Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti kuhusu udhalilishwaji kijinsia wanaofanyiwa wanawake nchini Somalia na askari wa kulinda amani nchini humo.Majeshi hayo yamo nchini Somalia yakiwakilisha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kupambana na wapiganaji wa kikundi cha Kiislam cha Al Shaabab.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamula Human Rights Watch limesema liliwahoji wanawake 21, wakiwemo wasichana waliobakwa na wanajeshi hao mwaka 2013.
Visa vingi vimeripotiwa katika kambi zinazosimamiwa na wanajeshi wa Burundi na Uganda.
Walinda amani wa Muungano wa Afrika wamedaiwa katika ripoti hiyo, kutumia chakula cha misaada kushawishi wasichana na wanawake kufanya mapenzi nao.
Wanajeshi hao wanadaiwa pia kuwabaka ama kuwadhalilisha kingono wanawake waliofika katika kambi hizo kuomba msaada wa matibabu au maji. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment