Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu.
WAKATI Mbunge wa Bariadi Magharibi (Chadema), John Shibuda akiwasilisha maoni ya wachache ya Kamati namba 8 ya Bunge Maalum la Katiba linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma Jumatano mchana, Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu alimsifu na kusema kuwa mwakilishi huyo wa wananchi ndiye orijino, ukimuona mwingine ni photokopi.
Shibuda
aliyeingia katika ukumbi huo akipingana na msimamo wa chama chake
kilichoamua kususia vikao hivyo kwa kushirikiana na vyama vya CUF na
NCCR-Mageuzi, alitumia pia nafasi hiyo kuwapiga vijembe viongozi wake,
akisema hana matatizo na Chadema, isipokuwa ana ‘bifu’ na mfumo wa
utumishi wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Akifafanua
kauli yake hiyo, Shibuda anayefahamika kwa mbwembwe na mikogo ya lugha,
alisema yeye ni kama mchezaji wa mpira aliye staa, akiwatolea mfano
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao wanaponunuliwa na timu yoyote,
huenda kwa ajili ya kuiimarisha na si vinginevyo.
Mbunge wa Bariadi Magharibi (Chadema), John Shibuda.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Mimi
nikihama timu naenda kuboresha timu nyingine, sijanunua chama chochote,
nitahama kwa sababu mimi ni staa nitakayehitajika kwa ajili ya kwenda
kukiimarisha, mtu kuhama msikiti hakumaanishi kwamba umehama dini,”
alisema huku akishangiliwa na wajumbe wengi wa bunge hilo.
Chadema
pamoja na vyama hivyo viwili vya upinzani vinavyounda umoja unaoitwa
Ukawa, vimesusia kuendelea na vikao vya bunge hilo vinavyojadili Rasimu
ya Katiba Mpya kwa maelezo kuwa wajumbe wa CCM wameondoa maudhui ya Tume
ya Jaji Joseph Warioba na badala yake, wanaingiza vipengele ambavyo
havikuwepo.
Kususa
huko kwa Ukawa kumesababisha kuwepo kwa wito kutoka makundi mbalimbali
yakitaka warejee bungeni ili kuendelea na majadiliano, hali iliyomfanya
Rais Jakaya Kikwete aingilie kati kwa kuzungumza nao, lakini muafaka
zaidi unatarajiwa kupatikana katika kikao kitakachokaa Jumatatu ijayo.
Kitendo
cha Shibuda kuhudhuria kikao hicho, kinatarajiwa kuchukuliwa hatua kali
na viongozi wa chama chake, hasa kutokana na historia yake ya kusigana
mara kwa mara katika masuala mbalimbali ya chama hicho. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment