Tuesday, January 13, 2015

"WALIOJITOKEZA KUWANIA URAIS CCM HAWANA SIFA" KINGUNGE


Mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombare Mwiru akizungumza na wanahabari. Picha na Maktaba 

Harakati za kuwania urais ndani ya CCM zimeingia katika hatua mpya baada ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale - Mwiru kuibuka na kudai kuwa wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo hawana sifa kwa kuwa wanatumia fedha kutaka kuingia Ikulu.
Kauli ya mwanasiasa huyo ambayo imekuja siku moja kabla ya Kamati Kuu ya CCM kukutana leo mjini Unguja na moja ya ajenda ikitajwa kuwa suala la maadili, inaweza kuwa mwiba mchungu kwa wanasiasa hao ambao wanaongezeka kila kukicha.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kingunge alisema: “Kuna suala la kukosa uadilifu, kuna suala la matumizi ya pesa na nikwambie ukweli, hao wanaotangaza urais wote wanatumia pesa, wanatumia faulo mbalimbali na wananchi wanajua.” Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

AFRIKA YAJIFUNGULIA MTANDAO WAKE WA AFRILEAKS

Afrileaks utakuwa kamna mtandao wa Wikileaks ambao kazi yake ni kufichua ufisadi 
 
Mtandao mpya mfano ule wa Wiki Leaks , unaolenga kutangaza visa vya ufisadi umezinduliwa barani Afrika. Mtandao huo kwa jina 'Afri Leaks' unanuiwa kutumiwa kulinganisha na kutangaza wazi visa vya ufisadi katika bara nzima.
Kile Afrileaks inaahidi ni mfumo wa hali yajuu wa kama posta mtandaoni ambapo mtu anaweza kuutumia kufichua habari za siri lakini muhimu kwa jamii bila wao wenyewe kujulikana.
Mwenye habari nyeti ataweza kuzipeleka kwa vyombo vya habari kote barani Afrika ambavyo wamejiridhisha navyo kwamba viko huru na wana uhariri wa hali ya juu unaotambulika kimataifa.
Mojawapo ya Maswala yanayowakera wengi ambayo huenda yakapata kuchipuliwa kwa wingi iwapo mfumo huo wa Afrileaks utafana , ni kashfa za ufisadi.
Licha ya kuwa na viwango vya kuridhisha vya ukuaji wa uchumi,Mataifa mengi ya Afrika hata yale yaliyo na utulivu wa kisiasa hupoteza mabillioni ya fedha kila mwaka kutokana na ufisadi uiokithiri, huku taasisi hafifu zikibuniwa bila kuwa na nia ya dhati ya kukabiliana na rushwa. .
Ufisadi ni jinamizi kubwa barani Afrika
Lakini Je Afrileaks wataweza kupata umaarufu kama ule wa wikileaks?
Shirika hilo la Afrileaks linasisitiza kuwa halitachapisha habari zozote za kibanfsi za mfichua siri.
Na kwamba lengo lao ni kuwaunganisha wenye taarifa muhimu na waandishi habari wanaoandika makala zilizopelelezwa na kuchunguzwa kwa kina. Pia wameahidi kutoa mafunzo zaidi kwa waandishi habari waliobobea ili kufahamu vyema vipi kuzishughulikia taarifa kama hizo.
Mashirika kadhaa ya habari barani Afrika tayari yameshajisajili na Afrileaks -ikiwemo kutoka nchini Zimbabwe, Mozambique, Angola na Botswana.
Hivyo wenye habari nyeti ambazo alikuwa anatafuta kwa kuzipeleka bila kutambuliwa anahimizwa kuziwasilisha kwa tovuti hiyo ya Afrileaks lakini wanapaswa kufuata utaratibu uliowekwa na wala wasitumie computer za ofisini mwao ili kutotambulika na kujiweka katika hatari.
Je nani atakuwa wa kwanza kujitosa na habari moto moto katika Afrileaks! Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC Swahili

KAMANDA WA LRA KUFIKISHWA ICC

Muasi Ongwen
Kamanda wa kundi la waasi la LRA nchini Uganda ambaye alijisalimisha katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Dominic Ongwen atakabidhiwa kwa mahakama ya kimataifa ya ICC, yasema serikali ya Uganda.
Kamanda huyo ni miongoni mwa watu wa kundi la LRA wanaosakwa na viongozi wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Waasi wa Seleka walioko katik Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako Ongwen alikamatwa walisema kuwa muasi huyo alikamtwa ingawa wanajeshi wa Marekani wanasema kuwa alijisalimisha.
Msemaji wa jeshi la Uganda, ameambia shirika la habari la Reuters kwamba Ongwen atakabidhiwa ICC na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako alijisalimisha.
Ongwen alikabidhiwa wanajeshi wa Marekani wiki jana na bado anazuiliwa na wanajeshi hao.
Marekani ilikuwa imeahidi kutoa kitita cha dola miliono 5 kama zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa kamanda huyo, kuhamishwa kwake na hatimaye kufunguliwa mashitaka.
Maafisa wakuu nchini Uganda wanasema kwamba Ongwen atapelekwa nchini Uganda katika siku chache zijazo.
Anajaulikana kwa jina "White Ant", jina lake la msituni na yeye ndiye naibu kamanda wa kundi la LRA Joseph Kony ambaye pia anasakwa na mahakama ya kimataifa ya ICC.
Kundi la LRA liliwateka nyara maelfu ya watoto na kuwalazimisha kupigana huku wasichana wakifanywa watumwa wa ngono. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...