Wednesday, May 28, 2014

WANACHAMA WA SIMBA WAANDAMANA NA KUFUNGA NJIA ZA MSIMBAZI WAKITAKA WAMBURA ARUDISHWE KWENYE ORODHA YA WAGOMBEA



Mashabiki wa Timu ya Simba wakijikusanya nje ya jengo la klabu hiyo kongwe kupinga Wambura kuondolewa kwenye uchaguzi unakuja hivi karibuni.
Hapa mashabiki wakizidi kujikusanya kwa wingi mchana huu.
Wanachama wa simba wakiwa wamelizunguka Jengo la klabu yao mchana huu kupinga kuondolewa kwa wambura kwenye uchaguzi wa klabu hiyo.
Wanachama wa Simba wakipiga kelele nje ya jengo la klabu yao hiyo wakitaka wapewe ufafanuzi wa kina kwanini Wambura ametolewa kwenye uchaguzi unaokuja. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MBUNGE WA NKASI NUSURA APIGWE NJE YA UKUMBI WA BUNGE...!!!




Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Mohamed Kessy (kushoto) akiwakwepa wabunge wa CUF, Kombo Khamis Kombo (kulia) na Ibrahim Mohammed Sanya (wa pili kushoto) walipokuwa wakimfokea nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana na Mbunge wa Mikumi, Abdulsalaam Amer akijalibu kuwazuia. Picha na Edwin Mjwahuzi 

Na Fidelis Butahe na Sharon Sauwa, Mwananchi

Kelele, kukunjana na kunyoosheana vidole jana mchana vilitawala nje ya ukumbi wa Bunge wakati wabunge wa CUF kutoka Zanzibar walipotaka ‘kumkanya’ Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy.

Sakata hilo la aina yake lililodumu kwa takriban dakika 15 lilitokea saa 7:05 mchana baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuahirisha kikao cha Bunge.

Wabunge hao Mussa Haji Kombo (Chakechake), Kombo Khamis Kombo (Magogoni) na Muhammad Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe), walitaka ‘kumkanya’ Keissy kutokana na kile alichosema alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka 2014/15 na kusema Zanzibar haichangii katika Muungano, hivyo haina haki ya kuhoji mambo ya upande wa pili.

Kauli hiyo licha ya kulalamikiwa na wabunge wote wa CUF kutoka Zanzibar kiasi cha kufikia hatua ya kusimama na kuomba mwongozo wa Spika, Keissy alizidi kuwashambulia na kusema kuwa majimbo ya Zanzibar watu wake wanaweza kukusanywa sehemu moja kwa kupigiwa filimbi tu.

“Nyie Zanzibar idadi yenu ya watu ni asilimia 2.8 ya watu wote wa Tanzania. Sasa mnataka kupata kila kitu sawa ili iweje! Mnataka ajira asilimia 21 na Watanganyika wakafanye kazi wapi?” alisema Keissy.

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho na wabunge kuanza kutoka nje, wabunge hao wa CUF walikwenda kumsubiri Keissy karibu na jengo la kantini. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

DEREVA APORWA LORI LA MAFUTA AKIWA KWENYE FOLENI MIZANI


Picha na Maktaba

Watu watano wasiofahamika wanaodhaniwa ni wezi, wamemvamia dereva wa lori la mafuta, Stephano John eneo la Kibamba, Barabara Kuu ya Dar es Salaam -Morogoro alipokuwa katika foleni na kisha kumpiga, kumjeruhi sehemu kadhaa za mwili, kumfunga kamba na kumtupa mtaroni.

Ilielezwa kuwa baada ya kumfunga kamba, wahalifu hao walimdhibiti ndani ya lori na kutembea naye umbali wa kilomita moja walipofika maeneo ya Kiluvya ambako walimtupa katika mtaro na kuendelea na safari. Walifika mizani Kibaha wakapima uzito wa gari kama kawaida na kutokomea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea saa mbili usiku wakati dereva huyo akiwa kwenye foleni na lori lake aina ya Scania lililokuwa na tela pia lilikuwa na shehena ya petroli lita zaidi ya 39,000.

“Wakati dereva akiwa katika mwendo wa polepole kwenye foleni ya malori kuingia mizani, alivamiwa ghafla na watu watano waliofungua mlango na kuingia ndani.

“Wakati dereva akishangaa, walimnyanyua kwenye kiti na kumweka kiti cha nyuma na wakimtaka kukaa kimya,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

PAPA FRANCIS, WAZIRI MKUU WA ISRAEL WALUMBANA KUHUSU YESU




Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.PICHA|MAKTABA 

Malumbano makali ya maneno na hoja yamezuka baina ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusu lugha gani aliyotumia Yesu Krtisto miaka 2,000 iliyopita.

Viongozi hao Jumatatu mchana wakati wa ziara ya siku tatu ya Papa aliyoifanya katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu atwae wadhifa huo. “Yesu aliishi hapa katika ardhi ya nchi hii. Alizungumzia Kiebrania,” alianza Netanyahu wakati akimweleza Papa Francis kwenye mkutano wa hadhara mjini Yerusalemu.

Netanyahu, pia akaeleza kuwa upo uhusiano wa karibu baina ya mahali alikozaliwa Yesu na Ukristo. Naye Papa Francis akasikiliza kwa muda, kisha akajibu: “Yesu alizungumza lugha ya Kiaramaiki.”

“Ndiyo, nimesema alizungumza Kiaramaiki, lakini pia alijua Kiebrania,” akaingilia kati Netanyahu.

Hata hivyo, mjadala huo umepokewa kwa hisia tofauti na watu wengi ambao wamekuwa wakifuatilia ziara ya siku tatu ya Papa Francis katika nchi takatifu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 28, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

OBAMA ATANGAZA WANAJESHI 10, 000 KUBAKI AFGHANISTAN

Rais Obama akitangaza kubakia kwa wanajeshi 10,000 Afghanistan katika Ikulu ya White House Mei 27, 2014.
Rais Barack Obama ametangaza kuwa Marekani itaendelea kuwa na wanajeshi 10,000 nchini Afghanistan baada ya mwisho wa mwaka 2014. Alitangaza kuwa Marekani kisha itaendelea kuwapunguza wanajeshi hao ili kufikia mwaka 2016 kuwe kumebakia na wanajeshi wachache sana.
Rais Karzai amekuwa akipinga kila hatua au pendekezo linalotolewa na maafisa katika utawala wake hasa kuhusiana na uwezekano wa kuendelea kuwepo na wanajeshi wa Marekani nchini humo baada ya mwisho wa mwaka huu. Wakuu wake wa kijeshi, washauri wa maswala ya usalama na Mawaziri wake wengi, wangalitia sahihi mapatano ya usalama na Marekani mwaka uliopita.
Lakini yeye, hata baada ya kuitisha mkutano wa wazee uliotazamiwa kuidhinisha mapatano hayo alikiuka matarajio ya wengi na kusema kuwa hatii sahihi mapatano hayo.
Wagombeaji wa Urais wawili waliosalia kwenye kinyanganyiro cha Urais kuchukua nafasi yake Karzai wanaunga mkono mapatano ya usalama na Marekani na hiyo ndiyo sababu Rais Obama ametoa tangazo lake kuhusu wanajeshi watakaobakia nchini humo, ikiwa yamebakia majuma mawilli kabla ya awamu ya mwisho ya upigaji kura nchini humo.
Hata hivyo kusita kwa Rais Karzai kutia sahihi mapatano hayo kumeimarisha kampeni ya wale nchini Marekani wasiotaka kuendelea kuwepo wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.
Sasa wanajeshi watakaobakia Afghanistan watakuwepo kwa mwaka mmoja pekee kabla ya kupunguza idadi hiyo kwa nusu halafu baadaye kupunguza hadi sufuri ifikapo mwisho wa mwaka 2016. Maoni ya wengi hapa ni kuwa ni heri wanajeshi wa Marekani waendelee kuwa nchini humu kwa muda mrefu zaidi.
Mapigano yametokea nchini humu mara kwa mara hivi kwamba kuwepo kwa wanajeshi wa kigeni nchini kungetoa hakikisho zaidi kwa wananchi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC

AL-SHABAAB WAKIRI KUSHAMBULIA DJIBOUTI

Hali ilivyokuwa baada ya kushambuliwa kwa Bunge nchini Somalia
Al Shabaab wamesema katika taarifa kuwa kwa kushambulia mgahawa huo, walikuwa wakiwalenga raia wa mataifa ya Magharibi wanaopendelea kuutembelea Djibouti.
Kundi hilo liliwalaumu Wafaransa - walio na kambi kubwa ya wanajeshi nchini Djibouti - kwa kuwadhulumu Waislamu katika Jamhuri ya Africa ya Kati (CAR) na kwa kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Djibouti walio katika kikosi maalumu cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika, AMISON, nchini Somalia.
Al Shabaab pia walilaumu Djibouti - ambayo ni mwenyeji wa vituo kadhaa vya kijeshi vya mataifa ya Magharibi, kukiwemo Marekani - kwa kuruhusu mataifa ya Magharibi kutumia taifa lao kama sehemu ya kushambulia Waislamu.
Al Shabaab wamepunguzwa makali nchini Somalia tangu kuanzishwa kwa msukumo wa kijeshi wa kukabiliana nao wa Serikali ya Somalia na wanajeshi wa AMISOM.
Hata hivyo kundi hilo halijaishiwa na uwezo wa kushambulia. Mnamo Jumanne wanajeshi kadhaa wa Ethiopia waliuawa baada ya kuvamiwa na Al Shabaab katika eneo la Bakol.
Na Jumamosi, walishambulia Bunge katika mji mkuu wa Mogadishu.
Kwa kuwa kundi hilo tayari linaweza kushambulia nchini Kenya na sasa limechipukia Djibouti, ni ishara kamili kuwa limeanza kuwa tatizo katika eneo zima, mbali na kushambulia taasisi mbalimbali nchini Somalia. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC Swahili

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...