Gazeti la Mwananchi la Machi 13, 2015 lilibeba
ujumbe mzito kwa Watanzania. Kichwa cha habari kimoja kilisomeka:
“Maaskofu: Pigieni Katiba kura ya hapana.”
Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo ambao ni Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Kikristo (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcicius
Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT)
Askofu Daniel Awet, kwa sauti moja wamewataka waumini wao kujiandikisha
kwa wingi katika Daftari la Wapigakura, kuisoma vyema Katiba
Inayopendekezwa na hatimaye kuikataa kwa kuipigia kura ya ‘hapana.’
Sababu kuu za kuwahamasisha waumini wao na
Watanzania kuikataa Katiba Pendekezwa ni mbili. Mosi ni kulazimisha kura
ya maoni ya katiba mpya kufanyika bila maandalizi ya kutosha, yakiwamo
maridhiano ambayo yameligawa Taifa katika vipande vipande. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Pili viongozi waandamizi wa Serikali ya CCM kuupigia debe muswada wa Mahakama ya Kadhi.
Tamko hili nyeti ambalo limesambaa katika makanisa
mengi iwapo litasomwa kwa waumini wote na kuhamasishwa na mapadri,
wachungaji na wainjilisti basi unaweza ukawa ndiyo mwisho wa Katiba
Inayopendekezwa kupigiwa kura Aprili 30 mwaka huu.
Viongozi wa jukwaa hilo wana wajibu wa kushiriki
kikamilifu katika zoezi la kuandika Katiba Mpya ambalo linawahusu
waumini wao pia. Katiba siyo suala la siasa, bali ni la Watanzania wote.
Itakumbukwa kuwa CCM ilitumia mabavu na fedha
nyingi katika kusimamia mijadala ya Katiba Mpya, wakapitisha Katiba kwa
kutumia vyombo vya dola.
Hofu ya kukataliwa kwa Katiba Mpya kumeifanya
Serikali ya CCM ivunje kabisa makubaliano na Kituo cha Demokrasia
Tanzania (TCD) kwamba Kura ya Maoni ingesitishwa hadi baada ya uchaguzi
2016.
Hata hivyo, kwa sababu ya hofu ya kuanguka
madarakani, CCM imeamua iendelee kulazimisha kura ya maoni kwa kutumia
mabavu na hivyo kuwaburuza wananchi.
Matokeo yake Serikali ya CCM inafanya kila hila
ili Daftari la Wapigakura lisiboreshwe ili waweze kuchota kura vizuri
kiholela holela.
Nionavyo hofu kuu ni Katiba hii kuja kukataliwa na
umma, hivi Rais Kikwete ameona heri aendelee kuisukuma walao ikubalike
na umma. Lakini ukweli ni kwamba katiba hii imekataliwa na wananchi
wengi pia hata na Mungu kwa sababu ‘sauti ya wengi ni sauti ya Mungu’.
Sababu nyingine kubwa ya kukataliwa na wananchi
wakiwamo maaskofu ni Katiba Inayopendekezwa kulenga kulinda masilahi ya
watu wachache ndani ya chama na Serikali ya CCM.
Ukawa nao
Amani inavyozorota
Kuvuruga uchaguzi kwa kutumia katiba mbaya na kanuni mbaya ndiyo
mwanzo wa machafuko, vita na mauaji kama yale yaliyotokea nchini Kenya
mwaka 2007, Kibaki alipolazimisha ushindi na akaapishwa usiku usiku
mbele ya watu wachache tu.
Katiba Mpya inabidi ilete amani na siyo machafuko.
Ukisoma alama za nyakati hayo ndiyo yanayokuja mbele yetu. Watanzania
tujiulize tunataka nini?
Katika mkutano wa Maaskofu hao uliofanyika 10
Machi mwaka huu, walisema kwamba Katiba inayopendekezwa imeleta
mgawanyiko mkubwa katika Taifa, kwani imepatikana kwa njia zisizo za
kiuadilifu na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe.
Viongozi hao kama wadau wa demokrasia, amani na
ustawi wa Taifa letu, wamewaomba waumini wao kujiandikisha kwa wingi
katika Daftari la Wapigakura na kwenda kupiga kura ya “hapana”
Maaskofu wana wajibu na haki ya kutoa mwelekeo kwa
waumini wao ili wachague kitu kizuri na siyo kibaya kitakachokuja
kuwadhuru hapo baadaye. Kama viongozi wa dini na jamii, hawawezi kuacha
kuitahadharisha jamii juu ya hatari iliyopo mbele yao.”
Ukawa nao
Kwa upande wa Ukawa, wanaonekana kama walipata
maono ya kusoma alama za nyakati wakasusia Bunge la Katiba, uamuzi wa
kutoshiriki uovu huo ulikuwa mzuri na leo wapo huru kwamba hawakushiriki
dhambi hii ya kuua demokrasia nchini Tanzania.
Ikiwa mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba
Inayopendekezwa umekiuka Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, maana yake ni
kwamba katiba hiyo ni feki, haina uhalali wowote wa kisiasa, umekosa
maridhiano na wala haikubaliki kwa wananchi wazalendo wa Tanzania.
Amani inavyozorota
Maaskofu hao wanaendelea kubainisha jinsi usalama
wa nchi na raia ulivyozorota na kuanza kuzalisha vikundi vya kihuni na
ujambazi kama “Panya Road, Mbwa Mwitu’ na vingine.
Kama wadau wakubwa wa amani nchini wana haki ya
kuongelea suala hili nyeti kwa sababu amani ikitoweka viongozi wa dini
wanakuwa wa kwanza kulaumiwa kama ilivyotokea nchini Rwanda.
Tamko la maaskofu hao “ Kataeni katiba” naliona la
“kinabii na la kimapinduzi” lililokuja muda mwafaka ambapo waumini wa
Kikristo walikuwa hawana mwelekeo juu ya suala la kura ya maoni ya
Katiba Inayopendekezwa na suala la Mahakama ya Kadhi. Ndiyo kwa maana
naandika Maaskofu wa Jukwaa la Kikristo wachochea moto wa kuikataa
katiba pendekezwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na Padri Baptiste Mapunda
Na Padri Baptiste Mapunda
2 comments:
Askofu Ikongo ametoa siku 14 kwa Jukwaa la Kikristo kutoa tamko la hatua walizochukuliwa Maaskofu waliotuhumiwa na Bunge la Januhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba wamepokea mgao wa fedha za ESCROW. iLI Viongozi hawa wa Dini kuonyesha wao ni Maaskofu waadilifu, wawa weke pembeni waliotajwa bila upendeleo. Serikali yenyewe inafanya kazi hiyo kupitia tume ya maadili ya viongozi wa uma. 0752558069
Reply
Askofu Ikongo ametoa siku 14 kwa Jukwaa la Kikristo kutoa tamko la hatua walizochukuliwa Maaskofu waliotuhumiwa na Bunge la Januhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba wamepokea mgao wa fedha za ESCROW. iLI Viongozi hawa wa Dini kuonyesha wao ni Maaskofu waadilifu, wawa weke pembeni waliotajwa bila upendeleo. Serikali yenyewe inafanya kazi hiyo kupitia tume ya maadili ya viongozi wa uma. 0752558069
Reply
Post a Comment