Saturday, April 02, 2016

MAKONDA ATANGAZA NEEMA KWA BODABODA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na waendesha bodaboda na kuahidi kushugulikia kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa vikwazo vya wao kuingia katikati ya jiji.

Aidha, amewaahidi kuwapatia pikipiki kwa marejesho ya  Sh25,000 kwa wiki  kwa muda maalum kabla ya kuwaachia kabisa.

Kwa mantiki hiyo, Makonda amewataka kufanya usajili upya na kusajili vituo vyao ili watambulike kisheria huku akisema atawapatia mavazi maalum 'reflectors' kama utambulisho.

Awali, mmoja wa waendesha bodaboda hao, Daud Laurian alimsomea RC Makonda risala iliyoainisha matatizo yao ikiwemo zuio la ya jiji kutokana na agizo la aliyekua  mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick Machi 3, 2014.

Waendesha hao wamehaokikishia Makonda kuwa raia wema katika suala zima la ulinzi iwapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum litawachukulia kama ndugu zao na marafiki.

KONDAKTA ALIETISHIA KUMUUA MAGUFULI ASHTAKIWA

Kondakta wa daladala amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli.

Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji, alidaiwa kutenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto, maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Wakili wa serikali Keneth Sekwao aliambia mahakama Alhamisi kuwa mshtakiwa, akiwa katika baa hiyo, alitishia kumuua Dkt Magufuli kwa maneno kwa njia ya kujitoa mhanga. 

“Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli, mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alinukuliwa na Wakili Sekwao. Mshtakiwa alikana shtaka hilo 

Hakimu Mkazi, Hellen Liwa aliweka wazi dhamana ya mshtakiwa huyo na kumtaka kutafuta wadhamini wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni. Alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na akawekwa rumande hadi 14 Aprili kesi ikatapotajwa tena.

BOKO HARAM WAAPA KUTOSALIMU AMRI

 Abubakar Shekau kiongozi wa Boko Haram

 Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wametoa kanda mpya ya video wakiapa kuendeleza vita vya kutaka uongozi wa sheria za kiislamu. 

'Lazima mujue kwamba hakuna ukweli, hakuna majadiliano,hakuna kusalimu amri'', alisema mtu mmoja aliyejifunika uso na kuzungumza kwa lugha ya hausa.

 Ujumbe huo unajiri baada ya kanda ya video isiojulikana mwezi uliopita kumuonyesha kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau akionekana dhaifu swala linaloongeza uvumi kwamba mda wake katika uongozi wa kundi hilo unaelekea ukingoni.

 Katika kanda hiyo ya video kuna watu wamesimama na bunduki za AK-47 mbele ya magari.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...