Friday, March 01, 2013

SOGGY DOGGY "HUNTER" AACHA KAZI UHURU FM,ATIMKIA KWA WANYARU-IRINGA

 


Msanii/Mtangazaji Soggy Doggy ameacha mzigo pande za redio Uhuru na leo rasmi ameondoka Dar es salaam nakwenda Iringa ambapo atakuwa akifanya kazi katika kituo kingine cha Redio kinachoenda kwa jina la Ebony Fm.Soggy Doggy ashawahi kufanya kazi katika vituo vya redio mbalimbali hapa nchini kama Arusha na Mwanza.

Mtendaji mkuu TAZARA Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika aachia ngazi.



Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika,(Pichani) hatimaye ameachia ngazi baada ya kuendesha kampeni kali ya miezi kadhaa kutaka aendelee kuongoza Mamlaka hiyo kwa miaka mingine mitatu.
Hatua hiyo ya kuachia ngazi imekuja baada ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri la Mamlaka hiyo kuonyesha dhahiri kutotaka Mzambia huyo aendelee na uongozi wa TAZARA kutokana na utendaji wake mbovu na uongozi mbaya uliowabagua wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa misingi ya utaifa wao.
Habari za ndani za Mamlaka hiyo zimesema Bw. Akashambatwa ambaye kipindi chake cha uongozi kiliisha tarehe 22 Januari, 2013 kiliongezwa kwa maombi maalum ya Serikali ya Zambia kwamba Serikali hiyo ilihitaji muda mrefu kidogo kumpata mbadala wake, licha ya Serikali ya  Tanzania kutoridhishwa na utendaji wake.
Katika kikao chake cha tarehe 20 Februari, 2013 jijini Lusaka, Zambia, Baraza la Mawaziri lilijadili kwa siri na kwa kirefu suala la mtendaji Mkuu huyo ambaye inasemekana aliombewa tena na Serikali ya Zambia kipindi cha nyongeza, ombi ambalo inadaiwa lilipingwa vikali na ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Taarifa za uhakika ndani ya Wizara ya Uchukuzi zinasema Serikali ya Tanzania haikumtaka Mtendaji Mkuu huyo kwa sababu kadhaa zikiwemo :uwezo mdogo, ubadhirifu, kuchochea ubaguzi kati ya Watanzania na Wazambia, ukaidi na uchochezi. Inadaiwa kuwa Mtendaji Mkuu huyo alizuia kuanzishwa kwa mradi wa usafiri jijini Dar es Salaam bila sababu yoyote ya msngi na kuishia kusambaza taarifa za uongo na uchochezi Zambia na magazeti mbalimbali nchini.
Tarehe 25 Februari, 2013 Gazeti la kila siku la Zambia, Zambia Daily Mail, liliripoti tukio hilo la kuachia ngazi kwa kiongozi huyo ambaye anajulikana sana nchini Zambia kama mfanyabiashara na kiongozi wa kimila (chief),                                              
Gazeti hilo lilinukuu barua ya Bw. Akashambatwa ya tarehe  22 Februari, 2013 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ujenzi, Ugavi na Mawasiliano ya Zambia, akielezea kuwa hakuna faida ya kuomba kurefushwa kwa mkataba wake wakati vyombo vikuu vya uongozi vya TAZARA, Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri, havionyeshi kumkubali.
Kuondoka kwa Bw. Akashambatwa kwenye uongozi wa TAZARA kunatarajiwa kupokewa na wafanyakazi wa TAZARA kwa nderemo na vifijo.

Google Waja na Miwani Inayopiga na Kurekodi Picha kwa Maelekezo.

Glass ya google
TEKNOLOJIA waliyotumia Google kutengeneza miwani ambayo ina uwezo wa kumpiga picha mtu au kurekodi bila muhusika kujua (google glass) sio mpya ila Kampuni ya Google ndio wakwanza kuja na teknoloji hiyo, ili kila mtu aweze kutumia na inakadiriwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo.
Google glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa kusema ni “OK Glass, take a picture.” upo kwenye foleni unaona fujo unataka kuchukua video, mwambie Google Glass naye atakusaidia kuchukua video. Hii ndio kali, unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote hayo, inakuja na kitu kama “Skype-style video chat”.
Umesafiri kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia kuchukua kutafsiri lugha. Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa tour guide.
Google glass ni kifaa ambacho unaweza kutumia kurekodi video, kupiga picha, kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, na unaweza fanya yote haya bila kutumia mikono yako (hands free). Tatizo ni kwamba, ukishavaa hiki kifaa kama miwani, watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au vipi, na kwa wabongo walivyo wanavyojua kujihami kupigwa picha au kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass unaweza tolewa baa.

 Kwa nchini Tanzania kifaa hiki ambacho kitakuwa na wastani wa bei ya sh. mil 2. 2 ($1500). Hata hivyo kifaa hicho kinachovaliwa kama miwani, sijui kama utaweza kutembea nacho hata hatua kumi kabla ya vibaka kukuvaa baada ya kujua thamani yake. Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini? Acha maoni yako.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

MWANAMZIKI AMUITA SHABIKI JUKWAANI NA KUANDA "KUDENDEKA" NAYE



 Baada ya Mziki kukolea Msanii Akimuita shabiki stajini ili wacheze naye lakini mambo yalikolea zaidi pale walipojikuta wana kisiana stejini kitu kilichosababisha minongono kwa mashabiki



Udaku spesho.

Rais Kagame wa Rwanda akanusha kuwa na nia ya kugombea tena urais kwa awamu ya tatu.


 

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema hana mpango wa kugombea tena muhula wa tatu madarakani baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2017.
Akizungumza mjini Kigali, rais Kagame amevishutumu vyombo vya habari kuanzisha mjadala juu ya iwapo ataibadili katiba ili aweze kuwania muhula mwingine.
Mjadala huo ulifuatia hatua ya rais huyo mapema mwezi huu kuunda kamati katika chama chake, kutafakari mwelekeo wa nchi baada ya muda wake madarakani kumalizika.
Chama cha upinzani cha FDU-Inkingi, kimetoa tangazo kikilaani njama zozote za kuifanyia marekebisho katiba ili kuruhusu muhula wa tatu kwa rais.-DW

Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.Dianna Melrose awasilisha hati zake za utambulisho ikulu



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.Dianna Melrose ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi (Picha na Freddy Maro)

Hivi ndivyo Chadema walivyotikisa Mbeya jana


Mapokezi makubwa ya Mh. Freeman Mbowe katika viwanja vya Rwanda Nzovwe jijini Mbeya.



 Burudani mbalimbali pia zilikuwepo





 




Mh. Mbowe pia alimtaka waziri wa Elimu na mafunzo  ya ufundi kujiudhuru pamoja na naibu waziri wa wizara hiyo kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne  na kusema kuwa katika siku 14 alizozitoa zimebaki siku tatu za wao kuendelea kuwepo madarakani na kuongeza kuwa wasipofanya hivyo wataitisha maandamano ya nchi nzima kushinikiza waondolewe katika nafasi hizo. Mara baada ya kauli hiyo Mbowe aliwataka wananchi kuchangia fedha kwaajili ya wahanga siku ya maandamano ambapo zilichangishwa fedha kiasi cha sh. 3, 267, 550/=



 

Wakichangisha fedha kwaajili ya wahanga wa maandamano yatakayofanyika pindi mawaziri wataposhindwa kujiudhuru picha ya kwanza ni Mh. Sirinde, inayofuata ni Mh. Msingwa na ya mwisho ni Mh. Mbowe.

 

Picha na Keny Pino

JOKETI KUPAMBA UZINDUZI KAMPENI YA UNYANYASAJI




Na Mwandishi wetu

MWANAMITINDO nyota nchini, Joketi Mwegelo, anatarajiwa kunogesha uzinduzi wa kampeni ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kike, unaotarajiwa kufanyika keshokutwa, ambapo shughuli mbalimbali na mada zitatolewa.


Joketi, ambaye anawika katika tasnia mbalimbali nchini  ikiwemo urembo, mitindo, muziki na filamu, atashiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama Okoa Mtoto wa Kike Tanzania utakaofanyika katika Kata ya Nyamongo wilayani Tarime, Mara.


Taarifa ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group iliyoandaa kampeni hiyo, Mossy Magere, imesema kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika na Joketi atawasili wilayani Tarime kesho tayari kwa kushiriki na atatoa mada ya masuala ya ujasiriamali kwa washiriki wa tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa.


Mossy alisema kuwa mbali na Joketi, wasanii mbalimbali watashiriki kutoa burudani wakiwemo wasanii nyota wa bongo fleva na wale wa asili wanaotamba mkoani Mara.


'Maandalizi yote ya msingi yamekamilika na kinachosubiriwa ni muda wa uzinduzi ufike, Joketi anatarajiwa kuwasili hapa kesho tayari kwa kushiriki nasi. Atapata fursa ya kutoa mafunzo na mbinu

za kimaisha kwa washiriki ambao wengi ni wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani hapa,' alisema Mossy.


Kampeni hiyo ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi sita, itazinduliwa rasmi keshokutwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye ameshirikishwa kwa karibu na Kampuni ya Nyumbani Kwanza.
Alisema mchakato wa uundwaji wa klabu za wapinga unyanyasaji  katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Tarime ambapo kampeni hiyo inaanzia umekamilika na wanafunzi wamevutiwa na kujiunga kwa wingi kwenye klabu hizo ambazo zitakuwa kichocheo cha kuendeleza kampeni hiyo.


Mossy aliongeza kuwa, uundwaji wa klabu hizo unalenga kukiwezesha kizazi cha sasa na kijacho kuwa mstari wa mbele kukataa vitendo vya unyanyasaji.


“Kila jambo jema huanzia ngazi za chini, kwa sasa tunaendelea kuunda klabu za wapinga unyanyasaji ambazo zitakuwa zikipewa mafunzo na mbinu mbalimbali ili kuwajenga kufahamu madhara wakiwa wangali  wadogo shuleni.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...