Friday, September 05, 2014

NISHA AZUA TAHARUKI HEKALU LA FREEMASON...!!!


STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha', Jumanne iliyopita alijikuta akizua taharuki kufuatia kuegesha gari lake nje ya Hekalu la Freemason lililopo nyuma ya Hyatt Regency Dar es Salaam The Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam.


Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha'.

Taharuki hiyo ilikuja pale Nisha alipoegesha gari lake eneo hilo na kushuka kisha wanafunzi na watu wengine kusitisha shughuli na kumzunguka kutaka kujua kulikoni staa huyo kufika eneo hilo linaloaminika kuwa kila anayekwenda ni muumini wa imani ya Freemason.

Baadhi ya watu walimuuliza Nisha alichofuata kwenye hekalu hilo huku mwenyewe akishindwa kujibu kwani alitupiwa maswali mfululizo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz


Chanzo chetu kilidai kuwa msanii huyo baada ya kuona amezingirwa na watu alisimama na kuzungumza nao kisha akabadili uamuzi, alirudi ndani ya gari na kuondoka eneo hilo ambapo baadhi ya watu walidai huenda alitaka kuingia kwenye hekalu hilo kama mastaa wenzake ambao mara nyingi huonekana wakiingia na kutoka.

Upande wa mbele wa Hekalu la Freemason lililopo karibu na hoteli ya Hyatt Regency Posta, Dar es Salaam.


Kufuatia taarifa za chanzo hicho, gazeti hili lilimsaka msanii huyo na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo alifafanua kuhusu suala hilo."Aah! Dah, nyie habari hizo mmezipataje, mbona pale sijaona mwandishi yeyote? Ukweli pale mimi nilipaki gari tu kwa ajili ya kufanya mambo yangu maeneo yale lakini ghafla nikashangaa umati umenivaa, kila mtu anataka kuniona laivu na kuongea na mimi.

“Wanafunzi ndiyo usiseme, sasa kutokanana na  kusongwa na umati kama ule nikabadili maamuzi na kuondoka zangu,” alisema Nisha.

Kumekuwa na dhana miongoni mwa watu kwamba, baadhi ya mastaa wenye mafanikio Bongo wamejiunga na imani ya Freemason huku ikisemekana wanaishi kwa kuabudu kwenye hekalu hilo mara moja kwa wiki.

Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja ni staa gani mwanachana wa Freemason kwani hakuna aliyewahi kukiri kwamba yeye ndiye. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na GPL

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...