Sunday, February 24, 2013

SIMBA YAPIGWA KIMOJA NA MTIBWA SUGAR


 Timu ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo jioni katika Uwanja wa Taifa.

Bao la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja.

Bao hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezu mtafaruku mkubwa baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba, walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharula.

Aidha mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha maji ya kuwasha, huku vingozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika uwanjani hapo. 

Hata hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha pili.
 Beki wa Simba, ambaye leo amechezeshwa kama kiungo wa chini, Shaban Kapombe, akimchezea vibaya Rashid Gumbo.
 Beki wa Simba Keita, akimdhibiti mchezaji wa Mtibwa.
Mshambuliaji wa Mtibwa, akiwasakata mabeki wa Simba.
 
credits: Sufiani Mafoto

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...