Saturday, August 09, 2014

WASALITI UKAWA: WAJIANDAE KUWA 'WABUNGE WA MAHAKAMA'

Mjumbe wa Bunge la Katiba (Chadema) Said Arfi  akisaini karatasi ya mahudhurio bungeni jana, kabla ya kwenda  kushiriki mjadala wa kamati  yake.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa wabunge wote walio wanachama wake, lakini wanakiuka msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa kuingia katika Bunge la Katiba, wajiandae kuongeza idadi ya ‘wabunge wa mahakama’.
Kauli hiyo ya tahadhari imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ya baadhi ya wabunge wa chama hicho kuonekana mjini Dodoma, kunakofanyika vikao vya Bunge Maalumu la Katiba (BMK) ambalo Ukawawamesusia kuhudhuria.
“Ni bora wawe wabunge wa mahakama kama mwenzao (akimlenga Zitto Kabwe), kuliko kuendeleza usaliti ndani ya chama. Tunatarajia kukaa na wenzetu kushauriana nini cha kufanya dhidi ya wote wanaoenda kinyume na  msimamo wa Ukawa,” alisema Tundu Lissu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 09, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LIPUA LIPUA YA KAMATI ZA BUNGE MAALUMU LA KATIBA

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana. Picha na Emmanuel Herman.

Kamati za Bunge Maalumu la Katiba zilizoanza vikao vyake juzi mjini Dodoma, zimejikuta zikifanya kazi kwa kulipua kutokana na uchache wa muda uliotengwa, ikilinganishwa na ukubwa wa kazi ya uchambuzi wa ibara za rasimu ya Katiba hiyo.
Kamati hizo zimetengewa siku 14 kwa ajili ya kujadili na kuchambua sura 15 za rasimu hiyo na siku mbili za kuandaa taarifa ambazo zitaanza kuwasilishwa kwenye Bunge Maalumu, Septemba 2, mwaka huu.
 Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wamekuwa wakilalamikia ufinyu wa muda uliotengwa na kwamba kazi imekuwa ikifanyika kwa kulipua, ili kuhakikisha kwamba wanamaliza katika muda uliopangwa.
 Malalamiko hayo yanatokana na ukweli kwamba baadhi ya sura za rasimu zina ibara nyingi ambazo ni vigumu kuzijadili kwa kina, kuzifanyia marekebisho kisha kuzipigia kura kwa lengo la kuzipitisha.
 Waraka wa mgawanyo wa sura kwa siku za mjadala katika Kamati za Bunge Maalumu unaonyesha kuwa kamati zilipaswa kujadili sura ya pili na ya tatu za rasimu hiyo siku ya kwanza zilipoanza kuketi, sura hizo zina jumla ya ibara 13, kazi ambayo baadhi ya wajumbe walisema ilikuwa ni vigumu kuikamilisha kwa siku moja.
 Mwenyekiti wa Kamati namba tano, Hamad Rashid Mohamed juzi alikiri kuwapo kwa changamoto ya muda lakini akasema: “Hiyo ndiyo hali halisi, lazima tutumie muda huo ambao tumepewa na tufanye kazi kwa ufanisi”. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WABUNGE WA CCM WAMEGUKA KATIBA MPYA...!!!




Kwa nini tukae siku 87 au 90 wakati tunajua upande wa pili haujakamilika? Kwa mujibu wa sheria inatakiwa ridhaa ya theluthi mbili. Mwigulu Nchemba 

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kumeguka baada ya baadhi ya wabunge wake ambao ni Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kuunga mkono kauli ya Naibu Katibu Mkuu wake, Mwigulu Nchemba.

Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Jumanne iliyopita akichangia wakati wa mjadala wa mabadiliko ya kanuni, alilitaka Bunge Maalumu la Katiba lijitathmini kama lina ulazima wa kuendelea wakati hakuna uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili.


Alisema kitendo cha Bunge hilo kukaa kwa siku 84 bila uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili kwa pande zote mbili inayohitajika kupitisha Rasimu ya Katiba Mpya, hakiwezi kueleweka kwa Watanzania.

Nchemba alisema ni vyema kujua idadi ya wanaoshiriki awamu ya pili ya Bunge hilo ili kutoa uthibitisho  kimahesabu kama uamuzi wa kuendelea kwa Bunge unaweza kuwa na maana.

Jana Mwigulu Nchemba alizidi kusisitiza kauli aliyoitoa akisema ni msimamo wake binafsi kama mtoto wa maskini. Alisema anatambua jinsi walipa kodi watakavyoumia, rasimu hiyo itakapokwama kupita kutokana na kukosekana kwa theluthi mbili ya pande zote.


Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  juzi alijibu akisema kauli ya Nchemba ni mtazamo wake binafsi na hakuongea kama kiongozi wa chama hicho.

Lakini jana wabunge mbalimbali wa CCM walijitokeza hadharani wakisema wanaunga mkono kauli ya Nchemba ili hesabu ijulikane badala ya kuendelea kutafuna fedha za wananchi bila tija.

Ali Keissy

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy, alisema msimamo wa Nchemba ndiyo msimamo sahihi ambao unapaswa kufuatwa kuliko kuendelea na Bunge wakati wakijua kuwa theluthi mbili haitapatikana.

“Kama kuna wabunge wa CCM wanaounga mkono kauli ya Mwigulu kwa asilimia 100 basi mimi naunga mkono kwa asilimia 500 na wako wabunge wengi tu wa CCM wanaunga mkono,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WATU 6 WAUAWA KATIKA GHASIA SOMALIA

Wapiganaji wa Al-shabaab
Takriban watu sita wameuawa katika ghasia katikati mwa Somali.
Ijumaa usiku, wanamgambo kutoka kundi la Alshabaab walishambulia kambi moja ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika katika mji wa Buloburde ,yapata kilomita 200 kazkazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.
Vikosi vya Amisom viliuteka mji wa Buloburde kutoka kwa Alshabaab mapema mwaka huu,lakini wanamgambo hao bado wanadhibiti eneo kubwa la viungani mwa mji huo.
Wameendelea kutekeleza mashambulizi mjini Mogadishu ili kujaribu kuiondoa serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...