Monday, August 19, 2013

VIONGOZI DECI JELA MIAKA 3 AU FAINI MILIONI 21 KILA MMOJA

SHERIA imewatia hatiani viongozi 4 kati ya 5 wa kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) iliyokuwa ikijihusisha na shughuli za kuvuna na kupanda fedha nchini kinyume cha sheria.

Hayo yalibainika hii leo wakati wa hukumu ya kesi hiyo iliyodumu kwa miaka kadhaa huku mtuhumiwa mmoja katika kesi hiyo akiachiw huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa yake.

Akisoma hukumu hiyo iliyo andikwa na Hakimu Mwenzake, Stuart Sanga, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Aloyce Katemana alitafsiri sheria kadhaa zilizowatia hatiani watuhumiwa hao.


Vigogo hao waliotiwa hatiani ni pamoja na Jackson Sifael Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo Saigaran ole Loitginye, Samwel Sifael Mtares,Samwel Mtalis huku sheria ikimwachia huru Arbogast Francis Kipilimba baada ya kushindwa kumtia hatiani.

Miongoni mwa makosa yaliyokuwa yakiwakabili ni kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume na kifungu 111A(1,3) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 na Mahakama iliwatia hatiani kwa maosa mawili ambayo yote mawili yaliwatia hatiani na adhabu ya kifungo cha miaka 3 kila mmoja au faini ya milioni 3 na milioni 18 (21 Milioni). 

Kati yao washitakiwa wawili walifanikiwa kulipa faini ya Milioni 21 kila mmoja huku wengine wawili wakienda jela. 
Washtakiwa hao walipatikana na kesi ya kujibu Julai 16 mwaka jana , hivyo kutakiwa kujitetea baada ya mashahidi 16 wa Jamhuri kutoa ushahidi wao.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya mwaka 2007 na Machi 2009 katika Makao Makuu ya DECI, Mabibo, Dar es Salaam walikusanya fedha kutoka kwa wananchi wakiwaahidi kuwa watapata faida ya riba kubwa (kupanda na kuvuna).

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...