Wednesday, June 18, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 18, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


IMG-20140618-WA0000_b70f2.jpg
IMG-20140618-WA0001_2c722.jpg
IMG-20140618-WA0015_1691e.jpg
IMG-20140618-WA0016_e5359.jpg
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ROBO TATU YA WALIOFAULU WACHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO



Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa alisema kati ya waliochaguliwa wavulana ni 31,352 na wasichana ni 22, 733.PICHA|MAKTABA

Robo tatu ya wanafunzi waliofaulu kidato cha nne kwa kupata daraja la kwanza hadi la tatu (Division I – III), wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano. Idadi hiyo ya wanafunzi watakaojiunga katika shule za Serikali mwaka huu, imeongezeka kutoka 33,683 mwaka jana hadi kufikia 54, 085 sawa na asilimia 75.6 ya wanafunzi 71,527 wenye sifa ya kujiunga na kidato cha tano Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa alisema kati ya waliochaguliwa wavulana ni 31,352 na wasichana ni 22, 733.

“Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2014 ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. 
Kati yao wavulana 14, 826 sawa na asilimia 27.41 wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi na wengine 16, 526 sawa na asilimia 30.5 wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi ya jamii,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MBASHA APANDISHWA KIZIMBANI KWA UBAKAJI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara, Emmanuel Mbasha. PICHA|MAKTABA 

Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara, Emmanuel Mbasha amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa mashtaka ya ubakaji. Mbasha ambaye pia ni mume mwa mwimbaji maarufu wa Injili nchini, Flora Mbasha alipandishwa kizimbani jana na kusomewa mashtaka mawili ya ubakaji.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Mei 23 na 25, mwaka huu, eneo la Tabata Kimanga, Ilala, Dar es Salaam.Wakili Katuga alidai kuwa katika tarehe hizo, mshtakiwa alimbaka mtoto (jina linahifadhiwa), mwenye umri wa miaka 17, kinyume cha sheria.
Hata hivyo, Wakili Katuga alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Ingawa dhamana ya mshtakiwa huyo ilikuwa wazi, aliswekwa mahabusu, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yalikuwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja akiwa ni mfanyakazi wa taasisi inayotambulika, ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni kila mmoja.
Hakimu Wilberforce Luhwago anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi kesho itakapotajwa kwa ajili ya kuangalia iwapo mshtakiwa amekamilisha masharti ya dhamana. Mbasha alifikishwa mahakamani hapo asubuhi akiwa amevaa shati jekundu la mikono mirefu, suruali ya rangi ya udongo na kandambili nyekundu.
Mahakamani hapo alikuwa ameambatana na wanaume wawili. Wakati akisubiri kupelekwa mahabusu, saa 7:35, watu hao aliokuwa ameambatana nao walikwenda kumnunulia chakula na maji kabla ya kuongozwa na polisi kwenda kupanda basi la Magereza kuungana na mahabusu kuelekea Gereza la Keko saa 7:05. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WAKUU WA POLISI WAFUTWA KAZI NCHINI KENYA

Inspekta wa polisi Kenya, David Kimaiyo
Idara ya polisi nchini Kenya imefanya mabadiliko ya dharura katika afisi kuu za Kaunti ya Lamu, kutokana na mashambulio yaliyosababisha vifo vya watu 60 wiki hii. Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya David Kimaiyo amechapisha katika mtandao wa jamii Twitter, maelezo ya wakuu wa polisi katika kaunti hiyo waliofutwa kazi mara moja, wakiwemo makamanda wa polisi.
Afisa mkuu wa kituo cha Polisi, OCS, pia amehamishwa kituo mara moja. Hatua hii tayari imepokewa kwa hisia tofauti huku wakenya wengi wakielezea kutoridhishwa na adhabu hiyo.
Miongoni mwa walioandika malalamiko yao kwa Bwana Kimaiyo, wamesema kuwa mabadiliko yalistahili kufanyika hadi ngazi ya juu zaidi, baadhi hata wakimtaka yeye mwenyewe kama Inspekta wa polisi kujiuzulu.
Tangu kutokea shambulio la Jumapili usiku katika kijiji cha Mpeketoni, karibu na kisiwa cha Lamu pwani ya Kenya, lawama zimeelekezwa kila upande, huku baadhi wakidai kuwa wanasiasa wamehusika na wengine wakilalamikia utepetevu wa polisi katika kutekeleza majukumu yao.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alihutubia taifa Jumanne akisisitiza kuwa ana imani kuwa mashambulio hayo yalichochewa kisiasa. Ametoa matamshi hayo licha ya taarifa kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiislamu wa AL shabaab waliodai kuwa wao ndio waliohusika.
Matamshi ya rais Kenyatta yame kejeliwa na wanasiasa wa upinzani nchini humo waliodai kuwa rais huyo hana ufahamu wa yale yanayoendelea nchini mwake.

Seneta kutoka chama kikuu cha upinzani, Moses Wetangula amesema matamshi ya rais sio ya kweli. '' Badala ya kuitisha usaidizi wa wenzetu wenye teknolojia bora, hata tutumie ndege zisizo na rubani kuwalipua huko waliko, tunakaa hapa Nairobi na kudai AL shabaab hawakuhusika.'' Wetangula aliambia bunge la Kenya. '' Huu ni mzaha,'' Aliongeza bwana Wetangula.
Lakini uchunguzi uliofanywa na BBC umeonesha kuwa huenda kuna uzito kwa madai ya rais Kenyatta. Wakaazi wengi wa Mpeketoni waliozungumza na BBC wametueleza kuwa, wanaamini shambulio la Jumapili usiku linatokana na mzozo wa ardhi kati ya jamii zinazoishi huko. Wakaazi hao wamesema kuwa Al shabaab wamedakia tu kujigamba kwa yaliotokea huko ila wao wanaamini kuwa ni jambo lililokuwa likitokota kwa muda mrefu.
polisi waimarisha usalama
Huku hayo yakiarifiwa, polisi wanasemekana kuimarisha doria katika eneo la Lamu na vitongoji vyake. Wanajeshi wachache wametumika kuimarisha usalama hasa katika kijiji cha Mpeketoni. Katika taarifa zilizotufikia ni kuwa Polisi wameimarisha usalama katika mkoa wa magharibi mwa Kenya kutokana na duru walizopokea kuwa huenda eneo hilo likalengwa kwa shambulio.
Al shabaab wamefanya mashambulio ya mara kwa mara katika sehemu mbali mbali nchini Kenya tangu majeshi ya Kenya yaingie nchini Somalia mwaka wa 2011, katika oparesheni ya kuwafagia kutoka nchini humo. Shambulio la punde zaidi linadaiwa kufanywa kama kulipiza kisasi ya kuuawa kwa masheikh 2 wa kiislamu katika mji wa Mombasa pwani ya Kenya hivi majuzi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DAKIKA 90 ZA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA ZA JUNI 17

Kwenye mechi zilizochezwa usiku wa June 17 2014 matokeo yake ni Russia 1 (Kerzhakov 74′ ) – 1 Korea Republic goli lao lilifungwa na K Lee kwenye dakika ya 68.
Game nyingine ilikua ya Brazil vs Mexico iliyoisha kwa 0-0 huku ile ya nyingine ya mwanzo ikiwa ni Belgium 2 ( Fellaini 70′ + Mertens 80′) – 1 Algeria (Feghouli aliefunga kwa penati dakika ya 25 ) Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MASHABIKI WA SOKA WALIPULIWA

Mlipuko watokea Yobe watu wakitizama kombe la dunia
Shambulio limetokea katika jimbo la Yobe nchini Nigeria wakati watu wakitazama mechi za kombe la dunia. Jimbo hilo limewekwa katika hali ya hatari huku maafisa wa usalama wakijaribu kukabiliana na mashambulio yanayofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wakaazi wanasema walisikia sauti ya mlipuko mkubwa nje ya eneo la kutazama sinema mjini Damaturu ambapo mashabiki wa soka walikua wamejumuika kutazama mechi za kombe la dunia. Walioshuhudia wanasema mshambuliaji wa kujitolea mhanga aliyekuwa amebebwa kwa baiskeli alijilipua karibu na mgahawa katika jimbo la Yobe wakati mechi kati ya Brazil na Mexico ikiendelea.
Yobe imekumbwa na mashambulizi ya Boko Haram katika miaka iliyopita.
Duru kutoka hospitalini zinasema malori kadhaa yamewasafirisha majeruhi kupata matibabu na polisi wanasema maafisa wamepelekwa katika eneo hilo. Mfanyikazi mmoja wa hospitali ameaimbia BBC kuwa waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu na mikono.

Wiki iliyopita maafisa wa utawala katika jimbo la Adamawa ambalo liko katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria walipiga marufuku watu kujumuika katika maeneo ya umma kutazama mechi za kombe la dunia kutokana na hofu ya Usalama. Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya shambulio kutokea katika eneo la burudani na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.

Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa yako katika hali ya tahadhari kuanzia mwezi Mwezi 2013 kufuatia mashambulizi ya kila mara ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram. Takriban watu 2,000 wamepoteza maisha yao yangu visa vya uasi kuanza kutekelezwa mwaka wa 2009. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...