WATAALAMU
wa masuala ya afya na kilimo kutoka mataifa mbalimbali duniani,
wamebaini mahindi, karanga na mihogo yenye sumukuvu ni moja ya vitu
vinavyochangia saratani ya ini, udumavu wa mwili na akili kwa watoto.
Ingawa takwimu sahihi hazijapatikana kuonesha madhara ya kila
Kutokana
na ukubwa wa tatizo, wataalamu hao kutoka nchi 20, wanakutana jijini
Dar es Salaam kwa siku tatu, kuanzia jana, kutafuta njia madhubuti za
kukabiliana na sumukuvu. Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi
zilizochukua hatua za awali dhidi ya tatizo hilo.
Akizungumza jana katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema,
“Lengo
la mkutano huu ni kuwapa fursa wataalamu kuja na mikakati
itakayoisaidia serikali na sekta binafsi kupambana na sumu ya aflatoxin
kwa kuwa hata hapa Tanzania ni tatizo kubwa.”
Dk
Mwinyi alifafanua kuwa, tatizo kubwa linaonekana kwenye mazao
yanayoathiriwa zaidi na sumukuvu ambayo ni mahindi, mihogo na karanga na
husababisha watumiaji kupata saratani ya ini na watoto hudumaa akili na
mwili.
Alisema
pamoja na serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na
sheria ya kudhibiti vyakula vinavyoingia nchini, lakini sheria pekee
haziwezi kumaliza tatizo hasa ikizingatiwa kuwa Watanzania wengi
wanatumia nafaka hizo wakati zikiendelea kukua shambani bila kuzipima
kiwango cha sumukuvu kinachotakiwa.
Sumukuvu
ni aina ya sumu inayosababishwa na kuvu katika mazao na ingawa
haiepukiki katika nafaka, kuna kiwango kinachopaswa kuwepo na
kinapozidi, huleta madhara hayo.
No comments:
Post a Comment