Friday, September 05, 2014

TAZAMA PICHA ZA AJALI ILIYOTOKEA MUSOMA NA KUUA WATU ZAIDI YA 40

 Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba, Mjini Musoma mchana wa leo.
Watu zaidi ya 40 wamepoteza maisha papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio, ilielezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo, kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni hali iliyoipelekea dereva wa basi hilo kuamini kuwa atawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo. Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu, ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz 
Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 25 kupoteza maisha pamoja hapo.wakishuhudia tukio hilo la ajali.
Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni. Gari hii ilikuwa na watu watatu, ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.
Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.

Basi la J4 Express  T677CYC lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach T736AWJ leo asubuhi na watu zaidi ya 30 wanahofiwa kupoteza maisha huku webngine kadhaa wakijeruhiwa.
Ajali hiyo mbaya ambayo inaelezwa kuvunja rekodi ya matukio ya ajali ya barabarani yakihusisha mabasi kuwahi kutokea kwa mwaka huu, imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma wakati moja ya mabasi hayo yakiovateki gari lingine. Jambo Tz  Blog itawajuza zaidi kuhusiana na tukio hilo.
 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Jiachie Blog

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...