Thursday, April 11, 2013

JOHARI AGOMA KUTINGISHA MAUNO YAKE MBELE YA RAY


MKONGWE kwenye ‘Industry’ ya Filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alitoa kali ya aina yake baada ya kukataa kuzungusha nyonga mbele ya mwigizaji mwenzake, Vincent Kigos ‘Ray’ anayedaiwa ni mpenzi wake

Tukio hilo lililonaswa na mwandishi wetu juzikati, lilitokea katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wakati wasanii hao walipojumuika pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kitokee kifo cha msanii mwenzao, Steven Kanumba.

Akiwa viwanjani hapo, Johari aliitwa kupanda jukwaani na wasanii wenzake kwa ajili ya kucheza sebene kidogo lakini yeye alikataa na mwandishi wetu alimsikia akijitetea kuwa hawezi kukata nyonga mbele ya wasanii wenzake hususan Ray ambaye ni bosi mwenzake kwenye kampuni yao ya RJ Company.

“Siwezi kujidhalilisha mbele ya umati huo kwa kukata kiuno tena na bosi mwenzangu yupo pale, labda ningekuwa nimelewa kiasi cha kutojitambua hapo ningefanya madudu kama hayo,” alisema Johari.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, MULUGO ATANGAZA VITA NA WAZUSHI WAKE

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya sekondari. Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea kumdhalilisha.

Mulugo alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.

“Wanasema eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu waliorudia darasa.

“Kama kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.

Kwa miezi kadhaa sasa Mulugo amekuwa akidaiwa kughushi vyeti na kutumia jina la mtu ili kufikia kiwango cha elimu alichonacho madai ambayo alisema yanamchafulia jina katika jamii.

Kuhusu suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, Mulugo alisema matokeo hayo mabaya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wanafunzi.

Naye Ruth Mnkeni kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Mlugo amezindua tovuti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ijulikanayo kama Shule Direct.

Muluigo alisema kuzinduliwa kwa tovuti hiyo kutawafanya wanafunzi kupata maarifa mengi ya vitabu mbalimbali na kuinua kiwango cha elimu nchini

HALI TETE KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC

Ndani ya Taasisi ya Utangazaji Tanzania(TBC) kwa sasa kuna mgogoro mkubwa sana unafukuta chini kwa chini ukihusisha pande mbili kuu, yaani Wafanyakazi wa kawaida na Uongozi wa juu wa shirika hilo, kuhusu madai yafuatao na huku wakitaka Mkurugenzi mkuu wa sasa wa TBC afukuzwe na bodi ya shirika hilo ivunjwe;

1/Ubaguzi katika kupewa vyeo, Posho na marupurupu(Suala la Itikadi, Ukanda na Udini linatajwa sana)

2/Kuruhusu wanasiasa(Viongozi wa serikali na makada wa CCM) kuingilia wanavyotaka kazi za kitaaluma katika utoaji wa habari hususani kuhariri(Kuchuja) habari.

3/Kutokulipwa malimbikizo ya madeni ya madai ya siku za nyuma.

4/Utendaji Duni na Mbovu wa Mkurugenzi mkuu Clement Mshana hadi kufikia kumpa jina la dhihaka la 'BOYA'

5/Vitisho vya kufukuzwa kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohoji sana mwenendo mbovu wa shirika hilo kwa sasa.

6/Mvutano wa Chini kwa chini kati ya Wakurugenzi waliowekwa na Lowassa wakati akiwa waziri mkuu na wapya walioletwa na Pinda.

*Pia kuna issue ya mkataba tata(White Elephant) kati ya TBC na Startimes(Wachina!) ambao Terms, Conditions, Investment, Dividend na Shares havijawekwa wazi na sawasawa, japokuwa Mkurugenzi mkuu na Bodi yake ya sasa wanadai wameurithi tu lakini sio 'wapishi' kamili wa hicho kilichopikwa!!

source: JF

KAULI YA ZITTO KUTOKA BUNGENI ASUBUHI HII

CAG ameweka mezani taarifa yake asubuhi hii. Katika mkutano wa Kumi wa Bunge, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Ukaguzi ya mwaka 2008 Kwa kubadilisha vifungu 38, 39 na 40 ambapo Serikali ingeleta majibu yake sambamba na Taarifa ya CAG. Serikali haikuleta majibu hayo. Wamevunja Sheria wakiisha nikiwa siku ya kwanza ya kuanza kutekelezwa kwake. Spika alipowataka Serikali kutoa majibu, Mawaziri walibaki kutazamana tu

HATARI : WALA MAHINDI HATARINI KUDUMAA AKILI

WATAALAMU wa masuala ya afya na kilimo kutoka mataifa mbalimbali duniani, wamebaini mahindi, karanga na mihogo yenye sumukuvu ni moja ya vitu vinavyochangia saratani ya ini, udumavu wa mwili na akili kwa watoto.
Ingawa takwimu sahihi hazijapatikana kuonesha madhara ya kila 
nchi kutokana na utafiti hizo kuendelea, tatizo limeelezwa kuwa ni kubwa hasa katika nchi za Afrika kutokana na mfumo mzima wa uzalishaji katika sekta ya kilimo na ukuzaji wa mazao usiozingatia utaalamu.

Kutokana na ukubwa wa tatizo, wataalamu hao kutoka nchi 20, wanakutana jijini Dar es Salaam kwa siku tatu, kuanzia jana, kutafuta njia madhubuti za kukabiliana na sumukuvu. Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zilizochukua hatua za awali dhidi ya tatizo hilo.
Akizungumza jana katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema,
“Lengo la mkutano huu ni kuwapa fursa wataalamu kuja na mikakati itakayoisaidia serikali na sekta binafsi kupambana na sumu ya aflatoxin kwa kuwa hata hapa Tanzania ni tatizo kubwa.”
Dk Mwinyi alifafanua kuwa, tatizo kubwa linaonekana kwenye mazao yanayoathiriwa zaidi na sumukuvu ambayo ni mahindi, mihogo na karanga na husababisha watumiaji kupata saratani ya ini na watoto hudumaa akili na mwili.
Alisema pamoja na serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na sheria ya kudhibiti vyakula vinavyoingia nchini, lakini sheria pekee haziwezi kumaliza tatizo hasa ikizingatiwa kuwa Watanzania wengi wanatumia nafaka hizo wakati zikiendelea kukua shambani bila kuzipima kiwango cha sumukuvu kinachotakiwa.
Sumukuvu ni aina ya sumu inayosababishwa na kuvu katika mazao na ingawa haiepukiki katika nafaka, kuna kiwango kinachopaswa kuwepo na kinapozidi, huleta madhara hayo.

PETER WA P-SQUARE APATA MTOTO WA KIUME

DUNIANI KUNA MAMBO, HAWA WANASHEREHEKEA KIFO CHA MARGARET THATHER..........!!!




JK Atia Saini Kitabu cha Maombolezo ya Bi. Margaret Thatcher




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jana, Jumatano, Aprili 10, 2013 ametia saini Kitabu cha Maombolezo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Margaret Thatcher ambaye alifariki dunia Jumatatu wiki hii kwa ugonjwa wa kiharusi akiwa na umri wa miaka 87.

Rais Kikwete ametia saini Kitabu hicho kwenye Ubalozi wa Uingereza katika Tanzania ulioko Jengo la Umoja mjini Dar es Salaam.

Rais alikaribishwa kwenye Ubalozi huo na Balozi wa Uingereza katika Tanzania, Mheshimiwa Bi. Dianna Melrose na wafanyakazi wengine wa ubalozi huo na amekwenda moja kwa moja kutia saini kitabu hicho mara baada ya kuwasili kwenye Ubalozi huo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRIL 11, 2013

DSC 0038 d286d

DSC 0039 807d7
DSC 0040 53179

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...