Friday, January 10, 2014

CHADEMA HAPAKALIKI TIMUA TIMUA YAENDELEA... KATIBU WA WILAYA ASIMAMISHWA KAZI

  Kamati ya utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, imemsimamisha Katibu wake, Jordan Membe, kwa madai ya kwenda kinyume na katiba ya Chama.

Habari kutoka wilayani humo zilizothibitishwa na uongozi wa chama hicho, ngazi ya wilaya na ile ya mkoa, zinaeleza Membe amesimamishwa kutokana na
kukiuka maadili ya uongozi, ikiwa ni pamoja na kujihusisha na masuala ya kuleta na
kusababisha vurugu ndani ya chama.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho, kilichofanyika makao makuu ya ofisi ya chama hicho, wilayani Nachingwea, ambao hawakupenda majina yao kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwa madai sio wasemaji wa Chama, wameeleza kuwa Membe anadaiwa kusambaza waraka unaopinga kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu mkuu, Zitto Zuberi Kabwe na wenzake.


Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

IGP ATANGAZA MABADILIKO MAKUBWA JESHI LA POLISI


Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu ameanza kazi kwa kutangaza mabadiliko ya mfumo wa jeshi hilo huku akiunda vitengo vipya kwa lengo kuongeza ufanisi katika kukabiliana na uhalifu.
Katika mabadiliko hayo, IGP Mangu amesema polisi wameanzisha kamisheni mpya tano ambazo ni Intelijensia, Utawala, Fedha na Ugavi, Upelelezi, Uchunguzi wa Kisayansi wa Kesi za Jinai na Polisi Jamii.
Mfumo huo mpya wa polisi ndiyo uliowezesha kuundwa kwa nafasi mpya ya Naibu IGP, ambayo mteule wake wa kwanza ni Abdulrahman Kaniki ambaye kabla ya hapo alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Sayansi wa Makosa ya Jinai. Nafasi hiyo sasa inakaimiwa na watu waliokuwa chini yake.
Viongozi wengine katika safu hiyo ni Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Issaya Mngulu, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, Kamishna wa Fedha na Ugavi, Clodwig Mtweve, Kamishna wa Utawala, Thobiasi Andengenye na Kamishna wa Polisi Jamii, Mussa Ali Mussa. Naibu Kamishna wa Polisi, Diwani Athuman yeye anakaimu nafasi ya Kamisheni ya Intelijensia.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 10, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAJIBU YA UBALOZI WA TANZANIA CHINA JUU YA JACKIE CLIFF KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO MACAU/CHINA


J Cliff 1

Mwezi December 2013 taarifa zilitoka kwamba kuna binti wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 aliekamatwa na dawa za kulevya huko Macao China ambapo baadhi ya taarifa zilizoripotiwa na Waandishi wa Tanzania zilisema aliekamatwa ni mrembo ambae amekua akionekana kwenye video kadhaa za wasanii wa bongofleva (Jackie Cliff).
Macao

Macao.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

WAFANYABIASHARA WA DAR WAGOMEA MASHINE ZA TRA TENA ... WAAMUA KUFUNGA MADUKA YAO




Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...