Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema hana mpango wa kugombea tena muhula wa tatu madarakani baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2017.
Akizungumza mjini Kigali, rais Kagame amevishutumu vyombo vya habari kuanzisha mjadala juu ya iwapo ataibadili katiba ili aweze kuwania muhula mwingine.
Mjadala huo ulifuatia hatua ya rais huyo mapema mwezi huu kuunda kamati katika chama chake, kutafakari mwelekeo wa nchi baada ya muda wake madarakani kumalizika.
Chama cha upinzani cha FDU-Inkingi, kimetoa tangazo kikilaani njama zozote za kuifanyia marekebisho katiba ili kuruhusu muhula wa tatu kwa rais.-DW