Wednesday, January 14, 2015

'HATUFUKUZI MGOMBEA URAIS CCM'

 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM , mjini Unguja , Zanzibar jana.  Kushoto ni Makamu wake (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein .

Wakati Kamati Kuu ya chama tawala, CCM ikimaliza vikao vyake mjini hapa, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana amesema mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu baadhi ya wanachama wanaotajwa kuwania urais hayana ukweli, wala hakuna atakayefukuzwa uanachama.
Kinana aliyasema hayo jana mjini hapa kuhusu mambo yaliyojitokeza kwa wagombea wa nafasi za urais kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu, Oktoba.
Kamati Kuu ya CCM hadi jana jioni ilikuwa ikiendelea na kikao chake kwenye ofisi kuu ya chama, Kisiwandui, Zanzibar.
Kauli ya Kinana imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono kuwa baadhi ya makada waliojitokeza kutangaza ama kuonyesha nia kuutaka urais watachukuliwa hatua, zikiwamo kutimuliwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

NGELEJA, CHENGE WAPELEKWA KWENYE KAMATI YA MAADILI

 
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa (LAAC) za Mitaa, Kangi Lugola akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mjumbe mwenzake, Omari Nundu.

Licha ya Bunge kuazimia kuwa wenyeviti wa kamati zake waliotajwa kuhusika kwenye kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow wavuliwe nyadhifa zao, hali imekuwa tofauti katika vikao vya kamati hizo vilivyoanza jana baada ya baadhi yao kuongoza vikao hivyo. Jana, Kamati Kuu ya CCM imeamua viongozi hao, Andrew Chenge, William Ngeleja Na Profesa Anna Tibaijuka wafikishwe Kamati ya Maadili ya chama.
Awali, walitakiwa kuachia ngazi na kamati zao katika mabano ni Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala), Chenge (Bajeti) na Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini).
Kikao cha 16 na 17 cha Bunge kiliazimia kuwa kamati husika za kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge unaoanza Januari 27, kuwavua nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa kamati husika.
Hata hivyo, jana, Ngeleja alisema anaendelea na madaraka yake, kwa kuwa hatua iliyopo sasa ni ya uchunguzi.  Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JANUARI 14, 2015


.


.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

GAZETI LENYE KIBONZO CHA MTUME LAUZWA TENA...!!!

Gazeti la Charlie Hebdo leo limeanza kusambaza toleo la gazeti lake ambalo limechapishwa kibonzo cha Mtume Mohammad kwenye ukurasa wake wa mbele.
Nakala Milioni za gazeti hilo zimeanza kusambazwa na nyingine zitafuata iwapo wanunuzi wataongezeka.
Picha ya kibonzo hicho iliyopo ukurasa mbele wa gazeti hilo inamwonyesha Mtume Mohammad akilia.
Wandishi wa jarida la Charlie Hebdo wamechapisha tena picha ya kibonzo cha mtume Muhammad
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa picha hiyo itachochea chuki.
Hata hivyo waandishi wa habari wa gazeti hilo wanasema ukurasa wa mbele unamaanisha Waandishi wa habari wamewasamehe waliotekeleza shambulizi la kigaidi lilolofanyika jumatano wiki iliyopita.
Naibu Mhariri wa Gazeti la Liberalation Alexandra Schwatzbrod anasema ulikuwa uamuzi mwepesi kwa gazeti lake kuchapisha picha ya kibonzo hicho. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ONGWEN AKABIDHIWA KWA WANAJESHI WA UGANDA

Kamanda Ongwen sasa yuko mikononi mwa wanajeshi wa Uganda 
 
Kamanda mkuu wa kundi la waasi la LRA nchini Uganda, aliyejisalimisha wiki jana, Dominic Ongwen , amekabidhiwa kwa wanajeshi wa Uganda walio katika Jamuhuri ya Afrika ya kati.
Muasi huyo, Dominic Ongwen, anasemekana kuwa naibu kiongozi wa kundi hilo Joseph Kony na alikamatwa na wanajeshi wa Marekani wiki jana ingawa waasi wa Seleka wanasema wao ndio waliomkamata.
Waasi hao walisema kwamba walimkatama Ongwen baada ya makabiliano ya muda ingawa jeshi la Marekani lilisitiza kuwa alijisalimisha na tangu hao wamekuwa wakimzuilia.
Uganda imesema kwamba itamkabidhi kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, ambako anatakikana kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Kundi la LRA liliwateka nyara wasichana na wavulana huku wavulana wakilazimishwa kuwa wapiganaji na wasichana wakifanywa watumwa wa ngono.
Ongwen pamoja na Joseph Kony wanatakikana na mahakama ya ICC kujibu tuhuma za kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Je Ongwen ni nani?
-Inaarifiwa alitekwa nyara na waasi wa LRA akiwa na umri wa miaka 10 wakati alipokuwa anaelekea shuleni Kaskazini mwa Uganda.
-Miaka iliyofuata, alipanda ngazi na kuwa kamanda
-Anatuhumiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo, kuwatumia watoto kama watumwa.
-ICC ilitoa kibali cha kumkamata mnamo mwaka 2005.
-Kuliwa na madai kwamba aliuawa katika mwaka 2013 ambapo Marekani ilitangaza ahadi ya zawadi kwa yeyeote mwenye taarifa kumhusu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

AVULIWA NGUO KUTHIBITISHA JINSIA YAKE

Genoveva Anonma
 
Genoveva Anonma alidhalilishwa,kwa takriban miaka minne,amekuwa akihisiwa kuwa si mwanamke naye amekuwa akizidharau tuhuma hizo mara kwa mara.
Lakini kuna kitu ambacho hakukitegemea kilichokuwa kinamuandama kufuatia uwezo wake michezoni alipokuwa Equatorial Guinea mwaka 2008 katika michuano ya soka la wanawake wa mataifa ya Afrika.
Goli lake la ushindi katika ardhi ya nyumbani,na timu yake kuwa ya kwanza wakiifuatia Nigeria ,ambayo iliibuka kuwa washindi wa jumla,Anonma badala ya kuhesabika kuwa mkombozi na mwenye kuitimiza ndoto yake michezoni, badala yake amebaki njia panda.
Anonma awapo uwanjani huwa ana haha uwanjani huku na kule na nguvu alo nayo,timu pinzani humbeza kuwa hawezi kuwa mwanamke bali wanacheza na janadume,na ndipo sasa kituko kikaja kutokana na tuhuma hizo shirikisho la soka barani Africa walichagua njia ya kuhakiki jinsia ya Anonma. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KOCHA NOOIJ KUTAJA STARS MABORESHO

IMG_0316
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij anatarajia kutaja kikosi cha Maboresho kitakachoingia kambini Januari 18 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu jijini Mwanza.

Nooij atataja kikosi hicho kwenye mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Januari 15 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TANZANIA KUIKABILI KENYA BEACH SOCCER

Soka la ufukweni 
 
Timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni (beach soccer) imepangiwa kucheza na Kenya katika raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa ajili ya fainali za Afrika ambapo michuano hiyo itafanyika Aprili mwaka huu nchini Shelisheli.
Mwenyekiti wa Kamati ya Beach Soccer, Ahmed Idd Mgoyi amesema jijini Dar es Salaam, kuwa Tanzania itaanzia ugenini ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwaka huu nchini Kenya.
Mechi ya marudiano itafanyikaa Tanzania kati ya Februari 20 na 22 mwaka huu. Iwapo timu ya Tanzania itasonga mbele, katika raundi ya pili itacheza na Misri ikianzia nyumbani kati ya Machi 13 na 15 mwaka huu.
Mgoyi alisema maandalizi ya Tanzania kushiriki kwenye mashindano hayo yameanza ambapo timu ya Tanzania Bara itacheza na Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kupata kikosi kimoja kitakachoingia kwenye michuano hiyo ya Afrika.
Benchi za ufundi la timu ya Tanzania litaongozwa na John Mwansasu wakati Msaidizi wake ni Ali Shariff 'Adolf' kutoka Zanzibar, na Meneja wa timu hiyo ni George Lucas. Wote hao walishiriki kwenye kozi ya ukocha wa beach soccer iliyoendeshwa mwaka jana nchini na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kocha Mwansasu atatangaza timu ya Tanzania Bara, Januari 19 mwaka huu, na mazoezi ya pamoja na timu ya Zanzibar yatafanyika Januari 24 na 25 mwaka huu.
Wachezaji wa timu ya Tanzania Bara watatokana na michuano ya beach soccer iliyofanyika mwaka jana ikishirikisha timu za vyuo vya elimu ya juu vya Mkoa wa Dar es Salaam. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...