Friday, June 05, 2015

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 05, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC03316
DSC03317
DSC03318
Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

IDADI YA WALIOFARIKI GHANA YAFIKIA 175


Ghana moto
Takriban watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na stima.


Ghana moto
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra. Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.


Ghana moto
Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.

Ghana moto 
Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu, Accra alipotembelea eneo la tukio. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

RAHEEM STRLING KUELEKEA OLD TRAFFORD

Raheem Sterling
Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.

Hatahivyo Liverpool imesema kuwa haiko tayari kufanya biashara na wapinzani wao wakuu kutoka Kaskazini Magharibi. Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Luois Van Gaal anavutiwa na kasi ya mchezaji huyo na uwezo wake wa kuwaponyoka mabeki.

Sterling amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa kushinda mataji. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

SERENA ATINGA FAINALI FRENCH OPEN 2015

Serena William,mchezaji tenis nambari moja duniani akifurahia ushindi.
Serena Williams amefanikiwa kutinga fainali za michuano ya tenis ya French Open. Licha ya kujisikia kuumwa Serena aliweza kupambana vikali na kumbwaga mpinzani wake Timea Bacsinszky kwa seti 4-6 6-3 6-0 na kufuzu kucheza fainali za mwaka huu.

Serena nambari moja duniani kwa wanawake sasa atapambana na Lucie Safarova katika mchezo wa fainali kesho, Jumamosi. Serena amekuwa akiumwa kipindi chote cha michuano hiyo, kiasi kwamba anasema hakutarajia kushinda katika mchezo huo.

Serena anajaribu kushindi taji la tatu la michuano hiyo ya French Open na taji la ishirini la michuano mikubwa. Mapema katika uwanja wa Philippe Chatrier, Safarova wa 13 kwa ubora alimtupa nje MSerbia Ana Ivanovic na kuwa mwanamke wa kwanza wa Czech kufika fainali za michuano hiyo katika uwanja wa Roland Garros katika kipindi cha miaka 34.
Kwa upande wa Wanaume, fainali zitafanyika Jumapili hii. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...