Wednesday, June 18, 2014

MASHABIKI WA SOKA WALIPULIWA

Mlipuko watokea Yobe watu wakitizama kombe la dunia
Shambulio limetokea katika jimbo la Yobe nchini Nigeria wakati watu wakitazama mechi za kombe la dunia. Jimbo hilo limewekwa katika hali ya hatari huku maafisa wa usalama wakijaribu kukabiliana na mashambulio yanayofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wakaazi wanasema walisikia sauti ya mlipuko mkubwa nje ya eneo la kutazama sinema mjini Damaturu ambapo mashabiki wa soka walikua wamejumuika kutazama mechi za kombe la dunia. Walioshuhudia wanasema mshambuliaji wa kujitolea mhanga aliyekuwa amebebwa kwa baiskeli alijilipua karibu na mgahawa katika jimbo la Yobe wakati mechi kati ya Brazil na Mexico ikiendelea.
Yobe imekumbwa na mashambulizi ya Boko Haram katika miaka iliyopita.
Duru kutoka hospitalini zinasema malori kadhaa yamewasafirisha majeruhi kupata matibabu na polisi wanasema maafisa wamepelekwa katika eneo hilo. Mfanyikazi mmoja wa hospitali ameaimbia BBC kuwa waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu na mikono.

Wiki iliyopita maafisa wa utawala katika jimbo la Adamawa ambalo liko katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria walipiga marufuku watu kujumuika katika maeneo ya umma kutazama mechi za kombe la dunia kutokana na hofu ya Usalama. Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya shambulio kutokea katika eneo la burudani na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.

Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa yako katika hali ya tahadhari kuanzia mwezi Mwezi 2013 kufuatia mashambulizi ya kila mara ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram. Takriban watu 2,000 wamepoteza maisha yao yangu visa vya uasi kuanza kutekelezwa mwaka wa 2009. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...