Thursday, October 10, 2013

SAKATA LA MADAWA YA LAMGEUKIA NEY WA MITEGO.... MAAFISA WA USALAMA WAANZA KUCHUNGUZA NYENDO ZAKE


Rapper Nay Wa Mitego amesema amekuwa akisumbuliwa mno na maafisa usalama pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wanaomdhania kuwa anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kitu ambacho amekuwa akikanusha kwamba sio kweli. Akiongea na Bongo leo kwa njia simu Nay amesema anasikitishwa kupokea taarifa zinazodai kuwa anajihusisha na biashara hiyo haramu, kitu ambacho hakifanyi kwakuwa anategemea shughuli zake za muziki zinazomlipa vizuri.
“Watu wamekuwa wakishangaa sifanyi show hata mwaka mzima lakini maisha yanaenda namiliki gari ndio maana wanaongea mengi huku media na maafisa usalama wananichunguza kila siku,” alisema Nay.
 
Msanii huyo wa Salam Zao amesema yupo kwenye maongezi na kampuni ya simu ili imfanye kama balozi wake.
“Nasubiria mambo yangu yaende poa, nimeingia mkataba wa kuwa balozi wa mtandao wa simu hapa nchini bado muda wake kuuweka wazi kwasababu tupo kwenye makubaliano zaidi na pia ikifika muda nataka kuanika vyanzo vyangu vyote vya mapato, ” alisema.

KENYA: HAKUNA RAIS AMEWAHI KUFIKA ICC


Amina Mohammed amesema kwa kuwa Kenyatta ni rais hali inabadilika kuhusu ICC
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed amesema kuwa hakuna rais hata mmoja aliye mamlakani amewahi kufikishwa mbele ya mahakama ya ICC. Taarifa hii bila shaka imetafsiriwa na wengi kuwa mpango wa Kenya kutokubali Rais Uhuru Kenyatta kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC mwezi ujao.
Duru zinseama kuwa kuwa hofu kuwa huenda Kenyatta akakosa kufika mahakamani kama alivyoamrishwa na mahakama.
Waziri Amina amesema kuwa Rais Kenyatta yuko tayari kushirikiana na mahakama ya ICC lakini kwa kuwa yeye ni rais hali imebadilika. Kenyatta anatakikana na mahakama ya ICC kuhusiana na uhalifu dhidi ya bindamu katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/2008
Bi Abdalla aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku tatu kabla ya mkutano wa Muungano wa Afrika kujadili uhusiano wa Afrika na mahakama ya ICC.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 10, 2013

DSC 0042 ad260
DSC 0033 484f1
DSC 0034 cbb76

VYOMBO VYA HABARI KUTOWAANDIKA WAZIRI MUKANGARA NA MWAMBENE


WanahabariClip_1f73f.jpg
Wadau wa habari nchini wametangaza msimamo wa kutotangaza wala kuandika habari zinazomhusu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari(Maelezo), Assah Mwambene kama sehemu ya kupinga mwenendo wa serikali wa kuvifungia vyombo vya habari.
Wadau hao kutoka taasisi mbalimbali za habari wamesema kuwa pamoja na kilio cha muda mrefu cha kuitaka serikali kufuta Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, lakini hakuna jambo lolote lililofanyika mbali ya kuendelea kuviandama vyombo hivyo.
Katika taarifa yao, wadau hao wamesema pia wamesikitishwa na tabia iliyoonyeshwa na Dk Mukangara na Mwambene kuchukua uamuzi wa kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania bila kuyasikiliza na kupotosha umma juu ya jambo hilo.
"Kwa msingi huo, wadau tumeamua kwamba tutasitisha kuandika, kutangaza na kupiga picha shughuli zozote zitakazowahusisha au kuratibiwa na Dk Mukangara na Mwambene hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Adhabu hiyo inaanza mara moja kuanzia leo," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

AFISA USALAMA ‘FEKI’ ANASWA MTEGONI

IMG 4926 e7e26

Kitambulisho cha Usalama wa Taifa, alichokuwa akitumia, Bw. Magige, kwenye majukumu aliyokuwa akijipangia

IMG 4927 1d844

Bw. Kennedy Magige, anayedaiwa kuwa Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa 'feki' akiwa hoi baada ya kunaswa na kupata kipigo kutoka kwa wananchi.
IMG 6228 779e5

Bw. Magige na mtuhumiwa mwenzake wakiwa kwenye gari la Polisi tayari kupelekwa kituoni

IMG 6245 13f0e

Gari aina ya Land Cruiser Prado, alilokuwa akitumia wakati wa shughuli zake za kila siku  

Watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya utapeli , huku mmoja akitumia kitambulisho kinachomtambulisha kuwa ni ofisa mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa, wametiwa mbaroni jijini Dar es Salaam.

BERGKAMP ATAKA KUREJEA ARSENAL KUPIGA KAZI

arsenal a88a5
GWIJI wa Arsenal, Dennis Bergkamp ameelezea nia yake ya kujiunga na dawati la makocha la timu ya Arsene Wenger.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 44 alunga mabao 87 katika miaka yake 11 ya kuchezea Arsenal na amesema klabu hiyo ina nafasi maalum moyoni mwake.
Robert Pires amekuwa akisaidia kuendesha mazoezi katika Uwanja wa Gunners, London Colney na Bergkamp, ambaye aliichezea timu hiyo kuanzia mwaka 1995 hadi2006, anaweza kuungana naye.
"Hisia alizonazo Johan Cruyff kwa Barcelona, nami ninazo hizo hizo kwa Arsenal," Bergkamp aliiambia Telegraph.
"Nikiwa Arsenal ilikuwa babu kubwa. Wakati wote nafurahia. Sijawahi kuwa na siku mbaya humo. Ipo katika fikra zangu wakati wote. Ni sehemu ya malengo yangu kurejea huko.
"Naona kama naweza kuwa sehemu ya makocha. Nafurahia hiyo kazi, hususan kufundisha vitu binafasi kwa washambuliaji,".
Bergkamp alijipatia sifa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka, ubunifu na maarifa ya kisoka alipokuwa Arsenal.
Mchezaji mpya ghali wa Arsenal, Mesut Ozil amekuwa akifananishwa na Mholanzi huyo, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi amesema kila mchezaji ni wa kipekee.
Sasa akiwa kocha Msaidizi wa Ajax, Bergkamp amevutiwa na mwanzo mzuri wa Arsenal msimu huu na kusema Ozil ni kipaji maalum.
"Pamoja na heshima zangu zote kwa wachezaji wengine wote wa Arsenal, nafikiri ni mmoja ambaye anaweza kutengeneza tofauti,"alisema.
"Wachezaji wengine ni wazuri katika kiungo. Lakini unahitaji mtu mmoja fulani wa kiwango cha juu ambaye anaweza kuhaha Uwanja mzima,". Chanzo: binzubeiry

CHICHARITO ATAJA SABABU KWA NINI ATAONDOKA MAN U

chicha fe087
MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amesema anaweza kuondoka Manchester United ili kusaka timu ambayo atapata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.


Mshambuliaji huyo anayefahamika kama Chicharito hapewi nafasi kubwa katika klabu ingawa mwezi uliopita aliifungia timu hiyo bao la ushindi katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One dhidi ya Liverpool na zaidi ya mechi hiyo alianza katika mechi nyingine moja tu, United ikifungwa nyumbani na West Brom.
Hernandez amesema kwamba wakati akiwa ana furaha kuchezea klabu kubwa kama hiyo, pia anataka nafasi zaidi za kucheza na anaamini anaweza kuwa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza iwe Old Trafford au katika klabu yoyote.
"Nasotea hiyo [kuanza katika mechi zaidi],"alisema Hernandez akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Mexico, Deportes Telemundo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...