Thursday, December 18, 2014

PROFESA TIBAIJUKA: SINA HATIA, SIWEZI KUJIUZULU


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka 

Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.

Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye hajahusika na jambo lolote.

“Huu uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote ya mimi  kujiuzuru kwa kuwa sijahusika kwa namna yeyote kwenye sakata hili la Escrow” anasema Profesa Anna Tibaijuka. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

RAIS KIKWETE AKATISHA ZIARA YA PINDA UARABUNI


Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda, hivi karibuni. Picha na Maktaba 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

ASILIMIA 97 WACHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015

 
Jumla ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliohiyimu elimu ya msingi mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani.

Idadi hiyo ni sawa an asilimia 97 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa waandishi wa habari leo imesema ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na mwaka jana.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 18, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

POLISI WAZUIA MAZISHI YA AISHA MADINDA HADI KESHO


Jeshi la polisi limezuia mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Madinda hadi hapo mwili wake utakapofanyiwa uchunguzi kutokana na utata wa kifo chake.
Akizungumza na Mwananchi, dada wa marehemu, Hamida Mbegu alisema Polisi waliwaambia kuwa mwili huo unahitaji kufanyiwa vipimo ili kubaini sababu za kifo chake, japokuwa familia haikuwa tayari kwa jambo hilo.
Alisema Polisi walisisitiza kuwa ni lazima mwili ufanyiwe vipimo kutokana na kuwapo kwa utata wa kifo hicho.
Hamida amesema kwa mujibu wa polisi vipimo vitafanyika asubuhi, hivyo baada ya vipimo kumalizika mwili utapelekwa Kigamboni ambako ndiyo familia imekusanyika na baada ya swala ya Ijumaa utazikwa kwenye makaburi ya familia yaliyopo Kibada, Kigamboni.
Akizungumzia suala hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, alisema kuwa kutokana na mazingira ya kifo hicho ni lazima Polisi wajiridhishe kwa kuufanyia mwili vipimo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

WABUNGE WARUSHIANA NGUMI BUNGENI...!!!

Wabunge wakiwa katika vikao bungeni 
Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bungeni na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.
Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani walipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.


Seneta Johnston Muthama alijipata pabaya kwani long'i yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo.
 
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year. 

NAIBU SPIKA AMWAGIWA MAJI BUNGENI

 Naibu spka Joyce Laboso ambaye amemwagiwa soda 
 
 Kikao cha adhuhuri cha wabunge nchini Kenya, kinaendelea kuzua hisia kali huku wabunge wakiendelea kuvurugana humo.
Wabunge hao wanajadili mswada tatanishi wa usalama ambao upande wa upinzani unasema unakwenda kinyume na katiba na kuwanyima wakenya haki yao ya kujieleza.
Mmoja wa wabunge hao wa upinzani amemwagia soda naibu spika Joyce Laboso ambaye alikuwa anasimamia kikao hicho cha kufanyia mswada huo mabadiliko kabla ya kupitishwa.
Spika wa bunge hilo sasa amechukua usukani na kuamuru kutimuliwa kwa wabunge wawili waliokuwa wamezidi vurugu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

WATU 33 WAUAWA, 100 WATEKWA NIGERIA

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram  

Wanamgambo wamevamia kijiji kimoja kazkazini mashariki mwa Nigeria na kuwaua takriban watu 33 na kuwateka wengine 100,mmoja ya waathiriwa amesema.
Amesema kuwa washukiwa wa kundi la Boko haram waliwakamata vijana wadogo,wanawake na watoto kutoka kijiji cha Gumsuri.
Shambulizi hilo lilitokea siku ya jumapili lakini habari hizo zilibainika baada ya waathiriwa kufika mji wa Maiduguri.
Wakati huohuo,jeshi la Cameroon limesema kuwa limewaua wanamgambo 116 ambao walikuwa wameshambulia kambi moja ya kijeshi kulingana na AFP.
Moja ya vijiji vilivyoavamiwa na wanamgambo wanaodaiwa kutoka kwa kundi la Boko haram
Wakaazi wameiambia BBC kwamba wanamgambo waliojihami na silaha walishambulia eneo la mpakani la Amchide siku ya jumatano,walipowasili kwa magari mawili huku wengine wakitembea.
Walivamia eneo la soko na kuchoma maduka na zaidi ya nyumba 50.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo lakini maafisa wamelaumu wapiganaji wa Boko Haram.
Zaidi ya watu 2000 wameuawa katika ghasia za makundi yaliojihami na silaha mwaka huu pekee,hususan kazkazini mwa Nigeria karibu na mpaka na Cameroon. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...