Saturday, July 26, 2014

SUDAN KUSINI YAKABILIWA NA BAA LA NJAA

Baa la njaa nchini Sudan Kusini

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini kama mbaya zaidi kuwahi kuonekana duniani na kuyataka mataifa ambayo yaliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dola millioni mia sita kutoa fedha hizo.
Limeonya kuwa vita vinavyoendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi huenda vikasababisha baa la njaa nchini humo.
Shirika la chakula duniani WFP limesema kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa watoto elfu hamsini huenda wakapoteza maisha yao kutokana na utapia mlo mwaka huu huku thuluthi moja ya raia wakikabiliwa na na viwango hatari vya njaa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...