Monday, August 19, 2013

CHADEMA WAVAANA NA POLISI KWENYE MAANDAMANO YAO...!!!


Maandamano ya chama cha CHADEMA yaliyokua yanafanyika huko Mwanza yamegeuka vurugu baada ya wandamanaji kuanza kupambana na polisi.

CHADEMA walikua wakiandamana katika kushinikiza Meya wa Ilemela Henry Matata aachie ngazi kwani hana sifa zakua meya, baada ya kuvuliwa uanachama na chama hicho.

Katika picha zilizokirushwa kupitia televisheni ya Barmedas Tv ya Mwanza,  barabara zimeonekana zikiwa zimefungwa kwa mawe na miti, huku  katika maeneo mengine uchafu ukiwa umejazwa barabarani na matairi kuchomwa.

katika mtaa wa Mission waandamanaji wamefunga barabara kwa uchafu uliokua katika dampo moja kando ya barabara hiyo.

Maandamoano hayo yalikua yamalizikie viwanja vya furahisha ambapo viongozi wa chadema walikua wahutubie.

Chanzo cha vurugu hizo hakijafahamika, ikizingatiwa CHADEMA walikua na kibali cha kufanya maandamano hayo.

Hivi sasa polisi wametanda mitaani katika kudhibiti vurugu hizo na hali inaonekana kutengamaa.

PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI MOROGORO HII LEO ASOMEWA MASHITAKA 3.


Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye  Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ''Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ''katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.

VIONGOZI DECI JELA MIAKA 3 AU FAINI MILIONI 21 KILA MMOJA

SHERIA imewatia hatiani viongozi 4 kati ya 5 wa kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) iliyokuwa ikijihusisha na shughuli za kuvuna na kupanda fedha nchini kinyume cha sheria.

Hayo yalibainika hii leo wakati wa hukumu ya kesi hiyo iliyodumu kwa miaka kadhaa huku mtuhumiwa mmoja katika kesi hiyo akiachiw huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa yake.

Akisoma hukumu hiyo iliyo andikwa na Hakimu Mwenzake, Stuart Sanga, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Aloyce Katemana alitafsiri sheria kadhaa zilizowatia hatiani watuhumiwa hao.


Vigogo hao waliotiwa hatiani ni pamoja na Jackson Sifael Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo Saigaran ole Loitginye, Samwel Sifael Mtares,Samwel Mtalis huku sheria ikimwachia huru Arbogast Francis Kipilimba baada ya kushindwa kumtia hatiani.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AUGUST 19, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

SIRI ZA TRAFIKI FEKI ZAFICHUKA, YADAIWA ALIANZA KAZI MKOANI SINGIDA,AKAJIPA UHAMISHO WA KIKAZI HADI DAR...!!!


SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari 'feki' wa Usalama Barabarani mwenye cheo cha Sajini, akifanya kazi ya kuongoza magari eneo ya Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam, mambo mapya yamezidi kubainika juu ya sababu za mtu huyo kujiingiza katika kazi hiyo bila kutambuliwa na Jeshi la Polisi.


Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vya kuaminika, zinasema trafiki huyo 'feki', ambaye inadaiwa jina lake halisi ni James Juma Hussein (45), mkazi wa Kimara Matangini, alianzia kazi hiyo mkoani Singida kabla ya kujipa uhamisho wa kikazi kwenda Dar es Salaam.


Chanzo chetu kilieleza kuwa, trafiki huyo alikuwa na shemeji yake aliyeitwa Shaban ambaye aliajiriwa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani aliyekuwa akifanyia kazi mkoani Tabora.Vyanzo vyetu viliongeza kuwa, baada ya shemeji yake kufariki mkoani Tabora, trafiki huyo alipata mwanya wa kuchukua nguo za kazini alizokuwa akizitumia shemeji yake.

MECHI YA NGAO YA JAMII YA YANGA NA AZAM YAINGIZA MIL 208

 
Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa 2013/2014 iliyochezwa jana (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 208,107,000. Washabiki 26,084 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Yanga kushinda Azam bao 1-0.


Mgawanyo wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 31,745,135.59, asilimia 10 ya mchango wa kusaidia jamii sh. 20,810,700, gharama ya tiketi sh. 7,309,866.


Uwanja sh. 22,236,194.76, gharama za mchezo sh. 13,341,716.86, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,188,445.44, TFF sh. 13,341,716.86 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,670,858.43. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 43,731,183.03.

MAJINA YA WALIOKOSEA KUJAZA FOMU ZA MIKOPO KWENDA CHUO KIKUU

Tizama majina kwa kubofya hapa chini 

1.NOTICE TO LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION IN THEIR LOAN APPLICATIONS 
2.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 13: S - Z
3.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 12: S - S
4.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 11: N - S
5.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 10: M - N
6.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 9: M - M
7.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 8: M - M
8.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 7: M -M
9.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 6: L - M
10.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 5: K - L
11.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 4: J - K
12.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 3: F - J
13.LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION LIST 2: B - F
14.NOTICE TO LOAN APPLICANTS TO CORRECT NECESSARY INFORMATION IN THEIR LOAN APPLICATIONS

DEREVA DALADALA AFUMANIWA GESTI AKIWA NA BINTIYE.....!!!


  Za mwizi 40:Temba baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na   bintiye.
 
 AMA kweli za mwizi arobaini! Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Temba, mkazi wa Kimara-Rombo, Dar ambaye ni dereva wa daladala amefumaniwa laivu na mkewe akiwa gesti na binti yao wanayemlea.



NI MTEGO
Tukio hilo la aina yake lilijiri wiki iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo maeneo hayohayo ya Kimara-Rombo, majira ya saa 10:00 jioni ambapo Temba ambaye ni dereva wa daladala inayofanya safari kati ya Kimara na Kariakoo alinaswa kiulaini baada ya kuwekewa mtego.
OFM YATAARIFIWA
Baada ya mke wa Temba kuweka mambo vizuri aliitaarifu Oparesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ambapo alihojiwa maswali muhimu kisha kutakiwa kuwajulisha polisi ili kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.

                      Jamaa akipelekwa polisi na taulo lake
MWANZO WA YOTE HADI FUMANIZI
Kwa mujibu wa mke wa Temba, siku kadhaa nyuma aligundua kuwepo kwa mawasiliano ya kimapenzi kati ya mumewe na binti yao hivyo akalazimika kufanya uchunguzi wa kina.

BARCELONA YAFANYA KUFURU, YAIGONGA LEVANTE 7-0


Wachezaji wa Barcelona wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Alexis Sanchez dakika ya tatu.



Lionel Messi kama kawaida yake katupia mbili katika mechi ya leo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...