SIKU chache
baada ya kufanyiwa fujo katika shoo yake nchini Ujerumani, staa wa
Mdogo Mdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kueleza namna ambavyo
alidhalilishwa nchini humo.
Diamond aliponea chupuchupu kupewa kipigo baada ya kuchelewa kwenye shoo iliyokuwa ifanyike katika Ukumbi wa Sindelfingen katika mji wa Stuttgart, Ujerumani.
Diamond aliponea chupuchupu kupewa kipigo baada ya kuchelewa kwenye shoo iliyokuwa ifanyike katika Ukumbi wa Sindelfingen katika mji wa Stuttgart, Ujerumani.
Staa wa Mdogo Mdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumza
na paparazi wetu baada ya kutua Bongo Jumanne iliyopita, Diamond
alisema anasikitika kwani alidhalilishwa wakati alipokuwa akidai haki ya
kumaliziwa malipo yake ya shoo euro 250 (zaidi ya sh 500,000). Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Inaniuma
sana kwani mimi pale nilikuwa nasimamia haki yangu, kwani nilikuwa
nawadai euro 250 sasa nikaona wananizungusha na nilipokomaa zaidi huku
wakiona muda wa shoo unapita, ndipo walipoanza kunitukana bila sababu.
“Wamenitukana
mimi, wamewatukana hadi ndugu zangu ambao hawakuhusika na chochote na
wala hawakuwepo kule. Wamenidhalilisha bila kosa. Kimsingi sikutaka
kupanda jukwaani pasipo kumaliziwa fedha zangu licha ya kuwa si nyingi
kiivyo,” alisema mtoto huyo wa Tandale.
Hali halisi ya ukumbi nchini Ujerumani ulivyoharibiwa na mashabiki waliovurugwa kwa kucheleweshewa shoo ya Diamond. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kwenye
maelezo menginena paparazi wetu, Diamond alisema baada ya kutokea vurugu
hizo alilazimika kurejea nchini pasipo kumaliziwa fedha zake lakini
promota wa shoo hiyo, Kamabritts aliahidi kuandaa shoo nyingine ya bure
ili kujisahihisha kwani kosa lilikuwa la kwake.
Kwenye
mvutano huo kati ya msanii na promota huyo, Diamond alitegemewa kupanda
jukwaani saa nne usiku lakini ilishindikana hadi ilipofika saa 10
alfajiri kitendo ambacho kilisababisha mashabiki wafanye vurugu kwa
kuvunja viti na thamani nyingine za ukumbi zinazokadiriwa kufikia Euro
128,222 (Sh. milioni 280).
NA GPL
No comments:
Post a Comment