Thursday, May 30, 2013

Wema Afunguka na Kusema: "Sikuwahi kumsaliti Diamond na tulikuwa tunapendana sana"

 
Miss Tanzania mwaka 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amefunguka kupitia jarida jipya la Mzuka kuwa katika uhusiano wake wote na Diamond hakuwahi kumsaliti.

Wema ambaye yupo kwenye cover la jarida hilo linalotolewa na  Bongo5,amefunguka kwa kusema kuwa yeye na Diamond walikuwa wakipendana sana.


“Maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo,” amefunguka Wema.

Wema amefunguka pia kuhusu jinsi Diamond alivyomcheat na Jokate kwa kusema, “nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza.”

Katika jarida hilo ambalo linauzwa kwa shilingi 1,500 tu, Wema amesimulia mengi tangia alipokutana na Diamond, jinsi alivyoumizwa na kitendo chake cha kumrekodi na kusambaza sauti kwenye radio, mapenzi yake na Kanumba, utajiri wake, jinsi anavyowapenda mbwa wake na mambo mengine exclusive.

HII NDIO RIPOTI YA KUTEKWA, KUUMIZWA KIBANDA



TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA IMEWASILISHWA NYUMBANI HOTEL - TANGA MEI 30, 2013


UTANGULIZI: 

Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013, Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi Juu, Dar es Salaam.Tukio hilo liliishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa ujumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lilomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madkatari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka lililotokea karibu miezi tisa kabla ya tukio la Kibanda yaani, usiku wa Juni 26, 2012.Ukiacha matukio hayo, miezi sita kabla ya Kibanda kutekwa na kuteswa Mwandishi Daudi Mwangosi, aliuawa akiwa mikononi mwa vyombo vya dola Septemba 2, 2012 huko Nyololo, Iringa akiwa kazini.Tukio la Kibanda limekuwa na sura ya mwendelezo wa mauaji au utesaji wa wanahabari, hasa ikitiliwa maanani kuwa Mwandishi Issa Ngumba (45) wa Radio Kwizera aliyekuwa anafanyia kazi zake katika Wilaya ya Kakonko, Kigoma, Januari mwaka huu, alipigwa risasi na kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.Kama hiyo haitoshi, tukio la kutekwa na kudhuriwa kwa Kibanda limetokea mwezi mmoja tu baada ya Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Shaaban Matutu kupigwa risasi na polisi akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam kwa maelezo kuwa kimakosa polisi walidhani Matutu ni jambazi.

BREAKING NEWZZZZZZZ....!!! MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA







HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB) ILIYOSABABISHA BUNGE KUHAIRISHWA LEO

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika bajeti ya wizara hii mwaka 2012/13, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA ilibaini mapungufu mengi ya kiutendaji na kiuwajibikaji katika wizara hii, na hivyo kuitaka Serikali kufanya mambo yafuatayo ili kuboresha utendaji na ufanisi:

1. Kuziwezesha balozi zetu nje kwa kuzitengea fedha za kutosha ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi
2. Kutoa idadi ya majengo ya balozi zetu nje (nyumba za mabalozi, nyumba za maafisa wa balozi na ofisi za balozi) kwa mchanganuo wa idadi ya nyumba katika nchi na kama nyumba hizo zina hati miliki au la.
3. Kutoa taarifa ya namna kila ubalozi ulivyotekeleza sera ya Diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia kwamba balozi nyingi ziko hoi kifedha kiasi cha kwamba waambata wa kiuchumi wanakosa fedha za kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa ajili ya upelelezi wa masuala ya kiuchumi.
4. Kulikarabati jengo la ubalozi wa Tanzania huko Msumbiji lililokuwa limechakaa kwa kutofanyiwa ukarabati tangu 1975 ingawa jengo hilo tulipewa bure na Serikali ya Msumbiji chini ya FRELIMO.

PICHA ZA MWAKILISHI WETU KATIKA BBA ALIVYOJIACHIA BAFUNI NA DILISH.

Dillish na Nando wakioga
Jana (May 29) ilikuwa ni usiku wa tatu katika jumba la big brother Afrika huko Afrika Kusini mengi yanazidi kuonekana na sasa washiriki wengi wanaanza kuonesha side B ya mioyo yao na kujaribu kupata muda wa kuwa romantic na kuonesha upendo (Romantic time). 
 Wakati washiriki wengine wakiendelea na mambo yao mtanzania Ammy Nando alijiachia kwenye bafu moja na na kuoga na mrembo Dillish kutoka na Namibia ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu akisomea Saikolojia.
Huenda huu ukawa mwanzo wa mahusiano yao humo ndani kwa sababu moyo hauna pazia na uruzi wa Dillish unaweza kumvuta to the limit model huyo wa kitanzania.
Dillish
Kwa upande mwingine the boss lady toka Kenya Huddah Monroe alipata nafasi ya kushare na  Denzel mawili matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel akiwa ameonesha tangu mwanzo kudata kwa Huddah. Jana Huddah alifunguka na kumwambia kuwa anahitaji mwanamme mwenye pesa na kwamba she is a gold digger. Lakini second kadhaa baadae akafuta kauli yake na kumwambia kuwa alikuwa anatania. Really?!

Wiki hii Benzel, Betty, Huddah, Selly na Natasha wako katika nafasi kukumbwa na Eviction.

MSANII K-LYN AFUNGUKA KUHUSU BABA WA WATOTO WAKE MAPACHA NI BOSS WA MEDIA KUBWA BONGO

Am just a messenger!

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAZIDI KUZUA UTATA

Matokeo ya kidato cha nne yanayotarajiwa kutangazwa leo, yamezidi kuzua mapya baada ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kulazimika kutumia kanuni iliyofanya ufaulu upande kwa asilimia tisa kutoka 34 wa awali, lengo likiwa ni kuepusha watahiniwa waliokuwa wamefaulu mwanzo kufeli.

Kanuni iliyokuwa imetumika mwanzo, ilifanya matokeo hayo yapande kwa asilimia kati ya 20 na 23, kiwango ambacho Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwaeleza wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wiki iliyopita maofisa wa wizara na taasisi zake wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa, walijadili matokeo hayo.


                       Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa.
“Wakati yakijadili, ufaulu bado ulikuwa kulekule kwenye zaidi ya asilimia 54, kutokana na kanuni hiyo wanafunzi kama 2,500 waliokuwa wamefaulu kwa madaraja ya juu walikuwa washuke,” kilisema.

Kutokana na hali hiyo, kwa sasa ufaulu ni asilimia 43 jambo linalofanya matokeo hayo yawe chini ikilinganishwa na mwaka 2011.
Chanzo chetu kilieleza kuwa, katika kikao hicho, kulikuwa na mvutano kuhusu kanuni ipi itumike ili kuwaokoa wanafunzi hao alama zao zisishuke.
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Necta ilienda tena kuyafanyia kazi matokeo hayo ambapo sasa ufaulu umeshuka kwa asilimia zaidi ya 20 hadi kufikia  asilimia tisa.

“Kwa sasa hakuna mtu ambaye matokeo yake yameshuka, ila bwana kazi ipo siyo kama ambavyo watu wanaona kuna vurugu kweli,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Ukijaribu kuangalia, Necta wanasimamia kanuni, lakini wakati mwingine inabidi mtu uangalie hali ilivyo, kwa sasa watu wanaangalia zaidi mwitikio wa wananchi utakavyokuwa haya matokeo yakitangazwa badala ya kuangalia vitu vya msingi,” kilisema chanzo hicho.

Producer Mswaki Aimba kama Ngwear Kumuenzi-Sikiliza Wimbo Huo Hapa...!!

Huu Wimbo Ameimba Producer wa mziki anayejulikana kwa jina la Mswaki Kutoka Studio ya Black Curtains....Ameimba kama Marehemu Ngwear Akiimba baada ya Kifo chake...Sikiliza Hapa chini: Big up Sana Mswaki 

>>>>>  Click Hapa

ANGALIA WALICHOCHAT WEMA SEPETU NA NGWAIR SIKU CHACHE KABLA YA KIFO, NI KUUSU KAJALA KUONEKANA KATIKA VIDEO MPYA YA MAREHEMU NGWAIR

 
Katika upekuzi wetu leo hii tuliweza kupata moja ya chat za mwisho mwisho ya marehemu Albert Mangwea akiwa afrika ya kusini na mwanadada wa bongo movies Wema sepetu. Katika maongezi hayo Ngwea alikuwa anapanga Kumtumia mwadadada mwingine wa bongo movies Kajala Masanja kwenye video yake mpya aliyokuwa anajiandaa kuifanya. Maongezi yao yalikuwa hivi.

Mangwea : kuku bandani..
Mangwea : Nataka Kajala…
Mangwea : Sikiza nyimbo then utanipa idea..
Mangwea : Nataka tukipiga hela kwa bro…
Mangwea : Tulipe na hela ya ticket ya Jux aje toka China tumalize huku kusini
Mangwea : #hugs
Wema Sepetu : Upo api?
Mangwea: Me nipo Pretoria now momo…
(Angalia screen shot ya maongezi hayo pichani)
Dah, inasikitisha sana. Maisha ya Msanii huyu yaliyokatika mapema. Mungu ailaze roho marehemu mahali pema peponi.

TCRA.... "SIMU ZISIZOSAJILIWA MWISHO KESHO"

TCRA: Simu Zisizosajiliwa Mwisho KeshokutwaMamlaka ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa simu ambazo hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni Mosi mwaka huu.
Tamko hilo lilitolewa jijiji Mbeya na Mkurugenzi wa Sheria na Leseni wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nziga wakati wa semina kuhusu utekelezaji wa sheria mpya ya mawasiliano ya elektroniki na posta ya mwaka 2010 kwa wadau mbalimbali.
Hiyo ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA, kwani awali ilikuwa na kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima na kuwataka wananchi kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 31, mwaka jana.
Mikoa mingine iliyoingia kwenye mfumo wa dijitali ni Arusha, Tanga, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Nziga alisema mamlaka hiyo inasisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano kati yake na watoa huduma za mawasilino ya simu na kufikia usiku wa Juni Mosi, namba za simu ambazo hazikusajiliwa zitakoma. Mmiliki wake hataweza kuitumia kupiga wala kupokea siku.
Alisema kuwa ni muda mrefu umepita ambao ulitolewa kwa ajili ya kusajili namba za simu lakini watu wengi hawakuweza kufanya hivyo kwa wakati na badala yake wamekuwa wakitumia simu vibaya ikiwa ni pamoja na kufanya uhalifu na kutoa lugha chafu.
Katika hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Abbas Kandoro, ilisema vyombo vya mawasiliano vimesaidia kukua kwa sekta mbalimbali

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 30, 2013


3 a8154


1 847ab

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...