Tuesday, May 14, 2013

AJALI TENA WILAYANI RUGWE MKOANI MBEYA JIONI YA LEO MMOJA AHOFIWA KUFA MAJERUHI MWINGINE APELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

AJALI MBAYA IMETOKEA LEO JIONI MAENEO YA KANYEGELE KIWIRA WILAYANI RUNGWE ENEO HILO MAALUFU KWA JINA LA UWANJA WA NDEGE LORI LILILOKUWA NA SHEHENA YA CHUPA LIKITOKEA DSM KUELEKEA NCHINI MALAWI LILIKATIKA BLEKI NA KUPAA KUINGIA MSITU NDANI YA LORI HILO KULIKUWA NA DEREVA PAMOJA NA TINGO WAKE MASHUHUDA WA AJALI HIYO WAMESEMA HUWENDA MMOJA AMEFARIKI ILA MWINGINE HALI YAKE INASEMEKANA NI MBAYA 


MKUU WA WILAYA RUNGE AKISIMULIWA NA MOJA WA MASHUHUDA WA AJALI HIYO

AFANDE SELE, AKAANGUA KILIO JUKWAANI

                      MSANII mkongwe wa muziki wa bongo fleva  ambaye mpaka sasa anashikilia taji la mkali wa mashairi nchini Seleman Msindi'Afande Sele a.k.a Dume la Simba juzikati alizua taharuki kubwa kwa mashabiki waliofulika ndani ya kiwanja kipyacha Tanzanati Complex baada ya kuangua kilio jukwaani.Baada ya kuona hali hiyo waandaji wa shoo hiyo walipata jukwaani kwa kushirikiana na mabaunsa ambao kwa pamoja walimbembeleza msanii huyo bila mafaniki hali iliyosababisha baadhi ya mashabiki hasa wa kike nao kumsapoti kwa kuangua vilio vilivyovuma ukumbi mzima.

HATIMAYE BINTI ANAYEDAI KUBAKWA NA MBUNGE AMTAJA KUA NI MH LEMA, CHEKI PICHA




ZITTO KABWE APIGWA KIBUTI LIVE MTANDAONI NA DEMU WAKE ( LOVENESS DIVA)


Waswahili  husema  ..."Mapenzi  ni UCHIZI"... 
Hili  ndo  tunalolishuhudia  kwa  Mh Zitto  na Manzi  wake MAPEPE ( Loveness Diva )  ambaye  ameamua  kumtema  na  kupeleka  penzi  lake  kwa Prezzo wa Kenya..Kwanza  ulianza  ujumbe  wa  kumpongeza  Prezzo  na  ahadi  ya  kumtema  RAIS WETU MTARAJIWA....


 Baaye  kikafuata  KIBUTI  kwa  mh. Mbunge.

WABUNGE WADAIWA KUPEANA MIMBA, STORI YA SAKATA ZIMA HII HAPA


SKENDO nzito inalitafuna Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikitawala madai kwamba kuna wabunge wawili wanawake, wamejazwa mimba na waheshimiwa wenzao wanaume.
Awali, ulitawala uvumi kuwa mmoja wa wabunge wa upinzani (viti maalum), akitokea Kanda ya Kaskazini, amepewa ujauzito na mheshimiwa mwingine ambaye ni kiongozi anayeshika nafasi za juu kwenye moja ya vyama vikuu vya upinzani nchini (wote majina yao tunayahifadhi kwa sasa).
Kashfa hiyo ya mtunga sheria huyo kupewa mimba na mheshimiwa mwenzake ambaye ni mume wa mtu, ilipata mbeleko na kuifanya ivume zaidi, baada ya Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde (pichani), kulipuka bungeni: “Humuhumu ndani kuna wabunge wanawake wenye mimba zisizotarajiwa.”
Lusinde, alitamka hayo Aprili, mwaka huu, wakati akichangia hotuba ya bajeti, Ofisi ya Waziri Mkuu, kipindi ambacho bunge lilikuwa limechafuka kutokana na wabunge kurushiana ‘mipasho’ wao kwa wao.
Kauli ya Lusinde, pamoja na kupokelewa tofauti na wabunge wengi wanawake, wakidai mheshimiwa mwenzao amewadhalilisha, upande mwingine, katika ‘vikao vya kwenye korido’, matukio ya vicheko na kugonga mikono yalitawala na kunena kwa msisitizo “message delivered”, yaani ujumbe umefika.
Wakati mwandishi wetu akifuatilia sakata lenyewe, mbunge mwingine wa Viti Maalum (CCM) ambaye jina lake tunaliweka kabatini, aliamua kufunguka: “Nashangazwa sana na haya madai, tunawasema wapinzani, wakati hata kwetu (CCM) kuna watu wamepeana mimba.”

JESHI LA POLISI LAWASWEKA RUMANDE POLISI 16 KWA MAGENDO JIJINI DAR ES SALAAM


Mkuu wa jeshi la polisi,Said Mwema 
DAR ES SALAAM. 

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata askari wake 16 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kushiriki na kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa magendo wanaovusha bidhaa zao kupitia bandari bu
bu kandokando ya Bahari ya Hindi na maeneo mengine.
Hatua hiyo umekuja baada ya kubaini baadhi ya askari wa vikosi mbalimbali ambao imeelezwa kuwa wametengeneza mtandao huo ulioanzishwa zaidi ya miezi sita kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao hukusanya fedha kinyume cha sheria kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa ushuru halali Serikalini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema: "Tumeshirikiana na wananchi kwa kufuatilia nyendo za askari hao na kubaini kuwa walitengeneza mtandao huo wa kuvusha mali kupitia bandari bubu zisizo rasmi maeneo ya Kawe hadi Bagamoyo."

Alisema polisi kupitia teknolojia ya kisasa iliwabaini askari hao kwa nyakati mbalimbali wakishirikiana na wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakitoa rushwa ili wasikamatwe.
“Mpaka sasa askari wa vyeo mbalimbali waliokamatwa wako 16 na wanaendelea kuhojiwa... majina yao yanahifadhiwa kwa sasa kwani bado kuna wengine wanatafutwa ili kuwabaini na kuusambaratisha mtandao mzima,” alisema.
Alisema mtu yeyote ambaye amefanya kosa ndani ya Jeshi la Polisi atachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani kama raia wengine.
Kamanda Kova alisema operesheni hiyo itawalenga wafanyabiashara, wafanyakazi wa TRA na wa taasisi nyingine watakaobainika kuhusika na mtandao huo.

KASHFA YA WABUNGE WA KIKE KUJICHUBUA YAIBUA MJADALA MZITO...!!

KUMBE! Baadhi ya wabunge wa kike ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatumia vipodozi vinavyochubua ngozi ya juu ya mwili ili wawe na mwonekano mweupe (kama wazungu). 
Kauli hiyo ya kushangaza ilitolewa bungni Mei 9, mwaka huu na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy wakati alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu udhibiti wa dawa kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Akizungumza bila kupepesa macho, Mheshimiwa Kessy  alisema kuwa baadhi ya waheshimiwa wa kike ndani ya mjengo wanatumia vipodozi ambavyo vina madhara makubwa kwa afya ya mtumiaji.

Grace Kiwelu.
MSIKILIZE KWA KINA
“Labda niseme tu TFDA wanapaswa kusimamia kuhakikisha vipodozi vyenye madhara haviingii nchini, watu wengi sana wanaathirika na kupata magonjwa ya kansa ya ngozi.
“Humu ndani (bungeni) wapo waheshimiwa ambao wanatumia vipodozi hivyo ambapo wanapokuja kuumwa serikali inapoteza fedha nyingi kwenda kuwatibia nje ya nchi,” alisema Kessy.
WABUNGE WAMEKASIRIKA?

ANGALIA PICHA ZA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MBALIZI MBEYA MMOJA AFARIKI PAPO HAPO NA WANNE MAJERUHI


MAREHEMU SELEMANI JUMA SELEMANI ALIYEKUWA TINGO WA LORI HILO AMEFARIKI PAPO HAPO 


AJALI HII IMETOKEA KWENYE MTEREMKO WA MBALIZI LORI HILO INA SEMEKANA LILIFELI BREKI

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 14.05.2013

01 3bf5a

4 2ae5d

REGINALD MENGI ATANGAZA DAU LA MILIONI MOJA KWA MTU ATAYEMTUMIA TWEET NZURI


Upo kwenye Twitter? Kama haupo fanya haraka ujiunge sababu kuna ulaji huko!! Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema kuanzia mwezi huu, atakuwa akitoa shilingi milioni 1 kwa kila tweet itakayomfurashia.

mengi2
Not to fast though…… Sio tweet zile za ‘I’m having fun being single, #TeamSingle, tupa kuleee! 

Mengi anataka ulikune jicho lake kwa tweet yenye akili ambayo inaweza kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupunguza umaskini uliokithiri nchini.
  
“Umaskini umekuwa sugu. Kwa mwaka 1 anzia Mei ntatoa sh 1m kila mwezi kwa tweet nitakayochagua kuwa bora kushinda vita na umaskini,” ametweet leo.
  
Ameongeza kuwa Tweet hiyo iende kwake, yaani mtu akiandika tweet afanye kummention ili aione. 

AJALI YA COASTER NA LORI YAUA ABIRIA MMOJA AFARIKI DUNIA WENGINE 17 WAKIJERUHIWA WILAYA RUNGWE MKOANI MBEYA.

GARI YA AINA YA COSTA T 399 AUD ILIYOGONGWA KWA NYUMA NA KISHA KUPINDUKA ENEO LA KANYEGELE UWANJA WA NDEGE WILAYANI RUNGWE

HUU NI UPANDE WA NYUMA WA COSTA HIYO 

HILI NDILO ROLI LILILO IGONGA COSTA KWA NYUMBA NA KUSABABISHA AJALI HIYO NAMBARI YA ROLI T 712 CZC NA TELA LENYE NAMBALI T 444 CCZ LIKIWA NA SHEHENA YA MBOLEA

MSANII WA BONGO MOVIE ATAFUTA MUME WA KUMZALISHA


Baada ya kuadimika kwa muda mrefu, mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aisha Bui ameibuka na kusema kuwa anatafuta mwanaume ambaye atamzalia mtoto na hatimaye waoane ila akadai wa kumuoa kwa sasa hamuoni

Akizungumza na mwandishi wetu,  Aisha amefunguka kuwa alikuwa kimya kwa sababu kuna mambo alikuwa akifanya.

Alisema kwa kuwa ameyakamilisha, sasa ana nafasi ya kusaka mtoto iwapo atampata mwanaume sahihi.

Aisha amevitaja vigezo vya mwanaume wa kumzalia kuwa amjengee nyumba ya kuishi yeye na mtoto wake kisha awe na uwezo wa kumlea na kumpatia elimu bora.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...