Friday, July 24, 2015

WAJUMBE WA CCM WAPATA AJALI, MMOJA AFARIKI


Mtu mmoja amefariki Dunia baada ya basi Dogo aina ya toyota HIACE, lililokuwa limewabeba wajumbe wa chama cha mapinduzi wa kata ya Milanzi kwenye manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, waliokuwa kwenye kampeni za kura za maoni za udiwani kuacha njia na kupinduka, ambapo pia ajali hiyo imeacha majeruhi kumi na moja.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga, mwenyekiti wa CCM wa kata ya milanzi Bw. Edgar Mwanandenje ambaye ni miongoni mwa majeruhi hao, amesema walikuwa wakitokea kwenye mchakato wa kampeni ya kura za maoni katika kata yao, ndipo dereva wa basi hilo dogo alipolazimisha kuipita kwa kasi pikipiki aina ya bajaj iliyokuwa mbele yao, na kupoteza mwelekeo kabla ya kupinduka. 

Katibu wa ccm wilaya ya sumbawanga mjini Bw Gabriel Kiula akiongelea juu ya ajali hiyo,amemtaja aliyepoteza maisha kuwa ni Didas Mwanisenga aliyekuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya kata ya milanzi, huku kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw. Jacob Mwaruanda akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

EU YAJADILI KUKATA MISAADA BURUNDI


Bendera ya Burundi

Muungano wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kukata msaada wake nchini Burundi. Inakisiwa kuwa fedha kutoka muungano huo unafikia zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya Burundi ya kila mwaka. 

Mkuu wa masuala ya kigeni wa Muungano wa EU Federica Mogherini, ameelezea wasiwasi wake juu ya ghasia zilizototokea nchini humo kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais, na ametilia shaka iwapo serikali itakayoundwa baada ya uchagzui huo itakuwa wakilishi ya taifa nzima. 

Upande wa uchaguzi ulisusia kura hiyo iliyofanywa siku ya Jumanne. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Ijumaa hii Uamuzi wa Rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula wa tatu umetajwa kwenda kinyume na mkataba waliosaini mjini Arusha miaka kumi na tano iliyopita, ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.

Ghasia zimezuka nchini humo tangu rais Pierre Nkurunzinza kutangaza kuwania kiti hicho ambapo zaidi ya watu laki moja wamikimbia nchi hiyo huku makumi ya maelfu wengine wakiuawa katika maandamano. Juhudi kadhaa za kuleta upatanishi kati ya makundi hasimu zimeambulia patupu.

BUHARI "MAREKANI INAWASAIDIA BOKO HARAM"


Rais Mahammadu Buhari akiwa na mwenyeji wake Obama alipokua ziarani nchini Marekani wiki hii.

Marekani "inawasaidia na kuchochea " kundi la wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram kwa kukataa kutoa silaha kwa Nigeria, ni kauli ya rais wa Nigeria Mahammadu Buhari.

Sheria ya Marekani inazuia serikali kuuza silaha kwa nchi ambazo zinashindwa kushughulikia ipasavyo masuala ya haki za binadamu.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alikutana na rais Barack Obama Jumatatu kuomba msaada zaidi. Boko Haram limewauwa watu 10,000 tangu mwaka 2009 na limewateka mamia ya wasichana na wanawake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...