji wake, huku wakimtaka asiishie kuchukua hatua kwa waliotajwa kuhusika na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow pekee, bali pia wazembe na wote wanaokutwa na tuhuma mbalimbali katika utawala wake.
Aidha, wamesisitiza kamwe asicheke nao, kwani kitendo cha kuwavumilia kinaweza kugeuka shubiri katika utawala wake kwa kuwa watamharibia kazi. Walisema hayo kwa nyakati tofauti katika salamu zao za maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi, jana.
Weka pembeni Akiongoza mahubiri katika Ibada Kuu ya Krismasi katika Kanisa la Champlesy la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Askofu Michael Hafidh wa Zanzibar, alishauri Rais Kikwete aendeleze utaratibu wa kuwawajibisha viongozi wazembe na wasio waadilifu katika kazi zao.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Alisema: “Rais Kikwete, viongozi wazembe na wenye kashfa usiwachekee kabisa, watakuangusha. Ukiona kiongozi anazembea weka pembeni tu, kuwa kama kocha, ukiona mchezaji hachezi vizuri weka pembeni, chagua mwingine, watu wanataka nchi iwe na amani na maisha bora kwa Watanzania wote.
“Hakuna sababu ya kumuonea aibu mtu, endelea hivyo hivyo, mtu akikosea unamwambia akae pembeni unachagua mwingine, shida yetu ni ushindi nchi yetu iwe na amani.”
Alisema viongozi wanapopata nafasi ya kuongoza haimaanishi wao wanajua zaidi, ila wamepewa neema kuongoza na kwamba Watanzania wana hazina ya wasomi, hivyo wasilewe madaraka na badala yake waifanye kazi waliyoaminiwa kuifanya kwa niaba ya Watanzania.
Alisema anashangazwa kusikia kiongozi katika jamii anakuja na ahadi kemkem, zikiwamo za kuwapelekea wananchi huduma za maji, umeme, barabara, dawa hospitali, ilhali zote ni haki za msingi za mpigakura.
“Ifike mahali watu watafute njia nyingine za kutafuta kura, si sera zile zile za maji, umeme, madawa, barabara nzuri…kwanini uende kwa mwananchi kumshawishi kumpa haki yake ya msingi? Wewe tafuta njia bora ya kuisaidia jamii unayoiongoza, si kugeuka mzigo kwa Mtanzania,” alisema na kuongeza kuwa, kwa kushindwa kutimiza majukumu yao, viongozi wa aina hiyo husababisha chuki dhidi ya serikali na kukata tamaa, hali inayoweza kusababisha kuvunjika kwa amani.
Viongozi wa dini kugeukia siasa Aliwataka viongozi wa dini na kuwataka kuachana na siasa, kwani jukumu lao ni kuombea taifa na viongozi wake sio kuingia katika migogoro ya wanasiasa na kuanza kuhubiri siasa katika nyumba za ibada.
“Tunataka kusikiliza habari njema kanisani, sasa viongozi wa dini wakisimama majukwaani ni kubomoana tu, wakisikia jambo bungeni nao wanalidaka, kazi yetu ni kupiga goti kuwaombea sio kuungana nao,” alisema Askofu Hafidhi.
Askofu huyo aliwataka pia wanahabari kuzingatia maadili ya uandishi katika kutoa taarifa kwa jamii kwa sababu habari nyingine zinasababisha chuki kwa wananchi, hivyo wasiangalie mauzo ya kazi zao pekee, bali pia wageukie uzalendo kwa nchi yao.
Akitoa salamu za Krismasi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Askofu Dk Alex Malasusa, Askofu Hafidhi alisema nchi inakabiliwa na mambo makuu ambayo ni Uchaguzi Mkuu pamoja na ule wa kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini kuepuka vurugu za aina yoyote.
Alisema amani imedumu kwa miaka mingi, ingawa zilijitokeza vurugu kidogo katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni, hivyo badala ya kuichezea, ni vyema ikatunzwa mithili ya mboni ya jicho.
JK asiishie Escrow Mawazo ya Askofu Hafidhi yameshabihiana na yale ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu aliyeitaka serikali isiishie kuwaadhibu wachache waliotajwa kwenye sakata la Escrow, bali ihakikishe wote waliohusika kwenye tuhuma hizo, wanachukuliwa hatua za kisheria na wanarudisha fedha walizoiba ili kuleta amani.
Alisema pamoja na baadhi ya waliotajwa katika sakata la Escrow, kuondolewa katika nyadhifa walizokuwa nazo wanatakiwa kurudisha fedha walizoiba na kuchukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa viongozi wengine wa umma.
Alitoa kauli hiyo jana wakati wa mahojiano mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Krismasi, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kilutheri mjini hapa. Alisema sasa nchi inatakiwa kuomba ili iweze kupata viongozi wenye hofu ya Mungu wenye moyo wa kutumikia wananchi ;na si tu kujali maslahi yao binafsi huku kundi kubwa la wananchi wakiishi kwenye umasikini.
Pia, aliitaka Serikali kuchukua hatua za haraka katika kuwawajibisha mafisadi ili kukomesha vitendo hivyo, ambavyo vimekuwa vikiita hasara nchi. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Hatua ziwe zinachukuliwa mapema isiwe mpaka wananchi wanaanza kupiga kelele na kuhatarisha usalama wa nchi,’ alisema. Askofu Kinyunyu alisema tatizo kubwa lililopo jambo linapotokea linachelewa kuchukuliwa hatua mpaka wananchi wapige kelele na ndipo maamuzi yafanyike.
Alisema hata maamuzi mengi yanakuwa ya zimamoto, lakini kinachotakiwa ni kutekeleza na kusimamia maadili na hata sheria za utumishi wa umma. Askofu kinyunyu alisema tatizo kubwa kwa baadhi ya Viongozi wanapoingia madarakani wanawaza kujilimbikizia mali wao hawakumbuki kuwahudumia wananchi wengine.
Alisema hali hiyo imekuwa ikichangia wananchi kukosa huduma muhimu. “Serikali isiishie kuwaadhibu hao wachache wanaotajwa kwenye sakata la Escow, bali ihakikishe wote waliohusika kwenye tuhuma hizo, wanachukuliwa hatua za kisheria ili kuleta amani,” alisema.
Pia, aliitaka Idara ya Maadili ya Utumishi wa Umma kufanya kazi zake bila kumwonea mtu yeyote ili wote waliohusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na sheria ifuate mkondo wake. Awali, akihubiri katika ibada ya Krismasi aliwataka watu wote kudumisha amani na upendo.
Alisema maana ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni amani na upendo hivyo watu washerehekee kwa kukumbuka kudumisha mambo hayo. “Maana ya Krismasi ni amani na upendo ni lazima tuhakikishe tunadumisha mambo hayo ambayo ni muhimu sana katika maisha.
Fagio la chuma Askofu Dk Martin Shao wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, amesema fagio la chuma alilokabidhiwa Rais Jakaya Kikwete na Watanzania, amekuwa akilitumia vizuri katika kufagia uozo wote unaofanyika.
Alisema hayo jana alipokuwa akitoa salamu maalumu ya Krismasi kwa taifa, kwa niaba ya Dayosisi ya Kaskazini. Alisema Rais Kikwete amekuwa akitumia busara na hekima kubwa katika kufanya maamuzi makubwa ya nchi.
Alisema amekuwa akitumia fagio lake la chuma vizuri katika kuondoa uchafu, unaofanywa na baadhi ya watendaji wasio waaminifu. Mbali na kumpongeza Rais Kikwete kwa hotuba yake nzuri ya hivi karibuni, alisifu pia uamuzi wa kutengua uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, lakini pia askofu huyo akaongeza kuwa, bado Watanzania wanasubiri amalizie kazi iliyobaki.
Alisema Watanzania wameridhika na maamuzi ya Rais kuhusu sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, na kueleza kiu kubwa wanasubiri kuona maamuzi makubwa yatafanyika zaidi ya hayo.
Alimtaka Rais Kikwete kuendelea kuwa na ujasiri wa hali ya juu, wa kutumia fagio lake la chuma, kwa kufagia watu wote wanafanya ubadhirifu wa mali za umma, na watumishi wote wanaokiuka maadili ya utumishi na kujilimbikizia mali.
“Rais wetu ameweza kutumia vizuri fagio lake la chuma katika kufanya maamuzi, nampongeza sana kwa hotuba yake iliyojaa busara na maamuzi mazuri, lakini atambue Watanzania bado wanasubiri maamuzi mengine yaliyobaki kiporo kwa hamu kubwa….tunaamini atafanya maamuzi mazuri zaidi,” alisema Askofu Shao.
Katiba Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa alisema ni vyema Watanzania wakaisoma Katiba Inayopendekezwa kipengele kimoja kimoja na kuielewa, ili ukifika wakati wa kuipigia kura waweze kukubali au kukataa kitu wanachokijua wao wenyewe.
Alisema kila Mtanzania anatakiwa kuitambua Katiba yake ambayo haina maslahi kwa chama chochote. “Tusiache watu wasome Katiba Inayopendekezwa kwa ajili yetu, au kutusemea yaliyomo, ni vyema kila Mtanzania akaisoma na kuielewa ili wakati wa kuipigia kura afanye maamuzi akiwa anaitambua,” alisema Askofu Shao.
Uchaguzi mkuu ujao Katika uchaguzi mkuu wa mwakani, Askofu Shao amewataka Watanzania kuliombea taifa, kwani ndicho kipindi cha kuitafuta amani bila ya kujali itikadi za kidini na siasa.
Aliwataka Watanzania kutokubali kununuliwa wa baadhi ya wagombea katika nafasi za udiwani, wabunge na urais watakaohitaji madaraka, kwa lengo la kuwapigia kura, na badala yake waangalie kiongozi mwadilifu.
Askofu Shao alisema taifa linahitaji kiongozi mwenye hofu ya Mungu, bila kuangalia chama cha siasa, ambaye atakuwa mwadilifu katika kutunza na kulinda rasilimali za Watanzania, pamoja na amani iliyopo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...