Friday, July 24, 2015

WAJUMBE WA CCM WAPATA AJALI, MMOJA AFARIKI


Mtu mmoja amefariki Dunia baada ya basi Dogo aina ya toyota HIACE, lililokuwa limewabeba wajumbe wa chama cha mapinduzi wa kata ya Milanzi kwenye manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, waliokuwa kwenye kampeni za kura za maoni za udiwani kuacha njia na kupinduka, ambapo pia ajali hiyo imeacha majeruhi kumi na moja.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga, mwenyekiti wa CCM wa kata ya milanzi Bw. Edgar Mwanandenje ambaye ni miongoni mwa majeruhi hao, amesema walikuwa wakitokea kwenye mchakato wa kampeni ya kura za maoni katika kata yao, ndipo dereva wa basi hilo dogo alipolazimisha kuipita kwa kasi pikipiki aina ya bajaj iliyokuwa mbele yao, na kupoteza mwelekeo kabla ya kupinduka. 

Katibu wa ccm wilaya ya sumbawanga mjini Bw Gabriel Kiula akiongelea juu ya ajali hiyo,amemtaja aliyepoteza maisha kuwa ni Didas Mwanisenga aliyekuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya kata ya milanzi, huku kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw. Jacob Mwaruanda akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...