Sunday, February 24, 2013

ADEN RAGE MWENYEKITI WA SIMBA KESHO KUACHAIA NGAZI?


Mwenyekiti wa Simba ismail Aden Rage
HABARI zilizotufikia hivi punde kutoka ndani ya klabu ya soka ya Simba zinasema kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage anatarajiwa kujiuzulu nafasi yake kutokana na kipigo ilichopewa timu yake jioni ya leo na Mtibwa Sugar. 
Taarifa hizo zimedokeza kuwa, Rage atatangaza msimamo huo wa kuachia ngazi Msimbazi kesho atakapokutana na waandishi wa habari.
MICHARAZO imekuwa ikimsaka Rage mwenyewe kusikia kauli yake, lakini simu yake imekuwa haipatikani, hivyo juhudi zinaendelea ili kuthibitisha taarifa hizo na tutawajuvya mara tukibahatika kumpata.

MUIGIZAJI STEVE NYERERE ATUPWA LUPANGO



 
 Eneo la tukio la ajali hiyo.
 Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
 Kushoto ni gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.
 Huu ndiyo waya wa umeme uliosababisha ajali hiyo.
 Askari wa usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
 Askari akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka kituoni Mabatini.
 Gari la Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.
 Gari husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi ya warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
**********
Movie mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.
Msanii huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini, wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.

Wasanii hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.

Ajali hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.

Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni. 

Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.

Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.

Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini. 
 
credits: Sufiani Mafoto

WAANDISHI WA HABARI WANUSURIKA KUTEKWA WAKITOKA KUHOJI MASWALA YA GESI MTWARA

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, walioshiriki Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mjini Mtwara, wakilindwa na Askari wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), eneo la Chuo cha VETA, mjini Lindi jana asubuhi walipopelekwa na  mabasi madogo maarufu kwa jina 'Coaster' kutoka Mtwara Mjini, walikokimbia vitisho vya baadhi ya wakazi wa mji huo, waliopanga kuwavamia wakiwa kwenye mabasi makubwa mawili yaliyopangwa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam jana, wakiwahisi kuwa wanahabari hao walikuwepo mkoani humo kupeleleza suala la Gesi.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA  Na Richard Mwaikenda, Mtwara

WAANDISHI wa Habari 150  kutoka vyombo mbalimbali wamenusurika kuvamiwa na wananchi wakiwahisi kwamba walikwenda mjini Mtwara kupepepeleza suala la Gesi.

Wanahabari hao waliokuwepo Mtwara katika Kongamano la siku mbili la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lilibidi wabadili muda wa kuondoka jana badala ya saa mbili asubuhi waliondoka alfajiri saa 11.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kuwepo fununu kwamba wananchi hao walipanga kuwavamia na kuwadhuru waandishi wa habari wakiwa kwenye mabasi mawili ya Kampuni ya amanju yaliyotakiwa kuondoka Mtwara saa mbili asubuhi kwenda nao Dar es Salaam.

Fununu hizo ziliwapata wanahabari wakiwa kwenye hafla ya chakula cha usiku waliyoandaliwa na NHIF, kwenye Hoteli ya Makonde Beach juzi usiku, ambapo hata Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alihudhuria, lakini hakufika mwisho baada ya kusikia taarifa hizo.

Hongera rais Kagame : Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mke wake Bi Jeannette Kagame wakishirikiana na wananchi wa Kanyinya wilaya ya Nyarugenge kuchimba mitaro ya maji jana( Feb 23,2013).



Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mke wake Bi Jeannette Kagame wakishirikiana na wananchi wa Kanyinya wilaya ya Nyarugenge kuchimba mitaro ya maji  jana( Feb 23,2013): Hongera rais Kagame.

MDEE AONGELEA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE


 Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia”  inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo”

SIMBA YAPIGWA KIMOJA NA MTIBWA SUGAR


 Timu ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo jioni katika Uwanja wa Taifa.

Bao la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja.

Bao hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezu mtafaruku mkubwa baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba, walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharula.

Aidha mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha maji ya kuwasha, huku vingozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika uwanjani hapo. 

Hata hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha pili.
 Beki wa Simba, ambaye leo amechezeshwa kama kiungo wa chini, Shaban Kapombe, akimchezea vibaya Rashid Gumbo.
 Beki wa Simba Keita, akimdhibiti mchezaji wa Mtibwa.
Mshambuliaji wa Mtibwa, akiwasakata mabeki wa Simba.
 
credits: Sufiani Mafoto

Rais Kikwete ashiriki Utiaji Saini Mpango Wa Umoja Wa Mataifa Wa Amani, Usalama na Ushirikiano Katika DRC.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki-moon akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt.  Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma akisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
Rais Joseph Kabila wa DRC na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakibadilishana mawazo kwa furaha huku Rais wa Jamhuri ya Kongo (Brazaville) Mhe Denis Sassou Nguesso akiwa kati yao baada ya wote kweka saini  katika Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim na wajumbe wengine wa ujumbe wa Tanzania wakati wa uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon katika picha ya pamoja na viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu baada ya uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kwa kuwa mmoja wa viongozi wa bara la Afrika walio mstari wa mbele kusimamia amani baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt  Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma.(PICHA NA IKULU).

Naibu Waziri wa Fedha akagua Vitega uchumi vya PSPF Jijini Dar.


SIKU MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake.
Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Pichani ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia mchoro wa Jengo la Kitega Uchumi cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) ambalo linajengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam na litakuwa na Ghorofa 35. Ndani ya jingo hilo la kutakuwa na Ofisi, maduka na nyumba za kulala.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani katika moja ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF Tower ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika zitauzwa  kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment) zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akitembezwa  ndani ya jengo hilo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu.
 Watumishi wa PSPF wakizungumza  jambo ndani ya Jengo hilo.
Awali Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba 491 za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) zinazojengwa Buyuni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na ambazo zimekamilika ujenzi wake na kuanza kuuzwa kwa Wanachama wa mfukjo huo. Pichani mbele kutoka kushoto ni Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.

Nyumba hizo zikiwa zimekamilika ujenzi wake na kusubiri wateja tu.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene nje ya moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF, kwaajili ya kuwauzia wanachama wake kwa gharama nafuu.

Dkt. Mwakyembe azindua Bodi ya Wakurugenzi ya TRL jijini Dar.

 Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe(katikati) akizundua rasmi Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) . Dkt. Mwakyembe amezindua Bodi hiyo leo jijini Dar es salaam ambapo ameitaka kuhakikisha inasaidia kuimarisha reli ili mizigo mingi inayokwenda ndani na nje ya nchi isafirishwe kwa njia ya reli ili kuokoa barabara. (Picha na MAELEZO-Dar)

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...