Sunday, February 24, 2013

WAANDISHI WA HABARI WANUSURIKA KUTEKWA WAKITOKA KUHOJI MASWALA YA GESI MTWARA

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, walioshiriki Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mjini Mtwara, wakilindwa na Askari wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), eneo la Chuo cha VETA, mjini Lindi jana asubuhi walipopelekwa na  mabasi madogo maarufu kwa jina 'Coaster' kutoka Mtwara Mjini, walikokimbia vitisho vya baadhi ya wakazi wa mji huo, waliopanga kuwavamia wakiwa kwenye mabasi makubwa mawili yaliyopangwa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam jana, wakiwahisi kuwa wanahabari hao walikuwepo mkoani humo kupeleleza suala la Gesi.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA  Na Richard Mwaikenda, Mtwara

WAANDISHI wa Habari 150  kutoka vyombo mbalimbali wamenusurika kuvamiwa na wananchi wakiwahisi kwamba walikwenda mjini Mtwara kupepepeleza suala la Gesi.

Wanahabari hao waliokuwepo Mtwara katika Kongamano la siku mbili la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lilibidi wabadili muda wa kuondoka jana badala ya saa mbili asubuhi waliondoka alfajiri saa 11.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kuwepo fununu kwamba wananchi hao walipanga kuwavamia na kuwadhuru waandishi wa habari wakiwa kwenye mabasi mawili ya Kampuni ya amanju yaliyotakiwa kuondoka Mtwara saa mbili asubuhi kwenda nao Dar es Salaam.

Fununu hizo ziliwapata wanahabari wakiwa kwenye hafla ya chakula cha usiku waliyoandaliwa na NHIF, kwenye Hoteli ya Makonde Beach juzi usiku, ambapo hata Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alihudhuria, lakini hakufika mwisho baada ya kusikia taarifa hizo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...