Monday, September 08, 2014

"WAPAMBE WAMETUFITINISHA NA MBOWE" ZITTO KABWE


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akifafanua jambo. 


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameeleza tofauti yake na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akisema imesababishwa na watu aliowaita wapambe.

Zitto (37), ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, alisema kuwa hata kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama kulisababishwa na wapambe hao, lakini akasisitiza kuwa hana kinyongo tena kwa kuwa alishamwomba Mungu na sasa amesamehe kabisa.

Tofauti za wawili hao hazijawahi kutolewa hadharani licha ya mitandao mbalimbali kuzungumzia kuharibika kwa uhusiano wao ikinukuu habari kutoka vikao vya ndani vya Chadema.

Hata hivyo, mapema mwaka huu, Zitto alirushiwa tuhuma nzito na Chadema kutokana na uhusiano wake na baadhi ya makada wa CCM, lakini mbunge huyo aliyahusisha maneno hayo na mwenyekiti wake na aliandika maneno makali dhidi ya Mbowe kwenye ukurasa wake wa facebook. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SARAFU YA SH. 500 KUANZA KUTUMIKA OCTOBA

Sarafu ya Shilingi mia tano inayotarajiwa kuanza kutumika mapema mwezi oktoba. Picha na Emmanuel Herman
Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezindua rasmi sarafu mpya ya Sh500 itakayoanza kutumika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kutambulisha sarafu hiyo, mkurugenzi wa huduma za kibenki wa BoT, Emmanuel Boaz alisema Serikali imefanya uamuzi huo ili kurahisisha upatikanaji wa chenji na kutunza ubora wa fedha.
“Noti ya Sh500 ndiyo inayopitia mikononi mwa wananchi wengi hivyo kuchakaa mapema. Lakini kutokana na gharama ya kuzichapisha ukilinganisha na sarafu ambazo hudumu kwa muda mrefu, tumeamua kuziondoa noti na kuleta sarafu yenye thamani ile ile.
Kuna taratibu tunaendelea kuzikamilisha kabla hatujaziingiza sarafu hizo katika mzunguko mwezi Oktoba. Zitakapoanza kutumika hakutakuwa na haja ya wananchi kwenda kubadilisha noti walizonazo kwani zitakuwa zinatumika pamoja hadi zitakapopotea katika mzunguko,”alisema.
Sarafu hiyo ina umbo la duara, lenye kipenyo cha milimita 27.5 na michirizi pembeni ikiwa na uzito wa gramu 9.5. Mbele ina picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume na nyuma ni nyati. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 08, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WEZI WA GARI LA RAIS WAFIKISHWA MAHAKAMANI



Gari la msafara wa Rais Kenyatta lilipatikana mjini Kampala Uganda

Watu watano akiwemo raia mmoja wa Uganda pamoja na fundi mmoja wa magari wameshitakiwa kwa kosa la wizi wa gari la msafara wa ulinzi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini Kenya.
Watano hao pia walishitakiwa kwa kumuibia gari inspekta wa polisi David Machui aliyekuwa akiendesha gari hilo aina ya BMW 735 tarehe 26 mwezi Agosti mjini Nairobi lilipoibwa.
Washukiwa hao wote walikanusha madai hayo kwamba walihusika katika wizi wa gari hilo.
Kila mshukiwa aliachiliwa kwa kima cha shilingi milioni 5 isipokuwa mwanamume mmoja aliyesemekana kuwa na kesi tofauti mahakamani.
Raia wa Uganda Robert Mande Ochan, aliamrishwa na mahakama kutoa dhamana ya shilingi milioni mbili ili aweze kuachiliwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA AU

Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti kuhusu udhalilishwaji kijinsia wanaofanyiwa wanawake nchini Somalia na askari wa kulinda amani nchini humo.Majeshi hayo yamo nchini Somalia yakiwakilisha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kupambana na wapiganaji wa kikundi cha Kiislam cha Al Shaabab.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamula Human Rights Watch limesema liliwahoji wanawake 21, wakiwemo wasichana waliobakwa na wanajeshi hao mwaka 2013.
Visa vingi vimeripotiwa katika kambi zinazosimamiwa na wanajeshi wa Burundi na Uganda.
Walinda amani wa Muungano wa Afrika wamedaiwa katika ripoti hiyo, kutumia chakula cha misaada kushawishi wasichana na wanawake kufanya mapenzi nao.
Wanajeshi hao wanadaiwa pia kuwabaka ama kuwadhalilisha kingono wanawake waliofika katika kambi hizo kuomba msaada wa matibabu au maji. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LIONEL MESSI AMGARAGAZA CRISTIANO RONALDO TUZO YA FIFA 15, LIGI KUU ENGLAND

1410107894477_wps_32_image001_png
Mcheza bora wa dunia: EA Sports wamemuweka nyota wa Barcelona, Lionel Messi kuwa namba moja katika michezo mipya ya FIFA 15
CRISTIANO Ronaldo alimgaragaza Lionel Messi katika tuzo ya  Ballon d’Or mapema mwaka huu,lakini nyota huyo wa Barcelona amelipa kisasi kwa mpinzani wake huyo mkubwa kwa kushinda tuzo nyingine.
Akiwa amepata pointi 93 kati ya 100, messi amekuwa namba moja katika tuzo ya michezo ya Video ya FIFA, (FIFA 15) ambayo itatangazwa rasmi septemba 26 mwaka huu huko UK.
Ili kuwapa nafasi mashabiki kupiga kura kabla, waendeshaji wa tuzo hiyo, EA Sports walitangaza majina ya wachezaji 50.
Wanted man: Barcelona are sure to prove popular on the new game given Messi's eye catching statistics

MORIS AREJEA MAZOEZINI TAYARI KWA KUIKABILI YANGA


BEKI tegemezi wa Azam FC,Aggrey Moris leo ameanza mazoezi na timu yake kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga uliopangwa kufanyika Jumapili hii uwanja wa taifa..
Meneja wa Azam FC,Jemedari Said amesemeiambia Father Kidevu Blog kuwa Moris ameanza mazoezi na kikosi hicho baada ya kupona Malaria iliyomsumbua kwa wiki moja.
Moris hakuweza kusafiri na kikosi cha Taifa Stars juzi kutokana na kusumbuliwa na maradhi hayo na baada ya kupona anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha Azam kitakacho pambana na Yanga Jumapili. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

OKWI HURU KUCHEZA SIMBA


Wajumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF wakiwa katika mkutano jijini Dar es Salaam jana. 


Utata wa Emmanuel Okwi umemalizwa rasmi na mchezaji huyo wa Uganda sasa yupo huru.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilikutana jana na kupitia masuala mbalimbali ikiwamo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.

Mkataba huo ulipitiwa na kamati ikiwamo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa mkataba wa pande mbili haupo kwa sababu Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.

“Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote,” alisema Wambura.

Alifafanua kuwa mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...