Boti iliyojaza wahamiaji haramu kuelekea Yemen
Watu 70 wamekufa baada ya boti iliyokuwa imejaza wahamiaji haramu kupinduka baharini, magharibi mwa Yemen.
Maafisa nchini Yemen wamesema wengi ya watu waliokuwa katika boti hiyo ni raia wa Ethiopia.
Hali mbaya ya hewa inaelezwa kwamba ndio chanzo cha kuzama kwa boti hiyo.
Mamia
kwa maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa safari
zisizo na usalama katika nchi zilizo katika pembe ya Afrika na Yemen
kila mwaka.
Umoja wa Mataifa unamini kwamba kiasi cha watu watu mia mbili wamezama maji katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Na BBC