Wednesday, February 05, 2014

MTIBWA SUGAR KUWAKARIBISHA SIMBA UWANJA WA JAMHURI LEO MOROGORO

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 16 leo (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi tano huku Mtibwa Sugar ikiikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kiingilio katika mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000 tangu uanze mzunguko wa pili wa VPL kitakuwa sh. 5,000. Jonisia Rukyaa kutoka Bukoba ndiye atakayechezesha mechi hiyo.
Mechi nyingine za ligi hiyo ni Tanzania Prisons vs Coastal Union (Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na JKT Ruvu vs Ashanti United (Chamazi, Dar es Salaam).
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

TANZANIA YAKAMATA DAWA ZA KULEVYA ZAIDI YA KILO 200

http://jambotz8.blogspot.com/
Polisi nchini Tanzania wamekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo 201 katika eneo la bahari kati ya Dar es Salaam na Zanzibar nchini humo.
Kamanda wa kikosi maalum cha kuzuia dawa za kulevya Godfrey Nzowa ameiambia BBC kuwa Watu 12 wanashikiliwa kuhusiana na shehena hiyo.
Kamanda Nzowa amesema dawa hizo za kulevya zimekamatwa na Polisi wa doria baharini muda wa saa sita usiku wa kuamkia Jumanne zikisafirishwa katika Jahazi.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa Shehena hiyo ilikuwa ikitoka nchini Iran kuelekea nchi au eneo ambalo mpaka sasa bado halijafahamika.
Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kukamata dawa za kulevya aina mbalimbali kupitia viwanja vya ndege,nchi kavu na baharini, ambapo mwaka jana kiasi kikubwa cha dawa za kulevya zilizokamatwa ziliteketezwa.
CHANZO:BBC
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 


MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 05, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

NEC KUTANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA

malaba1 38164
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema wiki hii itatangaza tarehe ya uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga, lililopo wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wake, Dk William Mgimwa (CCM) kufariki dunia Januari Mosi mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Licha ya Kalenga, tume hiyo imesema uchaguzi mdogo pia utafanyika Jimbo la Chalinze baada ya Mbunge wake, Said Bwanamdogo (CCM) kufariki dunia Januari 22 mwaka huu.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba alisema uchaguzi mdogo hauwezi kufanyika kama jimbo litakuwa wazi miezi 12 kabla ya Uchaguzi Mkuu.
"Wabunge hawa wamefariki dunia ikiwa imebaki miezi zaidi ya 12 kabla ya Uchaguzi Mkuu na kuvunjwa kwa Bunge, hilo
linamaanisha chaguzi zitafanyika na wiki hii NEC itatangaza tarehe ya uchaguzi jwa Kalenga," alisema Malaba.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

LIBYA YAHARIBU SILAHA ZA SUMU

libya1_43539.jpg
Libya imekamilisha uharibifu wa silaha za kemikali katika mpango ulioanza miaka tisa iliyopita chini ya uongozi wa aliyekuwa rais, Muammar Ghaddafi.
Tangazo hilo lilipitishwa katika mkutano wa wanahabari uliofanyika Jijini Tripoli na kuhudhuriwa na wajumbe wa kimataifa .
Ikisaidiwa na Marekani, Ujerumani, na Canada, Libya imeharibu shehena ya sumu ya mvuke pamoja na silaha nyengine zenye sumu.
Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Shirika la Silaha za kemikali zilizopigwa marufuku amepongeza Libya kwa kuchukua hatua hiyo muhimu.
Amesema kwamba hatua hiyo ni mfano mwema wa ushirikiano wa kimataifa ambao unaigwa na taifa la Syria kwa kiwango kikubwa.
Kwenye mkutano huo waziri wa maswala ya kigeni nchini Libya ameeleza kwamba hatua hiyo ni ya kihistoria na ni mafanikio kutokana na ushirkiano na washirika wa kimataifa.
Mnamo mwaka wa 2004,Libya ilikuwa na takriban tani 13 za sumu ya mvuke.
Mrundiko huo wa kemikali hatari kwa sasa umeharibiwa.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...