Thursday, December 18, 2014

WATU 33 WAUAWA, 100 WATEKWA NIGERIA

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram  

Wanamgambo wamevamia kijiji kimoja kazkazini mashariki mwa Nigeria na kuwaua takriban watu 33 na kuwateka wengine 100,mmoja ya waathiriwa amesema.
Amesema kuwa washukiwa wa kundi la Boko haram waliwakamata vijana wadogo,wanawake na watoto kutoka kijiji cha Gumsuri.
Shambulizi hilo lilitokea siku ya jumapili lakini habari hizo zilibainika baada ya waathiriwa kufika mji wa Maiduguri.
Wakati huohuo,jeshi la Cameroon limesema kuwa limewaua wanamgambo 116 ambao walikuwa wameshambulia kambi moja ya kijeshi kulingana na AFP.
Moja ya vijiji vilivyoavamiwa na wanamgambo wanaodaiwa kutoka kwa kundi la Boko haram
Wakaazi wameiambia BBC kwamba wanamgambo waliojihami na silaha walishambulia eneo la mpakani la Amchide siku ya jumatano,walipowasili kwa magari mawili huku wengine wakitembea.
Walivamia eneo la soko na kuchoma maduka na zaidi ya nyumba 50.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo lakini maafisa wamelaumu wapiganaji wa Boko Haram.
Zaidi ya watu 2000 wameuawa katika ghasia za makundi yaliojihami na silaha mwaka huu pekee,hususan kazkazini mwa Nigeria karibu na mpaka na Cameroon. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...