Tuesday, June 11, 2013

Vodacom, MCL wazindua habari kwa simu

sms f6b99

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited, Tido Mhando (kushoto) akimwangalia Mkurugenzi wa Kampuni ya Vodacom, Rene Meza alipokuwa akijisajili katika huduma ya habari zilizotokea hivi punde (Breaking News) kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Dar es Salaam, jana. Picha na Silvan Kiwale

Kampuni ya Vodacom Tanzania na Mwananchi Communications Limited (MCL), zimezindua mradi wa kufikisha habari za punde (Breaking News) kwa jamii, kuanzia leo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza alisema kwa kuanzia, wanatarajia wateja wasiopungua milioni kumi kujiunga na huduma hiyo.

"Mtumiaji mtandao wa Vodacom ataunganishwa na huduma hii kwa kupeleka ujumbe wenye neno Habari kwenda namba 15569, kwa gharama ya Sh150 kwa siku, tunafurahia hatua hii kwani tuna hakika itatuimarisha sokoni," alisema Rene.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando alisema mradi huo umegharimu mwaka mmoja na nusu kuuandaa.

MHADHIRI WA CHUO KIKUU ATEMBEZWA UCHI BAADA YA KULIVAMIA KWA PUPA PENZI LA MWANAFUNZI...!!!

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Delta State huko nchini Nigeria alijikuta katika aibu kubwa baada ya kuvuliwa nguo na kubaki uchi wa mnyama baada ya mwanafunzi wa kike aliyekuwa akisumbuliwa na Mhadhiri huyo kuamua kumfanyia umafia kwa kumuwekea mtego.

Hatua ya kudharirishwa kwa Mhadhiri huyo ilikuja baada ya mwalimu huyo kumtishia Tega na kumwambia kuwa atamferisha kama hata kubali kufanyanae mapenzi.Kabla ya hapo Mhadhiri huyo aliwahi kumtongoza mwanafunzi huyo lakini mwanafunzi huyo alimkatalia kata kata baada ya kuona hivyo Mhadhiri huyo aliamua kutumia wadhifa alionao kwa kumtishia kuwa kama hato kubali kulala nae basi atamfelisha mtihani.

Baada ya kuona hivyo Tega aliamua kumkubalia Mhadhiri huyo na kumshawishi badala kwenda kwenye hoteli kuchukua chumba ni bora waende nyumbani alikopanga mwanafunzi huyo ili wapunguze gharama,kuona hivyo Mhadhiri huyo alikubali haraka na kwenda nyumbani kwa Tega bila kujua kuwa kuna mtego amewekewa kumbe kabla ya hapo Tega alikuwa amesha waambia majirani zake na wanafunzi wenzake kuwa atahakikisha anamrubuni Mhadhiri huyo mpaka akubali kuvua nguo akisha kubali tu anamuaga kuwa anakwenda chooni kisha anawapigia simu waje kumuumbua Mhadhiri huyo kwani milango yote alikuwa ameirudishia tu na alikuwa ameshawaelekeza chumba ambacho atakuwepo Mhadhiri huyo.

Basi baada ya kuwapigia majirani na wanafunzi wenzake walifika eneo hilo la tukio na kufungua milango kimya kimya na kufanikiwa kuingia ndani mpaka chumba alipo Mhadhiri huyo ndipo walipo fanikiwa kumkuta Mhadhiri huyo akiwa uchi wa mnyama kitandani na kisha kumtoa nnje na kumtembeza uraiani ili watu wajionee wenyewe nini baadhi ya wahadhiri hufanya kwa wanafunzi wa kike.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNE 11, 2013






Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...