Saturday, July 26, 2014

BASI LA HOOD LAPATA AJALI ASUBUHI YA LEO LIKITOKEA MBEYA


Muda mchache baada ajali kutokea. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
 Askari wa usalama wa barabarani wakiwa wamefika eneo la tukio  na baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo

SUDAN KUSINI YAKABILIWA NA BAA LA NJAA

Baa la njaa nchini Sudan Kusini

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini kama mbaya zaidi kuwahi kuonekana duniani na kuyataka mataifa ambayo yaliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dola millioni mia sita kutoa fedha hizo.
Limeonya kuwa vita vinavyoendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi huenda vikasababisha baa la njaa nchini humo.
Shirika la chakula duniani WFP limesema kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa watoto elfu hamsini huenda wakapoteza maisha yao kutokana na utapia mlo mwaka huu huku thuluthi moja ya raia wakikabiliwa na na viwango hatari vya njaa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

REINA ATHIBITISHA KUPENDA KUENDELEA KUICHEZEA LIVERPOOL

438662_heroa
MLINDA mlango wa Liverpool, Pepe Reina amejitia kitanzi mwenyewe katika klabu hiyo, licha ya kudai anapenda kustaafu soka la kimataifa nchini Hispania.
 Akicheza kwa mkopo Seria A katika klabu ya Napoli msimu uliopita-Reina alianza kuhusishwa kujiunga na bosi wake  wa zamani wa Anfield Rafael Benitez-na kuzua maswali juu ya hatima yake Liverpool.
 Reina amesisitiza kuwa anaheshimu mkataba wake Anfield-ambao utamalizka mwaka 2016 kabla ya kwenda nchini Hispania.
 “Nina mkataba ambao nahitaji kuuheshimu Liverpool,” Reina aliiambia radio ya Hispania ya Cadena Ser. “Ninafanya mazoezi vizuri na nipo sawa na wachezaji wenzangu”.
 “Nipo hapa kwa ajili ya kukaa”.
 “Sijazungumza na Brendan Rodgers, ni siku nne tu tangu nifike hapa, naangalia kufanya mazoezi vizuri ili kurudi katika kiwango changu”.
 Reina mwenye miaka 31 alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Barcelona, kabla ya kwenda Villarreal na kuelekea ligi kuu nchini England, na sasa amekiri kuwa kurudi La Liga itakuwa nafasi nzuri kwake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
 “Nimekuwa nikiwaza hili kwa muda mrefu kuwa ni vizuri kurudi ulipotoka,” Reina aliongeza.
 “Wakati Rafa Benitez ananisajili Liverpool mwaka 2005, nilikubali na nilisema nitarudi Hispania baadaye”.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 26, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC01150
DSC01151
DSC01152
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KATIBA MPYA NJIA PANDA, UKAWA WAAPA KUENDELEA KUSUSIA VIKAO

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta akisisitiza jambo juzi, baada ya mkutano wa Kamati ya Maridhiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. 

Wakati Bunge Maalumu la Katiba likiazimia kuzifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwabana wajumbe wa Bunge hilo ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), viongozi wa kundi hilo wamesema hawatishwi na uamuzi huo na kwamba wataendelea kususia vikao hivyo.
Kikao kilichokuwa kiwe cha mashauriano kilichoitishwa juzi na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta kiliazimia kuzifanya marekebisho baadhi kanuni za uendeshaji kwa lengo la kusimamia nidhamu wajumbe wake, hatua inayotafsiriwa kwamba inawalenga Ukawa.
Jana Sitta akizungumza na Mwananchi Jumamosi alisema mabadiliko yanayokusudiwa kufanywa yatahusisha masuala ya nidhamu, yakiwamo fujo na utoro, mambo ambayo hivi sasa hayawezi kudhibitiwa moja kwa moja na mwenyekiti wa Bunge hilo.
Sitta alikuwa akitoa ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake jana na kusomwa mbele ya waandishi wa habari na Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad, ikieleza maazimio ya kikao ya usuluhishi alichokuwa amekiitisha kwa ajili ya kutanzua mzozo unaotishia kukwama kwa mchakato wa Katiba Mpya.
Hata hivyo, Ukawa unaoundwa na wajumbe wa Bunge Maalumu kutoka Vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi, CUF na baadhi ya wajumbe kutoka Kundi la 201 walioteuliwa na Rais, walisusia kikao hicho na kusababisha uamuzi uliofikiwa kuwa wa upande mmoja. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

OKWI, KIIZA WAMPASUA KICHWA MAXIMO

 Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema mchezaji yeyote mwenye ubinafsi hana nafasi kwenye kikosi chake, huku akishindwa kujua yupi wa kumuacha kati ya wachezaji wawili wa kimataifa.
Akizungumza jana mara baada ya mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Loyola, Maximo alisema hadi sasa hajaamua wa kumuacha kati ya Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza.
“Kwa sasa siwezi kusema ninayemuacha hadi Septemba 17, nitatangaza nitakayemuacha, ila wachezaji wabinafsi hawatakuwa na nafasi katika kikosi changu.
“Nataka mchezaji anayejituma kwa moyo, anayepigania maslahi ya timu kwanza na si kukimbilia maslahi yake peke yake, tukiwa na umoja tunashinda pamoja, na kama tunapoteza tunaumia pamoja,” alisema Maximo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...