Mcheza bora wa dunia: EA Sports wamemuweka nyota wa Barcelona, Lionel Messi kuwa namba moja katika michezo mipya ya FIFA 15
CRISTIANO
Ronaldo alimgaragaza Lionel Messi katika tuzo ya Ballon d’Or mapema
mwaka huu,lakini nyota huyo wa Barcelona amelipa kisasi kwa mpinzani
wake huyo mkubwa kwa kushinda tuzo nyingine.
Akiwa
amepata pointi 93 kati ya 100, messi amekuwa namba moja katika tuzo ya
michezo ya Video ya FIFA, (FIFA 15) ambayo itatangazwa rasmi septemba 26
mwaka huu huko UK.
Ili kuwapa nafasi mashabiki kupiga kura kabla, waendeshaji wa tuzo hiyo, EA Sports walitangaza majina ya wachezaji 50.
FIFA 15 TOP 10 PLAYERS
Messi amemshinda Ronaldo kwa tofauti ya pointi moja nyota wa Real Madrid aliyepata alama 92 hasa katika uwezo wa kufunga mabao.
Nyota wa Bayern Munich na Uholanzi Arjen Robben ameshika namba tatu kwa pointi zake 90.
Takwimu
hizo zinazozingatia zaidi kiwango cha mchezaji katika mechi za ligi na
makombe katika siku 365 zilizopita, zinaonesga uwezo wa kila mchezaji
kila anapotumika katika mechi.
Mshambuliaji
wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic na kipa wa Bayern Munich,
Manuel Neuer wameshika nafasi ya nne na tano, licha ya kupata pointi
sawa na Robben.
Nyota
wawili wa Barca, Andres Iniesta naLuis Suarez – ambao wote wamepewa
alama 89 wanakalia nafasi ya sita na saba, wakati nyota wawili wa Bayern
Munich, Bastian Schweinsteiger na Franck Ribery (wote pointi 88)
wanashika nafasi ya nane na tisa.
Winga
wa Chelsea, Eden Hazard, waliyepata pointi 88 mwaka jana, ni mchezaji
pekee wa ligi kuu England aliyeingia 10 bora, akiwazidi kete nyota wa
Manchester United Robin van Persie na Radamel Falcao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment