Wednesday, June 04, 2014

ANGALIA MSAFARA WA RAIS WA KENYA UNAVYOKUWA BAADA YA KUPEWA KITISHO CHA KUUAWA NA AL- SHABAAB

Screen Shot 2014-06-04 at 9.53.41 AM 
Imefaamika kuwa baada ya kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab cha Somalia kutoa onyo kwamba mashambulizi yake yanayofata yatawahusu viongozi wa Kenya, imebidi system ya ulinzi wa rais kwenye msafara ibadilike.
Mabadiliko yalianza kuonekana toka mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye sherehe za 51 za kujitawala ambapo badala ya Rais kutumia gari aina ya Land rover iliyo wazi iliyokua pia ikitumika na marais wa awali, rais aliiingia kwenye uwanja wa michezo wa Nyayo na gari aina ya Land cruiser iliyo na vioo visivyo penya risasi.
Screen Shot 2014-06-04 at 9.53.52 AM 
Hiyo Land Cruiser ililoongozwa na gari lenye mitambo iliyo na uwezo wa kugundua bomu kwa zaidi ya kilomita 10, nyuma kabisa kulikua na gari lililo na uwezo wa kuhimili risasi na bomu au kilipuzi cha aina yoyote na inasemekana kwamba gari hilo huwa linatumika endapo msafara wa Rais umeshambuliwa kwa haraka Rais na wakuu wengine wanaondolewa na gari hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 04, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAMU WAFANYA MAUAJI


borno iliyoshambuliwa NIgeria
BBC imepata taarifa kuwa zaidi ya watu 20 wameuawa katika mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.
Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo yapata siku 50 zilizopita.
Wakaazi wa kijiji cha Attagara karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema kuwa watu waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza watu waje katika uwanja wa kanisa.
Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mbunge wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia BBC tukio hilo na kusema kuwa watu wengi wameuawa na nyumba kuchomwa katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.
'Jeshi lakanusha madai'
Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha madai katika vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imewapata na hatia baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi. Jeshi limesema kuwa taarifa hizo ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete.

nyumba zimechomwa Borno
Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wa maeneo mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio yaliyochacha. Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.
Suala la wasichana waliotekwa pia bado limekaa kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria ambapo shinikizo kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa haraka. Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kutokana na tisho la usalama lakini ssa polisi wametangaza kuwa maandamano ya amani yanaweza kufanywa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...