Wednesday, November 25, 2015

BARAZA LA MAWAZIRI LABADILISHWA...!!!


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, na kuwaacha wote wizara zao zilizotajwa katika ufisadi. 

Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa.

Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni. Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni, Rais Uhuru Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka kumi na tisa hadi ishirini na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora zaidi .

KILIMANJARO STARS YACHINJA MTU CECAFA...!!!


Wachezaji wa Kilimanjaro Stars

Michuanao ya Cecafa Chalenji Cup Imeendelea tena jana kwa michezo miwili katika hatua ya makundi. Zanzibar ilifungwa bao 4-0 na Uganda ikiwa ni Mechi ya Kundi B.

Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imeichapa Rwanda bao 2-1 katika mchezo uliopigwa mjini Awassa na kupaa kileleni mwa Kundi A wakiwa na Pointi 6 kwa Mechi 2 na kujihakikishia kucheza hatua ya Robo Fainali.

Mabao ya Kilimanjaro stars yalifungwa na Said Ndemla pamoja na Simon Msuva huku bao la Rwanda likifungwa na mchezaji Tisiyege.

Michuano hiyo itaendelea tena leo jumatano kwa mechi kadhaa ambapo Kenya itachuana na Burundi.

Somalia itaivaa Ethiopia, Malawi itaikabili Djibouti na Sudan kusini watachuana na ndugu zao Sudan.

BARCELONA YAIZIMA AS ROMA


Mchezaji wa As Roma

Barcelona wakiwa nyumbani walichomoza na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya As Roma.

Buyen Munich wakiichapa Olympiakos bao 4-0, Maccabi Tel Aviv wakila hio kwa Chelsea kwa kichapo cha mabao 4-0. 

BATE Borislov wakifungana bao 1-1 na Buyer Liverkusen , FC Porto wakilala bao 2-0 dhidi ya Dynamo Kiev, Zenit St P wakiichapa Valencia bao 2 – 0 na Lyon wakilala mbele ya KAA Gent bao 2-1.

ANDY MURRY TAYARI KWA DAVIS CUP


Kikosi cha Timu ya Tennis ya Uingereza

Timu ya Taifa ya Uingereza ya Tenis, imewasili nchini Ubegiji kwa mchezo wa fainali ya Davis Cup utakaopigwa ijumaa nchini humo. 

Timu hiyo inaongozwa na Andy Murray imewasili chini ya uangalizi wa ulinzi mkubwa kufuatia tishio la matukio ya kigaidi ambayo yameonekana kutishia amani nchini ubelgiji.

Timu hiyo inayojulikana pia kama Great britain ilipaswa kufika nchini humo tangu Jumapili lakini ikaahirisha kutokana na masuala ya kiusalama zaidi.

 Kikosi cha Uingereza kinawakilishwa na Andy Murray, Jamie, Kyle Edmund, Dominic Inglot na James Ward ambao tayari wapo nchini Ubelgiji.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...